Album ya D'mond ipo mtaani, Wachoma CD 1500/= why? Basata nao

Album ya D'mond ipo mtaani, Wachoma CD 1500/= why? Basata nao

Nchi ya Tz ni sawa kabisa na kichwa cha mwenawazimu...... Kila mtu atakinyoa tu.
Waziri anakurupuka tu kufungia nyimbo wakati alitakiwa apambane kuweka mazingira sawa ya haki za wasanii ndipo azuie kazi zao ambazo kimaadili haziko sawa. Lakini nimegundua kuwa waziri mwenyewe ni wale wale tu waliowekwa bado wakiwa na akili za kitoto wanakurupuka tu asubuhi asubuhi na kujisikia kuja na matamko ya kufungia nyimbo kwakua tz ni kichwa cha mwenda wazimu kiongozi yeyote anaongea chochote anachojisikia
 
Duh hii bongo land ni shida , Yani nimekuta album ya diamond inabaniwa kwa shilingi 1500, kwenye vibanda vya kuchoma cd, kiukweli album ni kali, sasa nashangaa kwanini haki ya msanii inatumiwa na watu wengine kupata kipato. Au ndio maana ali kiba kaamua kutotoa nyimbo kabisa. Maana mtu unatoa album wanafaidika wengine
kwahiyo 1500 unaona kafaidikaaaa? dah wabongo bhana.
 
Jana nikuwa vijijini ndani ndani....niko ki pub flan nakunywa bingwa...mhudumu anajipigia album nzima ...nikamuuliza hiyo ni full CD album..akaniambia ni flash..

Nikakaa kimya.
 
Khaa bongo land tuache hii tabia millions alizotumia ku launch hii album afu mchome cd fake muuze jero roho mbaya
 
Jana nikuwa vijijini ndani ndani....niko ki pub flan nakunywa bingwa...mhudumu anajipigia album nzima ...nikamuuliza hiyo ni full CD album..akaniambia ni flash..

Nikakaa kimya.
Yaani hata me nashangaa wanaonunua albam wakati naweka kwenyeflash au nadownload kwa cm. Na kupiga nyimbo zoote. Ila wasaniii wanakazi kweli kweli
 
Ngoja nami nianzishe hiyo biashara ya cd ya diamond
 
Mi nawashangaa hata hao wanaotoa 1500 kununua CD, kabando kangu tu ka chuo ka jelo kanashusha albam nzima naweka kwenye simu, flash, nikitaka naweka na kwenye CD/DVD, hiyo ndio nguvu ya jelo. Sema natania tu, tununue CD og tumtegemeze msanii wetu aendelee kutingishiwa mattako na kina Wema Sepetu
Unaishusha kutoka wapi kiongozi?
 
Kama series na movie za mbele zinabaniwa na kina DJ Murphy tena hadi wanazisimulia kwa Kiswahili sembuse ya Diamond
 
Sie watanzania ni mabingwa wakuongeza viewers,youtube basi.
 
Duh hii bongo land ni shida , Yani nimekuta album ya diamond inabaniwa kwa shilingi 1500, kwenye vibanda vya kuchoma cd, kiukweli album ni kali, sasa nashangaa kwanini haki ya msanii inatumiwa na watu wengine kupata kipato. Au ndio maana ali kiba kaamua kutotoa nyimbo kabisa. Maana mtu unatoa album wanafaidika wengine
Kwenye haki miliki sio kazi ya Basata.. Wanao husika hapa ni KOSOTA sasa hapa pia huwa inategemea kama Mond alisajiri album yake Kosota...

lakini pia mkuu Tanzania bado hakuna usimamizi mzuri wa kazi za wasanii..Leo hii ndiyo mana wasanii wengi wanaishi maisha ya kuigiza ili hali wao ni maskibi
 
ni bora mana wanajitafutia ugali na wali wakuweka mezani kuliko kusikiliza wanasiasa wapuuz wasiosaidia lolote.
 
Halafu wasanii wetu wakifa Maskini tunawacheka. Mimi naomba serikali itilie mkazo kwenye hili swala la wizi wa kazi za wasanii,watu wafungwe na Mali zao za biashara zinazofanya hizo kazi za kuibia wasanii vipigwe mnada ili kupunguza ili tatizo maana najua kulimaliza kabisa HAIWEZEKANI.

Pia serikali iache kushughulikia Mambo yasiyo na kichwa Wala Miguu wajikite kwenye Mambo Kama haya ambayo yanaumiza wasanii mojamoja.

Ps: Serikali iweke utaratibu mzuri wa kusimamia kazi za wasanii
 
Back
Top Bottom