Al Hilal anapoenda kutukung'uta mechi ijayo, naomba mtakapomtimua Gamondi timueni na wachezaji wafuatao

Al Hilal anapoenda kutukung'uta mechi ijayo, naomba mtakapomtimua Gamondi timueni na wachezaji wafuatao

Umeongea maoni yako ila hapo kwa Chadrack Boka na Khalid Aucho nadhani umekosea, Bila shaka umeona game ya leo bila hao watu + Clement Mzize game inapoa sana. Angalau ungesema Dube + Bacca watafutiwe mbadala. Kocha wa viungo na fitness naye anapwaya sana, wachezaji hawako fit kabisa, Kabla ya hii mechi, Manager na benchi lote la ufundi ilipaswa kupata mechi moja ya kirafiki ili kocha mpya awatambue wachezaji na wachezaji wawe fit, Jambo ambalo halikufanyika. Anahitajika striker mbadala wa Dube, na Namba 9 hatari kama Mayele. Kingine ni ari ya uchezaji ipo chini sana,ambayo inaweza kubadilishwa wakija wachezaji wapya dirisha dogo. Hayo tu, YANGA BINGWA.
 
Umeweka hiyo list yote ya wachezaji Wa kigeni, Je unazijua Sheria za TFF kuhusu namba ya wachezaji Wa kigeni wanapaswa kuwa kwenye team husika?

2. Je hiyo list uliyoweka na Ukasisitizia na wawe na uzoefu Wa kutosha na Ubora WA Kiwango cha Juu, Je Umefikia kuhusu gharama zao za usajili na mshahara Yao kuwalipa???

Yangu ni Hayo Tu.
"Daima mbele, Nyuma mwiko"
 
Umeweka hiyo list yote ya wachezaji Wa kigeni, Je unazijua Sheria za TFF kuhusu namba ya wachezaji Wa kigeni wanapaswa kuwa kwenye team husika?

2. Je hiyo list uliyoweka na Ukasisitizia na wawe na uzoefu Wa kutosha na Ubora WA Kiwango cha Juu, Je Umefikia kuhusu gharama zao za usajili na mshahara Yao kuwalipa???

Yangu ni Hayo Tu.
"Daima mbele, Nyuma mwiko"
Kwani ubora hua unaangalia gharama au kuscout kipaji..? Kuna wachezaji wamekuja hawana majina na kwa bei chee tu lakini ndo wanafanya mabalaa...
Mayele, maxi, yao, Tadeo Lwanga, Kipre Jr ni mfano wao
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane !

Tarehe 26 ni siku ambayo timu yangu ya Yanga unakwenda Kucheza mechi ya kwanza ya michuano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Hilal Omdurman,siku hii naelewa kabisa Yanga atafungwa si chini ya Goli 3 na ndiyo siku ambayo kocha Gamondi anaenda kutimuliwa rasmi!

Binafsi nilionya sana na nikapendekeza ya kwamba,baada ya kipigo Cha goli 3 kutoka Kwa walina Asali wa Tabora,ilipaswa Kocha Gamondi asikanyage tena Avic town,ilipaswa abebwe kwenye Guta na mabegi yake arudishwe kwao!

Kwakuwa mmejifanya kichwa ngumu na kuendelea kumuamini kocha ambaye mbinu zimemuishia,naamini hiyo Tarehe 26 mtatafutana pale Taifa!

Siku hiyo mtakapoamua kumfurusha Gamondi baada ya kipigo Cha aibu kutoka Kwa Al Hilal naomba na wachezaji wafuatao wasirudi Avic town,tena wakati wa kwenda Taifa waende na virago vyao wakiwa tayari Kwa safari!

1. AZIZ Ki
Huyu jamaa kwasasa hapaswi kabisa kuvaa kitu chochote chenye nembo ya Yanga !

Tulimng'ang'ania Kwa nguvu zote akaongeza mkataba Kwa gharama kubwa lakini anachokifanya uwanjani akiendani na malipo anayopewa!,Pesa anayolipwa ni heri akaongezewa mshahara Maxi Mpira Nzengeli

Yeye aende akavute shisha vizuri huko Burkinafaso na ikiwezekana aondoke na Malaya wake Hamisa!

Msipomtimua siku hiyo basi Hersi ajiandae kuiachia timu,hatuwezi kuvumilia huu ujinga Kwa wachezaji wasiokuwa na nidhamu halafu mkawachekea tu!

Ronaldo umri umeenda lakini pumzi aliyonayo Huwezi linganisha na hizi takataka kwasababu jamaa ana nidhamu binafsi na amejiweka kando na mambo ya kijinga!

Mbona kabla ya kuongezea mshahara hakuwahi kufanya huu ujinga?,chezaji gani kila siku lenyewe ni klabu tu kuelewa na kuvuta shisha?

2. CHADRACK BOKA
Huyu siku hiyo ya mechi pia anapaswa kwenda na Virago vyake Taifa,baada ya kipigo apandishwe Lori linaloelekea Tunduma,akifika Tunduma apandishwe gari la Sumbawanga hadi Kabwe,akifika Kabwe apandishwe mtumbwi kuelekea kwao Congo

Hatuwezi Kuwa na Mchezaji anachojua yeye ni mbio tu na siyo tekniki za mpira,huyu jamaa kipaji Chake siyo mpira Bali ni riadha,huku kwenye Mpira kavamia tu,kwenye riadha angefanya vema zaidi kuliko huku kwenye kabumbu!

Nitashangaa sana siku hiyo akiondoka Gamondi na huyu akibaki,nitashangaa sana!

3. KHALID AUCHO
Huyu yeye kwakuwa hapo Uganda ni Jirani,ni vema nae siku hiyo akaja na furushi lake la Virago kwasababu baada ya mechi inapaswa apandishwe Lori linaloelekea Uganda kupitia Mutukula!,hapaswi kupanda ndege kwasababu itakuwa ni uharibifu wa rasilimali fedha!

Hatuwezi Kuwa na Mchezaji ambaye anatumia nguvu nyingi kuliko Akili,kila uchwao anapokuwa kiwanjani badala ya Kuwa mfano Kwa wachezaji wenzie yeye anajifanya mwehu!,kama anazo nguvu ni vema akaenda Kucheza mieleka na kina John Cena lakini kwenye Mpira hizo nguvu hatuzihitaji!
Badala aboreshe kiwango Chake,yeye kaboresha matumizi ya nguvu kupita kiasi!

4. KENNEDY MUSONDA
Hakuna mchezaji niliyekuwa nikimkubali na kumpenda kama huyu Musonda,lakini Ujio wa Gamondi umeua kiwango Chake kabisa!

Nadhani ni muda muafaka kuachana naye ili akayaanze maisha mapya sehemu nyingine,TP Mazembe walimuhitaji sana jamaa sema ndiyo hivyo wamefungiwa kufanya usajili lakini naamini wakifunguliwa bado atakuwa na nafasi ya kwenda huko na kufanya vizuri!

Baada ya hiyo safisha safisha ya wachezaji hao,tutapaswa kufanya usajili wa wachezaji wafuatao;

1. Goli kipa wa ziada mwenye uzoefu mkubwa kutoka nje

2. Beki namba 2 mwenye uzoefu mkubwa kutoka ndani

3. Beki namba 3 mwenye uzoefu mkubwa kutoka nje

4. Beki namba 5 mwenye uzoefu mkubwa kutoka ndani

5. Kiungo mkabaji

Alikamwe najua upo humu na unapitia hili Jukwaa,tafadhali lichukue kama lilivyo umuonyeshe Hersi!
Acha wenge
 
Back
Top Bottom