Albert Chalamila: Wazazi Temeke Hawawajibiki Vizuri Kulea Watoto wao

Albert Chalamila: Wazazi Temeke Hawawajibiki Vizuri Kulea Watoto wao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Screenshot_20241005-164859_1.jpg

“Jambo kubwa ambalo tumekuja kuligundua ni pamoja na wazazi wa wilaya ya temeke kutowajibika ipasavyo katika malezi ya watoto.

Mara nyingi tunafahamu kuzaa lakini hatufahamu kabisa maswala ya kulinda watoto wetu na hili kuna mfano mzuri sana shule za temeke ambazo watoto wa shule za msingi na sekondari wanakula shuleni hazizidi hata asilimia thelathini. Lakini ukihoji unaambiwa wazazi wengi hawana mwamko wa kuchangia chakula.

Hakuwezi kuwa taaluma nzuri hata siku moja kama mtoto asipopata chakula, na moja ya wilaya katika mkoa wa Dar es Salaam zinazofanya vibaya hata katika matokeo kidato cha nne ni Temeke” amesema Albert Chalamila mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
 
Mheshimiwa mkuu wa mkoa hivi kuna uhusiano gani kati ya watoto kula shuleni na kuongeza ufaulu wa kitaaluma?,yaani chakula kinaongezaje ufaulu???
Nyie mnapaswa kutafuta mbinu ya kuwafanya watoto wafaulu sio kuanza kutuletea hadithi za abunuwasi
 
Back
Top Bottom