Alert: Pokeeni Salamu Toka Kwa JF Member-Lunyungu.

Alert: Pokeeni Salamu Toka Kwa JF Member-Lunyungu.

Thanks PJ kwa taarifa hii muhimu na kwa moyo mkuu uliouonyesha,Mungu akuzidishe.Ninamuweka Lunyungu kwenye maombi yangu siku zote,Mungu aliye mponyaji hatampita wala kumpungukia.Ni imani yangu kuwa tutakuwa nae tena punde.
 
Mkuu PJ,
Shukrani kwa taarifa na upendo ulioonesha kama member wa JF na Mtanzania kwa mwenzetu. Tunamwombea Lunyungu apate matibabu mapema, apone na kurudia afya njema. Mwenyezi Mungu Amsaidie. Amen.

Steve Dii
 
Thanx PJ
Get well soon Lunyungu..................... Mungu ni mwema, utapona tu
 
Shukrani kwako PJ. Mungu ni mwingi wa fadhili na rehema tunayo imani kubwa uponyaji upo. Mungu akutangulie kwa kila jambo na tunatangaza uponyaji kwani shetani hana mamlaka katika mwili wa mwanadamu.
 
PakaJimmy thanx kwa kutuwakilisha na kutupa taarifa.
Nilimpigia simu na kuongea naye kirefu sana. Naamini anafarijika tunapomjali hata kwa salaam.

Nina maombi kwa MODS na INVISIBLE.
Kama inawezekana tudundulize sh mia mia zetu kwa wazee wa jukwaa kisha zimfikie kwa ajili ya kununulia dawa na matibabu. Just kumsaidia maana leo kwake kesho kwangu.
Kwa kuanza nitatuma jioni la leo shs 10,000/- na text ya kuelekeza mchango ni wa nini. Nitatuma endapo ombi la kumchangia Lunyungu litakubaliwa. Sijali itikadi, imani, ukabila wala rangi. natukuza UTANZANIA na UDUGU.

Nasubiri jibu ktuoka kwa mods au Invisible
Naona Mods wako kimya...
Hey mods, could you pls expedite the launch of this vital initiative by Msanii!
 
Thanks PJ kwa taarifa, Tunamuombea ndigu yetu Lunyungu kwa Mungu, apone haraka.
 
Poel sana mkuu Mungu yuko pamoja na wewe utapona. Get well soon Dear
 
Thx Pj kwa info nimetoka kuongea na na Lunyungu kwa sim kwakweli anaumwa sana pia nimeongea na Pj maana walikuwa wote mda huu KIA anajiandaa kupanda ndege kuja Dar ili usiku aende nje kwa matibabu zaidi,Pj big up sana kwa msaada ulioonyesha maana nilikuwa nakskia unatafuta wheel chair na kuhangaika kumbeba ili apande kwenye ndege,Mungu atakulipa .Lunyungu Mungu ni mwema na hata kuacha daima maana imeandkwa ombeni lolote kwa jina langu nasi tunaomba uzima kwajili yako maana If God is with us who will be agaist us?GET WELL.
 
Naona Mods wako kimya...
Hey mods, could you pls expedite the launch of this vital initiative by Msanii!
Naona MODS hawataki mwenzetu asaidiwe ndo maana wanipita kimya kimya hii thread.
Nashindwa kutuma funds kwa kuwa sijapewa maelekezo na ruhusa kutoka kwa wasimamizi wetu.
Mungu amjalie apone na arudi hapa maana tunamtegemea auje hilo.
 
MUNGU MWENYE REHEMA NA UTUKUFU ATAMPONYA NDUGU YETU HUYU MPENDWA................

PJ sina cha kusema juu yako, wewe ni mtu wa ajabu sana, una moyo wa upendo sana, sijapata kuona maishani mwangu.. hongera sana
 
Thx Pj kwa info nimetoka kuongea na na Lunyungu kwa sim kwakweli anaumwa sana pia nimeongea na Pj maana walikuwa wote mda huu KIA anajiandaa kupanda ndege kuja Dar ili usiku aende nje kwa matibabu zaidi,Pj big up sana kwa msaada ulioonyesha maana nilikuwa nakskia unatafuta wheel chair na kuhangaika kumbeba ili apande kwenye ndege,Mungu atakulipa .Lunyungu Mungu ni mwema na hata kuacha daima maana imeandkwa ombeni lolote kwa jina langu nasi tunaomba uzima kwajili yako maana If God is with us who will be agaist us?GET WELL.

Ndege iliyomchukua Lunyungu (PW437, ATR-42, reg No 5HPWF, )imeondoka sasa hivi saa 10.00 jioni ikiondokea Arusha Airport!..Ni ya shirika la Precision....NA INATARAJIA kufika dar (via ZNZ) saa 1.00!
Akiwa Dar atafanyiwa final check-up na daktari kabla ya kuingia kwenye pipa muda wa saa6 usiku kuelekea ughaibuni!
Mungu amtangulie Bingwa huyu!
 
PJ - Watu tubishana hata hapa jukwaani kuhusu uzuri au ubaya wa dini hii au ile:

Lakini wewe umetuonyesha dini ya kweli - upendo kwa jirani.

Tunamtakia mema yote Lunyungu.
 
Nitampigia Lunyungu afikapo dar nimtakie safari njema.
Thanx PJ kwa updates
Ila USILEWE SIFA
 
Wapendwa wanajf napenda kumshukuru ndg yetu pj kwa taarifa za kuumwa na ndg yetu Lunyungu.baada kupata habari za kuumwa kwa nilitafuta mawasiliano na nikampata huyo ndg.alinipa maelekezo nikafanikiwa kufika ilikuwa kama saa moja na nusu usiku.Hapo ndipo tulionana kwa mara ya kwanza,tulifurahi sana pamoja na kwamba alikuwa na maumivu makali.niliona ana ujasiri mwingi na imani kwa mungu,kwamba atapona.Kwangu mimi ninaona ni vita vya kiroho na mwili pia,hivyo tumwombee sana ndg yetu.Mwisho napenda kuwashukuru waanzilishi na wanachama wa forum hii, kwani tangu nimeifahamu nimejifunza mengi Mungu awabariki sana.
 
Ndugu wanaJF,

...na kweli alinielekeza kwake maeneo ya Njiro, nikafika, na kwa mara ya kwanza tangu dahari tukafahamiana!.
Kwakweli huyu ndugu jamani anaumwa!...amekuwa totally incapacitated, na ni wa kupewa msaada kwa kila movement anayohitaji...sina maneno zaidi ya kusema ANASIKITISHA!

Asante Mkuu naamini kuwa ziara yako ilikuwa ni ya kutuwakilisha sisi wote hapa ambao hatuwezi kumuona kimwili mwenzetu huyu. lakini naamini tutaendelea kumuombea Mungu amrejeshe kwenye afya yake haraka iwezekanavyo kwa sababu mchango wake bado nimuhimu, si hapa tu, bali kwa taifa.
Mungu akujalie uzima mkuu Lunyungu
 
Back
Top Bottom