Unakaa haukumbuki kuanzia 2005-2011 port ya mombasa ilikua iko karibu kuwa unviable, tulikua tunalipishwa tax kwa bidhaa yoyote eti cost of insuarance kwasababu ya piracy....... meli zilikua zinatekwa nyara karibu kila mwezi, pirates hawa walikua wanafanyikiwa sababu ndani ya somalia ilikua hakuna serikali, kwahivyo wakichoka wanarudi ndani ya somalia na kupumzika.....
alafu umesahau alshabaab wakivamia vituo vya utalii karibu na mipaka?
pia umesahau wakati huo ndo tulikua tunaanza project ya lapsset ambayo ni project ya $29B na wawekezaji walikataa juwekeza kama somalia next door iko unpredictable?????
Umesahau kabla kenya kuingia somalia tulizunguka dunia nzima tukiomba nchi za kimataifa kuisadia somalia kwani ilikua inatudhuru kiuchumi.... na huo mda wote walikua hawatusikizi,
Kenya haiwezi endelea na project zake za kiuchumi ikiwa somalia ingeendelea bila serikali, mwishowe tungerudi pale pale tu, afadhali tuishughulikie somalia once and for all, wasije tupatia shida mbeleni wakati tumeshawekeza mabilioni ya pesa karibu na mipaka ya somalia
Kumbuka somalia haikuingilia kenya kwa miaka 30,walikua hawatudhuru sana kuisalama, tulikua tunaweza kuvumilia mahamia wakivuka mpaka kila siku....lakini ikazidi ikawa hatuna usalama tena, wakaanza kuteka nyara hadi wafanyikazi wa aid org