Ali Kamwe: Kocha wa APR anatakiwa kuomba msamaha hadharani

Ali Kamwe: Kocha wa APR anatakiwa kuomba msamaha hadharani

Kocha wa APR aombe radhi

"Mapinduzi Cup ni Tournament Maalum yenye heshima kubwa hapa Afrika Mashariki na Kati.. Timu nyingi kubwa, Wachezaji wengi wakubwa wameshiriki.

Tunapaswa kuyalinda, kuyaheshimu kwa nguvu zetu zote.. Hata mtu anapotaka kuyaongelea ni Lazima ayaongelee kwa Nidhamu.. Isionekana mtu anakuja kushiriki kama 'msaada' tu kwa wenye mashindano.. Hii sio sawa Kabisa.

Mistake za waamuzi kwenye Football zinatokea mpaka World Cup.. Hata ujio wa VAR bado kuna makosa mengi ya waamuzi yametokea.

Inakuaje mtu mwenye Taaluma ya Ukocha anayakosea Heshima mashindano ya Mapinduzi kirahisi tu kwa sababu ya Waamuzi?

Video hapo juu (Ipo kwenye ukurasa wa Ally Kamwe Instagram) Timu yake ya APR ilipewa BAO LA MCHONGO dhidi ya JKU kutoka ZANZIBAR mbona hakusema Hatushiriki Tena kwa sababu Waamuzi wanatupendelea?

Wakikosea Waamuzi kwa wengine Meno yote Nje na kujiona bonge la Kocha.. Wanashangilia mpaka wanavua Nguo uwanjani.. Wakikosea wengine Mnasusa??

Sasa Kwa Tukio la Jana na Hilo hapo la mechi ya JKU Lipi lina upendeleo wa wazi kabisa??? Nafikiri Kocha wa APR anatakiwa KUOMBA MSAHAMA HADHARANI kwa kauli yake.

Mwenyekiti wa Wasemaji Afrika Ally Kamwe." Ameandika Kamwe.​
Huyu huenda amejiunga na machawa anatafuta uteuzi. Stupid!
 
Hoja yake ni ya msingi sana hata mimi nimemuelewa.

Ila asivuke mstari kwa kuwataka APR waombe radhi kwenye madai ambayo yamegusa ukweli.

Kwamba ni uongo kuwa swala la waamuzi haliwezi kuitia aibu soka la Tanzania?

Mwezi October Ally Kamwe alipewa adhabu na TFF kwa kumdhihaki mwamuzi Tatu Malogo.

Na hata humu minions wake walikuwa wanakejeli watu wengine kwa kutumia jina la Tatu Malogo.

Lini Ally Kamwe alijitokeza hadharani kumuomba radhi Tatu Malogo?
Haya ni maoni ya Kolo kabla halijabebwa Kwa mbeleko.
 
Haya ni maoni ya Kolo kabla halijabebwa Kwa mbeleko.
Yapo matukio ambayo ni ya kweli na mimi nayakubali bila kutanguliza ushabiki

Ila kwa mechi ya leo sijaona hoja yeyote yenye mashiko zaidi ya malalamiko ya kihisia tu
 
Back
Top Bottom