Ali Kamwe aombe radhi yaishe asilete ujuaji wake

Ali Kamwe aombe radhi yaishe asilete ujuaji wake

Kusema katoa jezi MBAYA kuna sababishaje jezi nzuri zilizo tolewa na SANDA ziwe mbaya?

Kama ni nzuri halafu atokee mtu aseme ni mbaya na mazuzu wa simba waache kununua jezi nzuri kwa sababu tu mtu wa yanga amesema ni jezi mbaya.. Tatizo litakuwa kwa nani?
Hujaelewa alichoandika mtoa post. Yeye hajalaumu maoni ya Ally Kamwe, bali kalaumu kwa kumtaja mzalishaji wa jezi kwa jina lake moja kwa moja. Elewa utofauti huo na pia natanguliza pole kwa yatakayotokea kwa Che Majaliwa Stadium !!!
 
Hii ikipita maana tunafungua uwanja mpya wa kufunguliana kesi kwa kila kauli itakayosemwa na wasemaji wa timu hizi mbili.

Wazee wa Simba walihitishi mkutano na waandishi wa wa habari na moja ya shutuma zao walizielekeza kwa GSM kuhusu kudhamini timu nyingi wakihusisha na kupanga matokeo. Hatukuona mashtaka yoyote, sio kwamba hawakuweza ni katika kudumisha utani wa jadi.

Ila hii vita wanayoanzisha Sandaland itawagharimu wengi.
 
Bonge la hoja
Kusema katoa jezi MBAYA kuna sababishaje jezi nzuri zilizo tolewa na SANDA ziwe mbaya?

Kama ni nzuri halafu atokee mtu aseme ni mbaya na mazuzu wa simba waache kununua jezi nzuri kwa sababu tu mtu wa yanga amesema ni jezi mbaya.. Tatizo litakuwa kwa nani?
 
Simba na Yanga ni watani wa jadi, kama hutaki kutaniwa usijihusishe na clubs hizo. Personal issue mnaleta kwny utani wa jadi!! Mbona jezi za Taifa tars nzuri na Sanda ndio aliyetengeneza na watu wote tunavaa na kuzisifia.
Michezi ya Makolo ni ya hovyooo!!
 
Kwahio na mtu akisifia kwamba ni nzuri aende kuomba posho kwa kuwatangazia biashara ?

Hicho ni kitu subjective na hakuna nchi itamfunga mteja kwa kusema kwamba kitu fulani ni kibaya..., unaweza ukafunguliwa kesi kama ume mislead watu mfano kusema uzi unaotengenezea jezi umeoza au pamba imetoka kwenye mali za wizi, au jezi zina Corona au Ukimwi..., lakini kuongelea uzuri au ubaya hilo sio Kosa..., Sasa mtu akiona ni mbaya asiseme..., Na Je watu watakubali kwamba ni mbaya sababu yeye amesema ? Na akisema nzuri itageuka kuwa nzuri ?!!!
 
Kama ni utani angesema tu..makolo wametoa jezi mbaya baasi..lakini kasema bwana SANDA katoa jezi mbaya ndio maana viongozi wa Simba wamegoma kuzizindua ...huu ni ugonvi wake na SANDA.. Kamwe kakosea
Makolo ndio wamatoa jezi mbaya au sanda?
 
Defamation Haina uzito kwa tz tu kwakua watu wanachukulia poa, lakini kwa nchi za wengine ni bonge la case.

sio kosa kuponda jezi za Simba, kosa ni kutaja jina la mtengenezaji na msambazaji. kataja neno sanda ni kuharibu brand ya watu.

Sanda ni brand ndomana jina la sanda linasoma kwenye jezi za Simba. Kwahy kumtaja sanda Moja kwa moja ni kosa.

Ahmed Ally utamskia akiponda jezi za Yanga lakini huwezi kumskia akisema GSM katoa jezi mbaya, GSM ndo msambazaji wa jezi za yanga, GSM ni brand na yeye kama msemaji wa club kubwa anamamilioni ya watu wanaomfatilia , neno lake linasafiri masafa marefu.

Kumshambulia hadharani ni kuharibu biashara yake.

Hata kama watayamaliza kimya kimya lakini atapata funzo kuto kumshambulia mtu au brand yake Moja kwa moja. Nafikiri hata sanda Hana shida na hizo pesa Bali ni kumpa funzo kijana.
Kwani jezi si zimeandikwa SANDA..!!?? Akikuambia yeye alisoma kilichoandikwa na wewe utaomba radhi..!!??
 
Defamation Haina uzito kwa tz tu kwakua watu wanachukulia poa, lakini kwa nchi za wengine ni bonge la case.

sio kosa kuponda jezi za Simba, kosa ni kutaja jina la mtengenezaji na msambazaji. kataja neno sanda ni kuharibu brand ya watu.

Sanda ni brand ndomana jina la sanda linasoma kwenye jezi za Simba. Kwahy kumtaja sanda Moja kwa moja ni kosa.

Ahmed Ally utamskia akiponda jezi za Yanga lakini huwezi kumskia akisema GSM katoa jezi mbaya, GSM ndo msambazaji wa jezi za yanga, GSM ni brand na yeye kama msemaji wa club kubwa anamamilioni ya watu wanaomfatilia , neno lake linasafiri masafa marefu.

Kumshambulia hadharani ni kuharibu biashara yake.

Hata kama watayamaliza kimya kimya lakini atapata funzo kuto kumshambulia mtu au brand yake Moja kwa moja. Nafikiri hata sanda Hana shida na hizo pesa Bali ni kumpa funzo kijana.
 
Naye huyo sanda aache ufala... Watu kibao si walikuwa wanasema kaamua kutengeneza sanda (nguo ya maiti), mbona hakumaindi?

Ukiona imemuuma basi jua imemchoma na kumuingia kisawasawa. Kwa yale madekio halali yake amaindi
Kwani nyie Uto mnafika wapi na hizo jezi zenu mpya? Mwisho wenu ni makundi full stop.
 
Ni mtazamo wako
Sasa kama anaona jezi mbaya unalazimisha aseme ni nzuri.

Kwa mfano nikisema soda ya Pepsi ni mbaya ni kosa?
Sio kosa , kosa ni kusema SBS katengeneza soda mbaya tena hadharani mbele ya vyombo vya habari.
Kwani huyo kamwe angesema sanda katoa jezi mbaya akiwa chumbani kwake peke yake nani angembana!?, Hivi hata mchome anazipindaga jezi za Simba, ulishawahi kumskia akisema sanda katoa jezi mbaya!?.

Huyo alikamwe angeponda jezi sio msambazaji.
 
Uhuru wa maoni ni haki ya misingi kikatiba
Mtu anatoa mAoni popote
Sio hadi chumbani
Msambazaji akubali kwamba analeta bidhaa sokoni na ategemee mtazamo tofauti juu ya bidhaa anayodhalisha
 
Makolo ndio wamatoa jezi mbaya au sanda?
Duuh!! Unajua maana ya "direct attack"!?. Alichofanya kamwe ndo hcho kamshambulia sanda Moja kwa moja.

Mfano. Wewe una genge la nyanya na vitunguu akaja mteja akaona nyanya mbaya , akaanza kusema " Muuzaji wa nyanya m'baya sanaa ndomna nyanya zake zimedoda haziuzikani.

Hapo huyo mtu kakudhihaki wewe na Sio nyanya zako, kwakule kusema wewe m'baya ndomna nyanya haziuzikani.

Lakini mtu huyo huyo akisema " nyanya mbaya havieleweki" hapo kaidhihaki bidhaa na Sio wewe.

Kwahy bwana Ally kwa kusema kwake "Sanda katoa jezi mbaya ndomna Simba wamemsusia uzinduzi, hapo kamdhihaki sanda Moja kwa moja na Sio jezi, na sanda na Simba wanaubia wa biashara Hana uhusiano na utani wa jadi wa Simba na yanga. Ndomna aloshitaki ni Sanda na Sio Simba.

Simba hawahusiki na hiyo case kwakua wao hawatengenezi jezi wamempa mdhabuni, Chao wakishachukua zamani. Kwahy sanda akiuza jezi asiuze ni juu yake wao haiwahusu.
 
Maoni unayatoa kwa njia ipi!, Kosoa bidhaa sio mtu
 
FB_IMG_17324418554201699.jpg
 
Si yanga watampa s ndo walimtuma
Yanga watamlipa bwana SANDA akituthibitishia hiyo hasara. Atueleze kabla ya defarmation alikua anapata faida kiasi gani na sasa imepungua kiasi gani.
Tutahitaji mauzo yanayothibitishwa na EFD machine, kama hana hizo risiti tutajua hiyu ni mhujumu uchumi anauza bila kutoka risiti za EFD kuhumu uchumi wa nchi.

Tutahitaji na bank statements za kipindi hicho zisipotimia tutajua anahifadhi fedha kwenye viroba kuharibu mzunguuko wa fedha ili kuharibu uchumi wa nchi .Economic sabortage.
Tutawaalika TRA watuambie trend ya Kodi kwa miaka ya nyuma tangu aanze hii biashara inayolipa kiasi hiki ili kama kuna mapunjo ya kodi Serikali ilipata ifidie
 
Natamani kusingewekwa option ya kuomba radhi. Hawa watu wamezidi kuleta utani wa kijinga. Kuna haja ya kuwatia adabu
 
Back
Top Bottom