Tukiachana na wakongwe wetu waliosimama na mziki wetu wa dansi hadi mwisho wa uhai wao kama Marijani Rajabu na Mbaraka Mwinshehe. Banza Stone ni msanii mungine ambae anapaswa kuenziwa na kuheshimiwa katika mziki wa dansi.Huwa nafurahi sana kuona Banza anapewa heshima yake stahiki, nimekuwa nikisema mara nyingi huyu ndiye msanii bora wa dansi wa muda wote hapa nchini.
Aendelee kupumzika kwa amani.
Hakika.Banza alikuwa mbele ya muda!! Kipaji maridhawa
Mimi elimu ya mjinga ni majungu, mtaji wa masikini nazikubali sana.kama kuna wimbo banza stone alijua kucheza na sauti yake basi ni kwenye 'supu ya kuku wa kienyeji', ameondoka na kipaji chake kwa kweli.
Mkuu umekumbuka mbali, kwenye drums kulikuwa na mwamba Rastaman GABBY KATTANGA ilikuwa ni hatari. Mungu awape pumziko wanapostahili hawa miamba.Vipi ndugu zangu.
Vitu vitamu kama hivi hapo chini ni vigumu sana kuvipata kwa msanii mungine yoyote zaidi ya marehem Banza Stone:
1. Kisa cha mpemba.
2. Mwenye kwenu kwaheri.
3. Mtu pesa.
4. Aungurumapo Simba.
5. Mtaji wa masikini.
6. Elimu ya mjinga ni majungu.
Ama kweli udongo unakula watu, sio miti.
RIP Banza Stone mutoto ya mujini, acha tubaelezeye.
Ndio. Hapo tu ndio Banza alizingua.Wewe ni Yanga kama mimi eeh ? πππ