Albert Mangwea (Special Thread)

Albert Mangwea (Special Thread)

hivi mnategemea watangaze kwenye vyombo vya habari kua alifariki kwa kutumia dawa za kulevya zenye sumu au pombe kali au kingine chochote chenye picha mbaya kwa jamii?

kwa maneno ya chini chini kwa nini watu wameropokea madawa na sio pizza yenye sumu? Inamaana hawakuona vitu vingine vya kusingizia?

mwisho kabisa bado najiuliza kwa upeo wangu mdogo wa kifikra bado sijaona picha ya dada yetu msibani aliesaidiwa na kaka mkuu kurudia hali ya kawaida baada ya kua muathirika wa yale mavituzi.
 
Jamani vijana kweli mnalewa na msichokijua mm wimbo hata mmoja wa Ngwea siujui
Kwanza hazina maudhui ambapo unaweza fananisha na mbaraka Mwishehe, Gurumo, TX-Moshi, Bichuka na wengineo
Huyu mtu ni mtumiaji wa madawa ya kulevya, na hii itasababisha kuambukizana uSuper Star wa kuyabwiya
Naungana na Mwana Mtoka Pabaya , Mapolomoko na wengineo kuwasifia watu waliokufa tuwe tunaangalia wapo wengi hawajaacha ujumbe wowote kwetu na watasahaulika wiki moja tu, tofauti na kina Franco, Mbaraka Juma Salim nk
 
Last edited by a moderator:
kwa maoni yangu mi nilitaka maiti yake ichapwe viboko ili liwefundisho kwa mateja ote na wanao taka kuingia ktk mkumbo huo, binafsi hakuna jema nililo jifunza kwake kamakweli alikufa kwa madawa.
ni kweli yeye amekufa kwa kula unga, hiyo ni dhambi, lakini wewe unayeihukumu hadi maiti una usafi gani? Yawezekana kabisa wewe ni mzinzi wa kutupwa, ama ni mwizi, ama mlevi wa pombe, ama ni mwongo au mmbea, zote hz ni dhambi kama ilivyo kula unga, ninachokuomba kwanza usihukumu usije ukahukumiwa pili jaribu kutumia lugha nzuri na tatu elewa hakuna mkamilifu.
 
Don't be pathetic. Maana yangu ni hivi: Mwana Mtoka Pabaya nikafa kesho sababu ya uzinzi wangu, basi na muache upumbavu wa kunisifia ooh alikuwa anachangia sana JF, mara kila msiba anahudhuria na kadhalika. Badala yake, waambieni waliobaki kuwa, upumbavu ndio umemuua Mwana Mtoka Pabaya ...........

Maiti ni nini wewe mbona hujitambui? Wewe ni roho yenye mwili na sio mwili mwenye roho. Tambua hatma yako iko mikononi mwako na sio kuongea maneno dhaifu yasiyojenga. Watoto wanazidi kuharibika kwa ajili jamii imejaa watu wenye akili kama zako.

Wengi wa mlioenda pale, mlienda pale kwa ujiko na fahari lkn sio tafakari ya tukio. Wote mnawaza kwamba Ngwea kazikwa na watu wengi, mnatamani pia, lkn hamuwazi kwamba amekufa kwa upumbavu ili mjiepushe. Ngwea hakufa kwa kukosa matibabu, Ngwea alikufa kwa FAHARI ZA DUNIA. Tufundishane na kukemeana na sio kuongea unafiki.
 
Last edited by a moderator:
hivi mnategemea watangaze kwenye vyombo vya habari kua alifariki kwa kutumia dawa za kulevya zenye sumu au pombe kali au kingine chochote chenye picha mbaya kwa jamii?
Ilipaswa. Public Figure na atumike kuelimisha. Au wewe unadhani ni jambo jema kumsifia Hitler baada ya kufa hata kama dunia nzima inajua alikuwa muuaji?

kwa maneno ya chini chini kwa nini watu wameropokea madawa na sio pizza yenye sumu? Inamaana hawakuona vitu vingine vya kusingizia?
Kwa kuwa wanayafahamu maisha yake. Leo hii tunavyoongea, kuna mwingine mnamsifia majukwaani kwamba anabadili wanawake, akifa kesho na yeye mumsifie kuwa alikuwa mtu mzuri sana. Wakati anaishi maisha ya chini huko Tandale alikuwa salama, sasa kapata fedha anahatarisha maisha yake na kuwa mfano mbaya, we call him 'The King'

mwisho kabisa bado najiuliza kwa upeo wangu mdogo wa kifikra bado sijaona picha ya dada yetu msibani aliesaidiwa na kaka mkuu kurudia hali ya kawaida baada ya kua muathirika wa yale mavituzi.
Atakuwa bize anaandaa presentation ya kuwaonya vijana kuwa madawa ni mabaya
 
Na ningemshangaa angekwenda kuzika wahuni akaacha kazi yake ya safari zisizo na mwisho wala maslahi. Tusikengeuke tukawa kama wazungu, kwa akili kama hizi ndio leo tuna Sir Elton John ambaye ni mke wa mtu. Naye akifa, mtataka heshima kwake

Keshaitwa 'SIR' chezea dunia weye?!:embarassed2::embarassed2::embarassed2::embarassed2:
 
no one is perfect ..hata wew una mabaya yako...na kuhusu taarifa za Ngwea kufa kwa madawa huyo ni uzushi...m2 the p hatumii madawa na mbona alipotea fahamu?wabongo achen ushamba wa kuzusha zusha...R.i.p Ngwea

Mbona unatokwa na mapovu tu lakini husemi ukweli kuhusu kifo cha Ngwair upi? Kama siyo drugs zilizomuua ni nini? Mnafikiri mkificha source ya kifo chake itawasaidia? Kama na wewe ni teja anza kuacha taratibu la sivyo, ooh ooh!!
 
Ngwea na mwenzie M2 the P walilishwa sumu....
 
Mazuri yake ni mistari yenye burudani na ukarimu. Once you do bad thing they say ever and twice you do a good thing they say never.Halafu wewe mtoa thraed una utakatifu gani wakuona wengine ndio waovu?kwa Mungu hakuna dhambi kubwa wala ndogo
Mungu akuangazie nuru na akusamehe makosa yako
 
Shida yetu Watanzania ni UNAFIKI na kupenda kuambiwa maneno matamu huku ukweli TUNAUKATAA.

Hawa watoto tabia zao tunazijua. Tuachane na marehemu, keshaenda, sasa hivi tunaye huyu Diamond anayetoboa masikio na kuvaa ------ yako nje. Hakuna anayemkemea, ni kumsifia na kumsujudia kila anapopanda jukwaani. Siku atakapokufa, ndio tunakumbuka kuwa Mungu ni mkubwa kuliko Diamond na hapo hapo tunasahau kwamba Mungu haamrishwi.

Haka kamsemo kenu kachafu ka R.I.P kwa watu ambao uchafu wao u dhahiri ni masihara. Ni vyema kumuombea rehema na sio kumwambia Mungu amuweke mahali pema peponi. Kuna mmoja wetu ana mchango wa tofali kwenye ujenzi wa hiyo pepo?

Na wewe Black Bat, unapoambiwa matatizo yako dawa ni kuyaacha na sio kutafuta mifano kwenye matatizo ya mtu mwingine. Kama Michael Jackson hakuwa mwema sio kigezo cha Mtanzania mwenzetu Diamond kuweka ------ nje na kujichubua.

Naunga hoja 100 per cent
 
Don't be pathetic. Maana yangu ni hivi: Mwana Mtoka Pabaya nikafa kesho sababu ya uzinzi wangu, basi na muache upumbavu wa kunisifia ooh alikuwa anachangia sana JF, mara kila msiba anahudhuria na kadhalika. Badala yake, waambieni waliobaki kuwa, upumbavu ndio umemuua Mwana Mtoka Pabaya ...........

Maiti ni nini wewe mbona hujitambui? Wewe ni roho yenye mwili na sio mwili mwenye roho. Tambua hatma yako iko mikononi mwako na sio kuongea maneno dhaifu yasiyojenga. Watoto wanazidi kuharibika kwa ajili jamii imejaa watu wenye akili kama zako.

Wengi wa mlioenda pale, mlienda pale kwa ujiko na fahari lkn sio tafakari ya tukio. Wote mnawaza kwamba Ngwea kazikwa na watu wengi, mnatamani pia, lkn hamuwazi kwamba amekufa kwa upumbavu ili mjiepushe. Ngwea hakufa kwa kukosa matibabu, Ngwea alikufa kwa FAHARI ZA DUNIA. Tufundishane na kukemeana na sio kuongea unafiki.
unadhani ukiandika maneno makali ya dharau na kebeh ndio utaeleweka, wewe huiwezi kazi ya ushauri japo una hoja za msingi..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hata wewe ukifanikiwa kupata wadhfa wa kuweza kutoa wasifu wa marehemu ambaye ni public figure kama usemavyo nina uhakika asilimia mia moja hutataja maovu wala sifa mbaya ya marehemu hata moja.

kuna kitu kinaitwa ustaarabu, pale unapotoa taarifa kwa njia ya wazi kwa umma kaa ukijua unapotosha kile kizazi ambacho hakijapevuka vizuri kiakili kwa kuweza kuchanganua mambo mbali mbali katika maisha.

kuna vijana watapata uelewa kutumia madawa ya kulevya (unga, bangi, n.k) ndio usanii timilifu hii ni kutokana na wao kusikia au kusoma wasifu wa marehemu kutoka kwa mtu kama wewe. Waswahili wanasema "kua uyaone" sio uzaliwe tu na kuyakuta tayari yapo wazi wazi.

Ilipaswa. Public Figure na atumike kuelimisha. Au wewe unadhani ni jambo jema kumsifia Hitler baada ya kufa hata kama dunia nzima inajua alikuwa muuaji?

Kwa kuwa wanayafahamu maisha yake. Leo hii tunavyoongea, kuna mwingine mnamsifia majukwaani kwamba anabadili wanawake, akifa kesho na yeye mumsifie kuwa alikuwa mtu mzuri sana. Wakati anaishi maisha ya chini huko Tandale alikuwa salama, sasa kapata fedha anahatarisha maisha yake na kuwa mfano mbaya, we call him 'The King'

Atakuwa bize anaandaa presentation ya kuwaonya vijana kuwa madawa ni mabaya
 
Watanzania sisi ni wanafiki alivyokuwa mzma watu kimya tu wanamwangalia kwan walikuwa hawajui kuwa anabugia lakn kifo chake sasa watu eeeh radio ndo usiseme hata nymbo zke ameuza baada ya kifo.tujifunze mzik bla dawa inawezekana

Chifu, kuna uzi katika jukwaa la celebrities ambao ulimkanya Mangwea na wasanii wote manyoka. Ebu pitia kule ili uuone ule uzi; una kichwa, "Unga unamharibu Mangwea".

Cheki hapa:

www.jamiiforums.com/celebrities-forum/195369-unga-unamuaribu-albert-mangwea-5.html#post6483108
 
wanao hoji kwanini nimesema maiti yake ichapwe viboko mnijibu kwanza hili, kwanini mtu anae jinyonga huchapwa viboko tena mbele ya familia yake?
 
Tatizo letu Binadamu kunyoosha vidole na kuingilia maisha ya watu wakati yetu yanatushinda...

Mazuri aliyokuwa nayo ni kuburudisha jamii / wapenzi wake na kutumia kipaji chake japo kwa muda mfupi kujipatia mkate wake wa kila siku...

Hayo mabaya yake na his personal life yalikuwa yake na familia yake wala sidhani kama yanakuhusu kiasi cha ku-condemn life yake yote., makosa aliyofanya kayalipia kwa kukatisha maisha yake..., mazuri aliyofanya ndio yamemfanya hata wewe leo unamuongelea (which can not be said for more than 90% ya watanzania)

Chukua mazuri yake aliyofanya na mabaya achana nayo
 
Back
Top Bottom