Shardcole heshima yako Mkuu
Naomba nitofautine mawazo na wewe na naomba usikwazike tafadhali..
1. Lazima utambue kuwa AFRIMMA ni tuzo zenye hadhi kubwa na kamwe usanii wakitoto hivyo hauwezi kufanyika kiasi kwamba ati unaweza tu kuingia periscope na kujua kwamba wamecheat.. Ukitaka kujua ukubwa wa hizo tuzo angalia orodha ya Sponsors pia angalia jinsi wenzetu wa Afrika Magharibi wanavyoziheshimu!! Huo usanii wa kitoto hivyo ni impossible kufanyika
2. Tuzo za AFRIMMA na AEUSA haziko chini ya DMK kama unavyodai.! DMK ni promota wa matamasha tu na ukaribu wake na Diamond ni kwamba kama haufahamu yeye ndiye meneja wa diamond kwa USA. Lakini hana uwezo na wala sio anayemiliki tuzo za AFRIMMA na AEUSA.. Hii kafanye research tena
3. Kiba ni msanii mzuri ila ana inferiority complex! Nilichogundua ni kuwa akiwekwa category moja na diamond kwenye tuzo yoyote huwa ahamasishi watu wampigie kura coz anaamini diamond atachukua alafu ataonekana alikuwa anaitaka tuzo alafu ameikosa so suluhisho anaonaga bora asihamasishe kabisa.. Mfano tuzo hizi alikaa kimya lakini angalia jinsi anavyo hamasisha apigiwe kura MTV Ema coz kule yuko peke yake diamond hayupo!!
Kiba anatakiwa aanze kujiamini
4. Kiba pamoja na mashabiki na menejimenti yake wanatakiwa wakue kiakili na kimikakati! Waache utoto wa kutupia wengine lawama pale wanapofeli kimikakati na kushindwa kufikia malengo.. Wakiendeleza huu utoto baada ya mwaka mmoja watajikuta mtaani watu wanabishana kiba na harmonize nani mkali?? Hata Rayvany hadhi yake atajikuta iko juu kuliko yeye..
Mwanaume ukishindwa kufikia malengo unakaa chini unajitathimini sio kutupia wengine lawama.!!
Steve Jobs aliwahi kuwaambia wafanyakazi wa Apple kuwa wanatakiwa waache mawazo mgando kuwa ili Apple ifanikiwe inabidi Microsoft wafeli! Hayo ni mawazo finyu coz Apple inaweza kufanikiwa hata Microsoft nayo ikiwa inafanikiwa..
The same nawaasa team kiba, waache kufikiria kuwa ili kiba awe juu ati inabidi WCB washuke! Mimi nasema hapana, kiba anaweza akafanikiwa hata WCB ikiendelea kuwa juu.. Pia achukue WCB kama mfano kwake jinsi wenzake wanavyopanga mikakati na kuitekeleza! Hiyo ndio positive mentality