Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
Aldrich Ames alikuwa afisa wa ngazi ya juu wa CIA nchini Marekani ambaye aligeuka kuwa jasusi wa Urusi (KGB) wakati wa Vita Baridi.
Kuanzia mwaka 1985, Ames aliuza siri nzito za usalama wa Marekani kwa USSR ili kupata fedha za kufadhili maisha yake ya anasa. Alitoa majina ya majasusi wengi wa Kimarekani waliokuwa wakifanya kazi ndani ya Urusi, jambo lililosababisha takriban Majasusi kumi kuuawa na wengine kufungwa. Ames anachukuliwa kuwa mmoja wa wasaliti hatari zaidi katika historia ya Marekani
Ames alikiri kupokea takriban dola milioni 2.5 (zaidi ya Shilingi bilioni 7 za Kitanzania kwa thamani ya sasa) kutoka kwa KGB kuanzia mwaka 1985 hadi alipokamatwa mwaka 1994.
Inasemekana kulikuwa na kiasi kingine cha dola milioni 1.9 ambacho kilikuwa kimewekwa akiba kwa ajili yake nchini Urusi, hivyo kufanya jumla ya thamani ya usaliti wake kufikia takriban dola milioni 4.4.
Tofauti na majasusi wengi ambao huficha utajiri wao, Ames alitumia fedha hizo kwa namna iliyozua maswali mengi, ikizingatiwa mshahara wake wa CIA ulikuwa takriban dola 60,000 tu kwa mwaka. Mali alizokuwa nazo ni pamoja na:
Nyumba ya kifahari: Alinunua nyumba huko Arlington, Virginia kwa dola 540,000 akilipa kwa fedha taslimu (cash). Alimiliki gari aina ya Jaguar jekundu lenye thamani ya dola 50,000. Alifanya ukarabati wa nyumba yake kwa dola 99,000.
Maisha yake ya kifahari yalikuwa moja ya sababu kuu zilizowafanya FBI kutilia shaka na kuanza kumchunguza, kwani matumizi yake hayakuendana na kipato chake halali.
Vyote hivyo vilitaifishwa na Serikali ya Marekani.
Hadi kifo chake Januari 2026, Ames hakuwa na utajiri wowote; alikuwa mfungwa ambaye mali zake pekee zilikuwa ni zile zilizoruhusiwa gerezani.