pesakilakitu
JF-Expert Member
- Aug 17, 2024
- 1,618
- 2,861
Ama kweli siku ya kufa nyani...hawa makomandoo inaelekea wana nguvu sana kushinda hata uongozi wa Yanga..
Ali kamwe tunajua sote ni msemaji wa timu ya Yanga na ni jambo la kawaida kabisa kila kabla na baada ya mechi lazima ajitokeze ili aweze kuzungumzia mchezo ulikuaje.
Sasa katika hali ya kustaajabisha na kushangaza wakati Ali Kamwe anaongea na waandishi wa habari kama ilivyo ada, ghafla walijitokeza wanaojiita "makomandoo" wa Yanga na kukatisha ghafla press hio utadhani nchi inataka kutekwa na kumchukua Ali Kamwe mzobe mzobe na kumuondoa haraka na kutokomea nae kusikojulikana.
Kama wanamichezo na wapenda fair play tunapinga vitendo hivi vya kihuni na vyenye dalili ya uvunjifu wa amani katika soka.
Soka ni burudani, na soka ni furaha, na pia tunapinga kuvunjwa kwa taratibu na sheria za soka zinazosimamiwa chini ya jemedari mwamba Karia.
Tunaomba mamlaka za kiusalama, bodi ya ligi pamoja na uongozi wa klabu kuchukua hatua kali dhidi ya wahuno hao wanaojiita na wanaochafua neno "komandoo".