Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amepandishwa cheo na kuwa Kamishna wa Polisi, pamoja na kuteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan, kuwa Kamishna wa Polisi Jamii.
Kamishna Mkama ameapishwa rasmi leo, tarehe 26 Machi 2026, na Mkuu wa Jeshi la Polisi,
Camillus Wambura.
Kupandishwa cheo na uteuzi huu ni matokeo ya utendaji wake uliotukuka, nidhamu, na mchango wake mkubwa katika kuimarisha usalama na utulivu wa wananchi.
Tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya ya kulitumikia taifa.
Hongera sana Kamishna Alex Mkama 👏🏾🇹🇿