Al Qaeda yaitisha Tanzania

Al Qaeda yaitisha Tanzania

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
010812.jpg



ALHAMISI, SEPTEMBA 26, 2013 04:09 NA SARAH MOSSI

*Yajigamba kufanya mashambulio muda wowote
*Watanzania wapewa mafunzo ya ugaidi nje ya nchi
*Polisi nchini wasema vyombo vya ulinzi viko macho
*Mtanzania akamatwa Kenya akihofiwa gaidi

WAKATI wananchi wa Afrika Mashariki wakijawa na hofu ya mashambulio yanayopangwa kufanywa na vikundi vya ugaidi vya Al Qaeda na Al Shabab, imebainika kuna Watanzania waliopewa mafunzo ya ugaidi wanaojiandaa kufanya maovu.

Hayo yamebainika siku chache baada ya wanamgambo wa kundi la Al Shabab kufanya mashambulio katika Jengo la Biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya 70 na kuacha mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Mkuu wa Interpol Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na MTANZANIA.

Alikuwa akizungumzia kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab aliyetoa tahadhari kwamba kundi lake linapanga mashambulio mengine Tanzania na Uganda.

Babile alisema taarifa zinaonyesha vijana wa Tanzania waliojiunga na mafunzo ya ugaidi yanayotolewa na vikundi vya Al Qaeda na Al Shabab, wamefanya hivyo baada ya kushawishiwa watapata utajiri wa haraka.

Alisema hali hiyo imevifanya vyombo vya ulinzi na usalama nchini kutoipuuza kauli hiyo ya Sheikh Abdulaziz Abu Muscab.

“Tunajua wapo Watanzania wanapewa dozi za ugaidi, na sisi siyo kisiwa, watu ni hao hao… tumejipanga kuyakabili haya na kuushirikisha umma katika ulinzi,” alisema.

Babile alisema kauli ya msemaji wa kundi la Al Shabab ya kuivamia Tanzania siyo ya kupuuza na kusisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama nchini viko tayari kukabiliana na lolote litakalotokea.

“Tumeisikia kauli yake kwenye mitandao ya jamii, imetufanya kuwa alert (macho) vya kutosha, imetuweka sawa na imetukumbusha kuwa tunaweza kuvamiwa wakati wowote.

“Hatuja-relax hata kidogo, tumejiweka sawa kwenye human resources zetu, materials resource na hata frontline officers wetu wako makini mno.

“Mfano kwenye viwanja vya ndege ambako ni muhimu, kuna mitambo inayoweza kugundua hati za kusafiria za washukiwa wa uhalifu wanaotafutwa kimataifa na tutawakamata tu.

“Lakini hata kwenye mipaka yetu yote hatuko peke yetu, tumepanua wigo wa kupata taarifa za kiintelijensia na katika kufanya kazi hii tunashirikiana na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” alisema.

Baada ya kufanya mashambulio mjini Nairobi Jumamosi iliyopita, Msemaji wa Al Shabab, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, aliripotiwa kwenye mitandao ya jamii akisema shambulio hilo lilikuwa ni la kulipiza kisasi baada ya majeshi ya Kenya kuvamia kundi hilo lenye makazi yake mjini Kismayu, Somalia.

Mitandao ya jamii pia ilimnukuu Sheikh Abu Muscab akijigamba kuwa wakati wowote mashambulio ya kikundi hicho yataelekezwa Uganda na Tanzania.

Wakati huohuo, Babile amesema Mtanzania mmoja alikamatwa Kenya akishukiwa kuwa ni mmoja magaidi waliovamia jengo la Westgate.

Bila kumtaja jina, alisema mtu huyo ni mkazi wa Arusha na alikamatwa muda mfupi baada ya kuingia Kenya akitoa Tanzania, akitumia usafiri wa mabasi ya abiria.

“Walipomkamata wakatuletea taarifa sisi, tukatafuta kwenye database zetu na information za ndani zikatuonyesha hakuwa mtu hatari, tukamuachia.

“Kilichowatia hofu na kumshuku mtu huyu ni muda alioingia Kenya na muda wa tukio lilipotokea… lakini tumeangalia taarifa zote tukagundua hakuwa na shaka,” alisema Babile.


[h=4][/h]
 
Je wameelezwa kwa nini Tanzania inataka kushambuliwa? maana makundi ya kigaidi hayashambulii tu bila ya sababu
 
haya sasa sisi TZ tumewakosea nini?
Maana Kenya na UG wanasema sababu wamepeleka majeshi Somalia. watutajie basi na sababu ya kuvamia TZ. Ukichunguza hawa watu wameamua tu Dunia isitawalike baaaaasi, hawana sababu za msingi, they are MONSTERS period!
 
what is the motive behind their attack maana ya kenya walitoa sababu...sasa sisi hapa tunahusikaje?? msaada plizz au ndo kutaka kuuza magazeti
 
Ndio hapo sasa... Tanzania ina issue gani na Al Qaeda kushambuliwa? Au tu kwasababu ni SOFT TARGET? Lakini kama kweli wao ni SUNNI na wanajali Damu ya Waislamu Tanzania watu watatu wakipita mmoja ni Mwislamu Sunni kwahiyo hawata wajali hao?
 
what is the motive behind their attack maana ya kenya walitoa sababu...sasa sisi hapa tunahusikaje?? msaada plizz au ndo kutaka kuuza magazeti

Mkuu, njaa inauma kweli. wanatafuta namna ya kushiba
 
Wao kenya walidai wameishambulia kwa kuwa imepeleka majeshi somalia, haya na Tanzania wanaidai nini? Au ndio kutaka kuwasilimisha watanzania wote? Basi wanapenda kuona damu za watu wasio na hatia! Kisa ni dini sio? He kwa Tanzania watachemsha,na kuanzia sasa wale wenye midevu na suruali fupi tuwachunguze sana nyendo zao kila siku!
 
Ndio hapo sasa... Tanzania ina issue gani na Al Qaeda kushambuliwa? Au tu kwasababu ni SOFT TARGET? Lakini kama kweli wao ni SUNNI na wanajali Damu ya Waislamu Tanzania watu watatu wakipita mmoja ni Mwislamu Sunni kwahiyo hawata wajali hao?

Vice verse. Tanzania watu watano wakipita basi WATATU ni waislamu
 
Hivi gazeti hili lina uhusiano wowote na Mwananchi Communications yenye damu na propaganda za kwao Kenya?
 
Tanzania tunajipiga wenyewe kwa kisingizio cha ugaidi. Arusha nani alirusha yale mabomu? Gongo la mboto na mbagala?

Wenyewe watuambie, siku wanayalipua tukae nyumbani wasitutie jamba jamba. Hata kama wanateka eneo watutoe kwanza ndio wateke vitu.

Afu hawa Mtanzania si ndio walisema 'serikali imejaa damu?' Siamini cha al qaeda wala al shabab. Masogange mwenyewe imegeuka kuwa dawa za kuua magugumaji ziwa Victoria, alitumwa kuzipeleka maabara ya uhakiki Sauzi.
 
Back
Top Bottom