Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Albania imeweka rekodi ya dunia kwa kuwa nchi ya kwanza kuteua waziri aliyeundwa kwa akili bandia (AI), siyo waziri wa teknolojia ya AI, bali waziri halisi wa kidijitali, aliyeundwa kwa misimbo na kuendeshwa na mfumo wa kisasa wa akili bandia.
Jina lake ni Diella, linalomaanisha ‘mwanga wa jua’ kwa Kialbania ndilo jina la roboti, atasimamia shughuli zote za manunuzi ya umma, kama alivyoeleza Waziri Mkuu Edi Rama.
Aliteuliwa rasmi Alhamisi ya Septemba 11, 2025, ambapo Rama alimtambulisha kama ‘mwanachama wa baraza la mawaziri asiye na uwepo wa kimwili’, ambaye atahakikisha kuwa zabuni za umma zitakuwa huru kwa asilimia 100 dhidi ya ufisadi.
Wakati wa majira ya kiangazi, Rama alidokeza kuwa siku moja Albania inaweza kuwa na waziri wa kidijitali hata Waziri Mkuu wa AI, lakini ni wachache waliotarajia hatua hiyo itachukuliwa haraka kiasi hiki.
Kwenye mkutano wa Chama cha Kijamaa uliofanyika katika mji wa Tirana, Rama alitangaza mawaziri waliobaki na waliokatwa, alimtambulisha pia Diella mwanachama pekee wa Serikali asiye binadamu.
“Diella ni mwanachama wa kwanza wa baraza la mawaziri asiye na uwepo wa kimwili, bali aliyeundwa kwa akili bandia,” aliwaambia wanachama wa chama hicho.