Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Ninavyowaona hawa wazee hawapendi kabisa watu kuonewa .hawapendi dhuluma .ila hamna siasa isiyokuwa na dhuluma.Ndio maana Mzee mwinyi alijiuzuru uwaziri wa mambo ya ndani baada ya kuona dhuluma na mauaji yalifanywa na polisi wasio na maadili. Na aliweka wazi kabisa ni polisi ambao walikiuka majukumu yao ya kulinda mali na usalama wa raia.Pia Mzee kagasheki alijiuzuru kwa sababu ya askari waliofanya operation iliyoleta dhuluma na mauaji kwa watu wasio na hatia. Wote hawa wawili waliwajibika kwa makosa ya askari wasio na maadili. Ila mara kwa mara kauli za wazee hawa huwa zinaonyesha wazi hawapendi watu kuonewa na kudhulumiwa haki zao. Mfano mzee Kagasheki siku ya krismas aliweka wazi kabisa masikitiko yake juu ya watu wanaobambikiwa kesi. Jambo ambalo sasa limekuwa kama janga la taifa. Mtu anakamatwa na kosa la wizi wa simu atapewa kesi ya unyag'anyi wa kutumia siraha. Ili mradi tu ahangaike na kama ikibidi atoe rushwa sababu ni kesi ambayo haina dhamana. Ni wanasiasa wachache sana kama Mwinyi na Kagasheki ambao hawapendi kuona watu wanaonewa. Wengi wakipata madaraka ni kuonea watu tu." Polisi ni chombo cha kulinda raia na mali zao si chombo cha kuwaua" Wanasiasa wachache sana wasiopenda dhuluma!