Ali Kamwe naye atolewa mzobe mzobe na "makomandoo" asiongee na wanahabari

pesakilakitu

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2024
Posts
1,618
Reaction score
2,861
Ama kweli siku ya kufa nyani...hawa makomandoo inaelekea wana nguvu sana kushinda hata uongozi wa Yanga..

Ali kamwe tunajua sote ni msemaji wa timu ya Yanga na ni jambo la kawaida kabisa kila kabla na baada ya mechi lazima ajitokeze ili aweze kuzungumzia mchezo ulikuaje.

Sasa katika hali ya kustaajabisha na kushangaza wakati Ali Kamwe anaongea na waandishi wa habari kama ilivyo ada, ghafla walijitokeza wanaojiita "makomandoo" wa Yanga na kukatisha ghafla press hio utadhani nchi inataka kutekwa na kumchukua Ali Kamwe mzobe mzobe na kumuondoa haraka na kutokomea nae kusikojulikana.

Kama wanamichezo na wapenda fair play tunapinga vitendo hivi vya kihuni na vyenye dalili ya uvunjifu wa amani katika soka.

Soka ni burudani, na soka ni furaha, na pia tunapinga kuvunjwa kwa taratibu na sheria za soka zinazosimamiwa chini ya jemedari mwamba Karia.

Tunaomba mamlaka za kiusalama, bodi ya ligi pamoja na uongozi wa klabu kuchukua hatua kali dhidi ya wahuno hao wanaojiita na wanaochafua neno "komandoo".
 
Bodi ya Ligi haiingii hapo. CAF ina maslahi na official press kwa kuwa ina wadhamini wa michuano hiyo. Sina uhakika kama hiyo press ya Ali Kamwe ilikuwa inaangukia katika official press au la
 
Ama kweli siku ya kufa nyani...hawa makomandoo inaelekea wana nguvu sana kushinda hata uongozi wa Yanga..

Ali kamwe tunajua sote ni msemaji wa timu ya Yanga na ni jambo la kawaida kabisa kila kabla na baada ya mechi lazima ajitokeze ili aweze kuzungumzia mchezo ulikuaje...
Nyuma mwiko ni timu ya wahuni tu.

Wakishinda utawaona akina mama j wanafanya yao,wakifungwa utawaona mazmbie wanavyofanya ubabe.
Kwa kuwa wengi hutumika kwenye siasa,hutaona hatua zozote zikichukuliwa.
 
Ama kweli siku ya kufa nyani...hawa makomandoo inaelekea wana nguvu sana kushinda hata uongozi wa Yanga..

Ali kamwe tunajua sote ni msemaji wa timu ya Yanga na ni jambo la kawaida kabisa kila kabla na baada ya mechi lazima ajitokeze ili aweze kuzungumzia mchezo ulikuaje...
Sheria gani imevunjwa hapo.

Kocha ndio msemaji baada na kabla yq mechi.

Kama ni uminzi hata Messi ana commando wake
 
Sio lazima kuongea ila mbona 99% Mechi zote kaongea leo wameona nini au hasira za kukandwa yaan dose ni ile ile lazima atuambie kwanin alisema kwamba wananchi wasiende popote baada ya kupiga kura eti hakuna kuzurura 🤣🤣🤣Huyu hana uenyeketi wowote wa usemaji kutwa kuwajaza upepo mashabiki kwakuwapandikiza chuki dhidi ya wapinzani wao wa jadi hovyo kabisaa
 
Kusema ukweli Ali kamwe anekuwa kama mjinga siku hizi aneanza juropoka ropoka na kujenga uhasama ,bora wangekapiga tu
 
Sio lazima kuongea ila mbona 99% Mechi zote kaongea leo wameona nini au hasira za kukandwa yaan dose ni ile ile lazima atuambie kwanin alisema kwamba wananchi wasiende popote baada ya kupiga kura eti hakuna kuzurura 🤣🤣🤣Huyu hana uenyeketi wowote wa usemaji kutwa kuwajaza upepo mashabiki kwakuwapandikiza chuki dhidi ya wapinzani wao wa jadi hovyo kabisaa
Wapinzani ni mapunguani na mbumbumbu wa soka
 
Mbona jana sijaona mashaabiki wakiwapgia makofi wachezaji kuwapongeza kwa kipigo cha 2 km ambavyo huwa wanafaya wakipoteza
Mkuu jana hawakupiga makofi ila walifanya hivi sa sijui ni makasiriko au
1000288659.jpg
 
Back
Top Bottom