Albert Chalamila jitokeze hadharani uwataje kwa majina Mawaziri wanaokwenda nje kukopa ili kumtoa Rais Samia 2025

Albert Chalamila jitokeze hadharani uwataje kwa majina Mawaziri wanaokwenda nje kukopa ili kumtoa Rais Samia 2025

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert John Chalamila umemsikia live Mstaafu Kikwete akikuita muongo kwa kauli yako kuhusu Mawaziri kuacha majukumu ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhangaika nje ya nchi kusaka fedha za kuja kumng'oa 2025.

Kwa heshima na unyenyevu mkubwa na kwa kuwa wewe ndio kiongozi wa kwanza Tanzania kujitokeza hadharani kuuarifu umma juu ya mawaziri hao na kwa kuwa Mstaafu JK amekuita muongo nakuomba kwa muda na nyakati unazoona zinafaa jitokeze hadharani uwataje mawazi wote kwa majina yao matatu na wizara wanazoongoza ili watanzania wote wajue na tuwapime kama kweli wanayamudu majukumu ya Urais? na tuufunge rasmi mjadala huu.

Tukiuacha mjadala huu uendelee hivi hivi unaweza kuleta mgawanyiko mkubwa kati ya Chawa wa JK na Chawa wa Mama Samia na kusababisha Rais ashindwe kuongoza nchi kutokana na chokochokozo hizo.

Alamsikh!

Huyo atatumbuliwa.
 
aliombewa msamaha kijanja kwa kueleza umma ulimi uliteleza

Yes aliombewa, ila yeye hakuomba msamaha. Akina ndugai waliongea vitu vya maana ila waliomba radhi, ila mzee karopoka kimya hakuna aliyemnyoshea kidole zaidi ya CHADEMA heche na Susan kiwanga.
 
Yes aliombewa, ila yeye hakuomba msamaha. Akina ndugai waliongea vitu vya maana ila waliomba radhi, ila mzee karopoka kimya hakuna aliyemnyoshea kidole zaidi ya CHADEMA heche na Susan kiwanga.
issue ya ndugai iligonga ikulu moja kwa moja wapambe wakupiga kelele na kujipendekez wakawa wengi ndio mana shinikizo la kuomba msamaha likawa juu tofauti kabisa na issue ya mswahili maamba
 
Back
Top Bottom