Al Hilal anapoenda kutukung'uta mechi ijayo, naomba mtakapomtimua Gamondi timueni na wachezaji wafuatao

Al Hilal anapoenda kutukung'uta mechi ijayo, naomba mtakapomtimua Gamondi timueni na wachezaji wafuatao

Nsikuchoshe na Usinchoshe, Tusichoshane !

Tarehe 26 ni siku ambayo timu yangu ya Yanga unakwenda Kucheza mechi ya kwanza ya michuano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Hilal Omdurman,siku hii naelewa kabisa Yanga atafungwa si chini ya Goli 3 na ndiyo siku ambayo kocha Gamondi anaenda kutimuliwa rasmi!

Binafsi nilionya sana na nikapendekeza ya kwamba,baada ya kipigo Cha goli 3 kutoka Kwa walina Asali wa Tabora,ilipaswa Kocha Gamondi asikanyage tena Avic town,ilipaswa abebwe kwenye Guta na mabegi yake arudishwe kwao!

Kwakuwa mmejifanya kichwa ngumu na kuendelea kumuamini kocha ambaye mbinu zimemuishia,naamini hiyo Tarehe 26 mtatafutana pale Taifa!

Siku hiyo mtakapoamua kumfurusha Gamondi baada ya kipigo Cha aibu kutoka Kwa Al Hilal naomba na wachezaji wafuatao wasirudi Avic town,tena wakati wa kwenda Taifa waende na virago vyao wakiwa tayari Kwa safari!

1. AZIZ Ki
Huyu jamaa kwasasa hapaswi kabisa kuvaa kitu chochote chenye nembo ya Yanga !

Tulimng'ang'ania Kwa nguvu zote akaongeza mkataba Kwa gharama kubwa lakini anachokifanya uwanjani akiendani na malipo anayopewa!,Pesa anayolipwa ni heri akaongezewa mshahara Maxi Mpira Nzengeli

Yeye aende akavute shisha vizuri huko Burkinafaso na ikiwezekana aondoke na Malaya wake Hamisa!

Msipomtimua siku hiyo basi Hersi ajiandae kuiachia timu,hatuwezi kuvumilia huu ujinga Kwa wachezaji wasiokuwa na nidhamu halafu mkawachekea tu!

Ronaldo umri umeenda lakini pumzi aliyonayo Huwezi linganisha na hizi takataka kwasababu jamaa ana nidhamu binafsi na amejiweka kando na mambo ya kijinga!

Mbona kabla ya kuongezea mshahara hakuwahi kufanya huu ujinga?,chezaji gani kila siku lenyewe ni klabu tu kuelewa na kuvuta shisha?

2. CHADRACK BOKA
Huyu siku hiyo ya mechi pia anapaswa kwenda na Virago vyake Taifa,baada ya kipigo apandishwe Lori linaloelekea Tunduma,akifika Tunduma apandishwe gari la Sumbawanga hadi Kabwe,akifika Kabwe apandishwe mtumbwi kuelekea kwao Congo

Hatuwezi Kuwa na Mchezaji anachojua yeye ni mbio tu na siyo tekniki za mpira,huyu jamaa kipaji Chake siyo mpira Bali ni riadha,huku kwenye Mpira kavamia tu,kwenye riadha angefanya vema zaidi kuliko huku kwenye kabumbu!

Nitashangaa sana siku hiyo akiondoka Gamondi na huyu akibaki,nitashangaa sana!

3. KHALID AUCHO
Huyu yeye kwakuwa hapo Uganda ni Jirani,ni vema nae siku hiyo akaja na furushi lake la Virago kwasababu baada ya mechi inapaswa apandishwe Lori linaloelekea Uganda kupitia Mutukula!,hapaswi kupanda ndege kwasababu itakuwa ni uharibifu wa rasilimali fedha!

Hatuwezi Kuwa na Mchezaji ambaye anatumia nguvu nyingi kuliko Akili,kila uchwao anapokuwa kiwanjani badala ya Kuwa mfano Kwa wachezaji wenzie yeye anajifanya mwehu!,kama anazo nguvu ni vema akaenda Kucheza mieleka na kina John Cena lakini kwenye Mpira hizo nguvu hatuzihitaji!
Badala aboreshe kiwango Chake,yeye kaboresha matumizi ya nguvu kupita kiasi!

4. KENNEDY MUSONDA
Hakuna mchezaji niliyekuwa nikimkubali na kumpenda kama huyu Musonda,lakini Ujio wa Gamondi umeua kiwango Chake kabisa!

Nadhani ni muda muafaka kuachana naye ili akayaanze maisha mapya sehemu nyingine,TP Mazembe walimuhitaji sana jamaa sema ndiyo hivyo wamefungiwa kufanya usajili lakini naamini wakifunguliwa bado atakuwa na nafasi ya kwenda huko na kufanya vizuri!

Baada ya hiyo safisha safisha ya wachezaji hao,tutapaswa kufanya usajili wa wachezaji wafuatao;

1. Goli kipa wa ziada mwenye uzoefu mkubwa kutoka nje

2. Beki namba 2 mwenye uzoefu mkubwa kutoka ndani

3. Beki namba 3 mwenye uzoefu mkubwa kutoka nje

4. Beki namba 5 mwenye uzoefu mkubwa kutoka ndani

5. Kiungo mkabaji

Alikamwe najua upo humu na unapitia hili Jukwaa,tafadhali lichukue kama lilivyo umuonyeshe Hersi!
Ungetangaza kugombea urais wa Yanga na hizi ndiyo zikawe sera zako, kinyume na hapo umeamua kutengeneza comedy tu.
Pamoja na kuuona uzi huu kama comedy, ninapokubaliana na wewe ni sehemu moja tu ya Aziz K.
 
Hii mechi nyepesi sana kwa Yanga tarehe 26.11 amini hilo
Mechi nyepesi sana kwa yanga amini usiamini
🤣🤣🤣ninyi na kocha wena hakuna heshima na timu pinzani kazi kujificha kwenye kivuli cha tunawaheshimu wapinzani ila ndani kocha ana dharau sanaa ndio maana wanamkanda tu sahivi
 
Tarehe 26 wachezaji wa Yanga watazawadiwa sana kadi za njano na hawa (Job,Bacca,Aucho ) mmoja wao anaweza pewa red.
Dube atasema goli halipo
 
ko umguhaka hadithi umemaliz umehamia kweny mpira ongeza na dube na beleke kama vifungashio hatuwez kuwa na wachezaji hawajui kufunga mpk wapate magoli ya offside au penalty kama huyo dube wamroge asione aone mawe ili aondoke ana laana za azam kingine tuache uchawi sisi yanga na kuchoma sondano tutawaumiz watoto wa mo dewji aisee
 
Nimeamini ushabiki wa mpira hapa bongo kwa sasa umevamiwa na wapuuzi hasa kutoka mikoani, walioanza kuziona Yanga na Simba kupitia Azam tv.

Yani kupoteza mechi mbili tu, tayari anatokea mtu na dela lake mkononi hata kuchamba haja chamba anataka Gamondi afukuzwe.
Usikute hata kadi ya uanachama ya Yanga hana, achiliambali kwenda uanjani.

Ayah bhana, muna uhuru wa kuongea chochote.
 
Mkuu Sasa wewe unaujua mpira gani? Au mpaka Gamondi aingiziwe Vidole matakoni ndo uelewe uwezo wake umefika mwisho?

Kwani tarehe 26 mbali?,mashabiki wapumbavu na Wajinga kama wewe ndiyo mtaelewa ninachokimaanisha hapa!
 
ko umguhaka hadithi umemaliz umehamia kweny mpira ongeza na dube na beleke kama vifungashio hatuwez kuwa na wachezaji hawajui kufunga mpk wapate magoli ya offside au penalty kama huyo dube wamroge asione aone mawe ili aondoke ana laana za azam kingine tuache uchawi sisi yanga na kuchoma sondano tutawaumiz watoto wa mo dewji aisee
Makolokwinyo mna matatizo ya kiakili!
 
Nimeamini ushabiki wa mpira hapa bongo kwa sasa umevamiwa na wapuuzi hasa kutoka mikoani, walioanza kuziona Yanga na Simba kupitia Azam tv.

Yani kupoteza mechi mbili tu, tayari anatokea mtu na dela lake mkononi hata kuchamba haja chamba anataka Gamondi afukuzwe.
Usikute hata kadi ya uanachama ya Yanga hana, achiliambali kwenda uanjani.

Ayah bhana, muna uhuru wa kuongea chochote.
Achana na hao mataira mkuu
 
Mechi 2 tu kushindwa maneno mengi ata yasokua na maana
Ndo maana watanzania wengi ni maskini sabu sio wavumilivu wanakata tamaa mapema na wanataka matokeo mazuri tu kwa kila kitu anachokifanya

Wakat mambo hayaendi ivyo ukifungwa unarudi mnakaa km timu mnajadili makosa ndo mpira ulivyo Man city kapoteza mechi 3 mfukulizo hujaona mashabiki wakilalamika wala kuleta shutuma za kuduanzi

Wabongo tujifunze mpira lakin pia tujipe kaz za kufanya maana ukiwa huna kaz ya kufanya akili na mawazo yako yote ni kuwaza mpira na kutafta furaha kutoka kwenye mpira wakat furaha inapatikana ktk vitu kibao
 
Herse atuachie timu wakat hata uwakika wa kula wiki nzima huna ata ukipewa kibabage ama nkane umlipe mshahara mwezi mmoja huwezi
 
Shabiki wa kweli wa mpira hatarajii matokeo mazuri tu, kwa sababu hakuna timu isiyofungika duniani.

Pia wachezaji sio maroboti, hivo kupitia ups & down ni jambo la kawaida, tusiudharau mchango wa ki ktk tim yetu, kisa hafanyi vzr kwa sasa.

Nb: mleta mada punguza mdomo.
 
Back
Top Bottom