Alaah, Fariki usemwe!

Alaah, Fariki usemwe!

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Waswahili waliwahi kunena kuwa....kufa ili usemwe, haijalishi ni kwa ubaya au uzuri, ilimradi usemwe tu kwa sababu huwezi kujibu chochote.

Hivi ni kweli JPM kwa kipindi chake cha miaka 5 alikopa zaidi ya Trillion 29? Hizi pesa pamoja na miradi yote hii aliyoacha ambayo kwa kiasi kikubwa haijakamilika, hizi pesa zote alikopaje? Alikua anamtuma nani wakati alikua hatembezi bakuli nje yeye? Ama mabakuli yalikua yanakuja mwenyewe?

Ilikua awamu ya 5 wakafanya kisasa kiasi hicho kuwadanganya wananchi kua miradi yote hiyo ilikua ikijengwa kwa pesa za ndani? Trillion 29 kwa miaka 5, angekaa miaka 10 ingekuwaje? Deni zili lingefikia trillioni 100 sasa? Yaani JK aliye kaa madarakani miaka 10 pamoja na kuzunguka kwake kote na mtandao wa barabara kuunganisha mikoa yote nchi nzima lakini deni lake halikufikia la mwendazake la miaka 5?

Uchumi wa kati uliokua unatangazwa kwa nguvu kubwa leo hii uko wapi?
Huenda taifa hili linakwama kwa sababu ya unafki mkubwa wa baadhi ya viongozi ambao hawako tayari kusema kweli. Watu wapo tayari kulinda matumbo yao kuliko utaifa wao.
 
Hoja ninini?
Huamini kama alikopa?
Hujui alikopaje?
Miaka kumi ingekuaje?
Give fact... give opinion!!
Hoja yamashaka haifai kujadiliwa haina misingi yakujadiliwa
 
Wajanja wamekopa wakatia mfukoni fasta fasta alafu deni wakalisukumia kwa utawala wa jiwe kwa vile amelala usingizi na mababu zake, hawa akina mkwere hao siyo watu wema kabisa
 
wanasema ukweli una kawaida ya kuchelewa.

acha wajambe jambe kueneza propaganda zao za maandazi,mpaka 2025 watakuwa wanapigwa mawe wakipita kama ilivyokuwa 2015.
 
Yaani JK aliye kaa madarakani miaka 10 pamoja na kuzunguka kwake kote na mtandao wa barabara kuunganisha mikoa yote nchi nzima lakini deni lake halikufikia la mwendazake la miaka 5?
shooketh-computer.gif

Ebwanaee!! yule Interahamwe aliku wa Mwizi wa hataree!
 
Waswahili waliwahi kunena kua....kufa ili usemwe, haijalishi ni kwa ubaya au uzuri, ilimradi usemwe tu kwa sababu huwezi kujibu chochote.

Hivi ni kweli JPM kwa kipindi chake cha miaka 5 alikopa zaidi ya Trillion 29? Hizi pesa pamoja na miradi yote hii aliyoacha ambayo kwa kiasi kikubwa haijakamilika, hizi pesa zote alikopaje? Alikua anamtuma nani wakati alikua hatembezi bakuli nje yeye? Ama mabakuli yalikua yanakuja mwenyewe?

Ilikua awamu ya 5 wakafanya kisasa kiasi hicho kuwadanganya wananchi kua miradi yote hiyo ilikua ikijengwa kwa pesa za ndani? Trillion 29 kwa miaka 5, angekaa miaka 10 ingekuwaje? Deni zili lingefikia trillioni 100 sasa? Yaani JK aliye kaa madarakani miaka 10 pamoja na kuzunguka kwake kote na mtandao wa barabara kuunganisha mikoa yote nchi nzima lakini deni lake halikufikia la mwendazake la miaka 5?

Uchumi wa kati uliokua unatangazwa kwa nguvu kubwa leo hii uko wapi?
Huenda taifa hili linakwama kwa sababu ya unafki mkubwa wa baadhi ya viongozi ambao hawako tayari kusema kweli. Watu wapo tayari kulinda matumbo yao kuliko utaifa wao.
Hawakusema kuwa ni pesa za mikopo bali za ndani!
 
Back
Top Bottom