Matokeo Waliyo yapata Simba Mimi niliyategemea Kwaiyo sikushtuka, na nilisha andika zaidi ya mara mmoja.
Wydad hivi ndivyo hufanya ugenini, wata tafuta ushindi,sare au wakishindwa watafungwa ila tofauti haizidi goli mmoja.
Wameshafanya hivyo mara nyingi ila kule kwao goli zao zina anzia tatu ni Ahly pekee aliye pigwa 2
MO afanye kama alivyo fanya Mjomba wake Azim Dewji mwaka 1993 Tena hii itakua ugenini Haina shida, Kwakua Hakuna namna nyingine zaidi ya kubalance vitabu vya fedha.
Mashabiki wengi hawaelewi, Hii sio hatua ya kushinda tu, Hii ni hatua ya kufuzu.
Watu wa mpira wanaelewa nini namaanisha, Ingekua kwenye hatua ya makundi kushinda Kuna maana kubwa ila hatua hii kinacho tengenezwa ni tofauti ya Magoli.
Wengi wataelewa baada ya marudiano ya hizi mechi na watajifunza kuanzia hapo.