Ali Choki na Muumin Mwinjuma walikuwa wasanii wazuri mno miaka ya 2000 lakini itoshe kusema kuwa Banza Stone alikuwa mwalimu wao

Ni historia nzuri sana hii.
 
Muhasibu hapana nakataa, nyakati nyakati zimepita mkuu Muumini hajabadilika kitu ,

Tungo zake ni zile zile sauti yake ile ile ila nyakati hizi zinawataka kina
Oyoo oyooo yaah yaaah piga keleleeeee

Baasi nadhani umenielewa
Hizi ni nyakati za kulalamika lalamika tu hakuna cha mana kinachoimbwa.
 
Kabisa, unaujua ule wimbo wa Safari? Aliukuta usharekodiwa wakati anarudi Twanga, akausikiliza na akaanza kuuweka sawa.

Ikatoka bonge ya hit, hadi ikapewa jina la albamu. Kwenye Safari sauti ya Banza iko kwa uchache sana, ila kainyoosha.

Ova
Huo wimbo ni kama aliuweka sawa kwa ajili ya kaka mmoja mzuri aliyeko safarini…

Mimi ile sehemu aliyoimba ndio my favorite part, 🎶….. jua mimi nakupendaaa🎶

Apumzike kwa amani Jenerali, hatokaa atokee kama yeye tena.
 
Hicho kitu sio mchezo, hasa ukikisikiliza wakati ukiwa na hela mfukoni.
Lilikuwa ni goma la njiani ikiwa mko kadhaa mnahama kiwanja usiku sana baada ya Kiwanja A kuanza kupoa. Hapo hakuna wa kusema twendeni tukalale, mizuka inapelekwa juu sana.

Ova
 
Mimi elimu ya mjinga ni majungu, mtaji wa masikini nazikubali sana.

Actually kila alichoimba Banza nakipenda isipokuwa angurumapo simba.
"Aungurumapo Simba" ndio wimbo bora namba moja wa Banza Stone! Ahahahahaha!!
 
Hakun kapicha ukatupiye, hawo wazee hatuwajuwi.
 
Huwa nafurahi sana kuona Banza anapewa heshima yake stahiki, nimekuwa nikisema mara nyingi yeye ndiye msanii bora wa dansi wa muda wote hapa nchini.
Aendelee kupumzika kwa amani.
wapo sambamba na TX MOSHI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…