Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert John Chalamila umemsikia live Mstaafu Kikwete akikuita muongo kwa kauli yako kuhusu Mawaziri kuacha majukumu ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhangaika nje ya nchi kusaka fedha za kuja kumng'oa 2025.
Kwa heshima na unyenyevu mkubwa na kwa kuwa wewe ndio kiongozi wa kwanza Tanzania kujitokeza hadharani kuuarifu umma juu ya mawaziri hao na kwa kuwa Mstaafu JK amekuita muongo nakuomba kwa muda na nyakati unazoona zinafaa jitokeze hadharani uwataje mawazi wote kwa majina yao matatu na wizara wanazoongoza ili watanzania wote wajue na tuwapime kama kweli wanayamudu majukumu ya Urais? na tuufunge rasmi mjadala huu.
Tukiuacha mjadala huu uendelee hivi hivi unaweza kuleta mgawanyiko mkubwa kati ya Chawa wa JK na Chawa wa Mama Samia na kusababisha Rais ashindwe kuongoza nchi kutokana na chokochokozo hizo.
Alamsikh!