Alexander Mnyeti Maji ya Shingo, miradi yake yaanza kufa mmoja baada ya mwingine

Alexander Mnyeti Maji ya Shingo, miradi yake yaanza kufa mmoja baada ya mwingine

Bora hata angewekeza kwenye real estates. Ila siyo kwenye rimu ya mpira wa miguu. Anyway, siyo mbaya. Ameambulia hata ubunge.

Na kama ana akili timamu, 2025 asipoteze hela zake za kiinua mgongo kwa ajili ya kutetea huo ubunge wake.
Kumbe ni wapinzani wake kisiasa , 2025 tutaona mengi
 
Huyu ni miongoni mwa wale waliokuwa wanafaidi matunda ya nchi kwenye utawala wa Awamu ya 5, ni mmoja wa wale viongozi wa ngazi ya chini waliokuwa na Kiburi kilichopitiliza , inadaiwa alikuwa na uhusiano wa Kindugu na John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania .

Mnyeti aliokotwa kutoka kwenye ualimu na kupewa Ukuu wa Wilaya , ghafla akaanza kuwa Tajiri wa kutupwa na dharau na kejeli vikamwingia ( ulevi wa madaraka ) , akapandishwa cheo na kuwa RC , akaanza kumiliki miradi kadhaa ikiwemo timu ya soka inayoitwa Gwambina , akapewa na TCC CLUB na kuiita Gwambina , ili ajenge hostel kwa ajili ya timu yake , akajenga na uwanja wa soka , yaani RC anajenga uwanja wa soka ambao Taasisi nyingi za nchi hii hazina , alikopata hela anajua mwenyewe , japo inadaiwa alikuwa na kolabo na mkubwa kwenye mashimo ya madini (tetesi) , kukawa na mpango wa kupewa Uwaziri , ikabidi kwanza aanzie kwenye ubunge wa Misungwi , wapinzani wakahujumiwa , akapita bila kupingwa .

Waswahili wanasema ukiona ngedere mjini basi ufahamu kwamba kafugwa , mfugaji akifa huyo ngedere atarudi mwituni au atakufa njaa , Sasa kwa kufupisha ni kwamba , Timu ya soka ya Gwambina inayomiliki uwanja wake , ambayo ni Mali ya Mnyeti ,
sasa IMEJIONDOA KWENYE CHAMPIONSHIP kwa kile kinachodaiwa ni kuelemewa na gharama za uendeshaji , Yaani baada ya Magufuli kufa Mnyeti anashindwa kuendesha Timu ! Hivi mnanielewa lakini jamani ?

Neno la leo linatoka kwenye kitabu cha YEREMIA 17 : 5-8

View attachment 2457682

Itaendelea ........
Ningeshangaa kama usinge mtaja Magufuli.
 
Hasa ikiwa utajiri wenyewe umepatikana kwa wizi na dhuluma kwa hao masikini kwa sababu hakuna anayechukia utajiri wa baghresa au wa dewji.
Una hakika hao uliowataja utajiri wao ni wa halali.How about if it is masonic and therefore backed by human sacrifices,and I believe it is.
 
Back
Top Bottom