Ali Kiba ahujumiwa tuzo za Afrimma. siri yafichuka

Ali Kiba ahujumiwa tuzo za Afrimma. siri yafichuka

Aje imetoboa wapi? acha kujidanganya aje ni nyimbo maarafu tanzania na kenya , hapo Uganda kwenye haina umaarufu
Juzi alikiba anasema mkubwa kuliko Wizkid wanaijeria wanauliza alikiba ndo nani
Ngoja akaperform aje kule mtv mama uone kama umepenya

Ok basi ngoja niseme unachopenda kusikia, Salome na collabo la pepa wemba ndiyo zimetoboa Africa hahaha
 
Pole Ali Kiba kwa kuhujumiwa! Inabidi ukaoge maji ya baharini manake naona mdudu wa kuhujumiwa anazidi kukufuata! Mara unazimiwa mic; mara kwa mwaka wa pili mfululizo unadhulumiwa tuzo zako! Mara Sallam akupokonye collabo yako na Ne-Yo!! Yaani watu wana roho mbaya... bora ukashiriki zako Grammy Awards tu kama mambo yenyewe ndo haya!!!
 
Shardcole heshima yako Mkuu
Naomba nitofautine mawazo na wewe na naomba usikwazike tafadhali..

1. Lazima utambue kuwa AFRIMMA ni tuzo zenye hadhi kubwa na kamwe usanii wakitoto hivyo hauwezi kufanyika kiasi kwamba ati unaweza tu kuingia periscope na kujua kwamba wamecheat.. Ukitaka kujua ukubwa wa hizo tuzo angalia orodha ya Sponsors pia angalia jinsi wenzetu wa Afrika Magharibi wanavyoziheshimu!! Huo usanii wa kitoto hivyo ni impossible kufanyika

2. Tuzo za AFRIMMA na AEUSA haziko chini ya DMK kama unavyodai.! DMK ni promota wa matamasha tu na ukaribu wake na Diamond ni kwamba kama haufahamu yeye ndiye meneja wa diamond kwa USA. Lakini hana uwezo na wala sio anayemiliki tuzo za AFRIMMA na AEUSA.. Hii kafanye research tena

3. Kiba ni msanii mzuri ila ana inferiority complex! Nilichogundua ni kuwa akiwekwa category moja na diamond kwenye tuzo yoyote huwa ahamasishi watu wampigie kura coz anaamini diamond atachukua alafu ataonekana alikuwa anaitaka tuzo alafu ameikosa so suluhisho anaonaga bora asihamasishe kabisa.. Mfano tuzo hizi alikaa kimya lakini angalia jinsi anavyo hamasisha apigiwe kura MTV Ema coz kule yuko peke yake diamond hayupo!!
Kiba anatakiwa aanze kujiamini

4. Kiba pamoja na mashabiki na menejimenti yake wanatakiwa wakue kiakili na kimikakati! Waache utoto wa kutupia wengine lawama pale wanapofeli kimikakati na kushindwa kufikia malengo.. Wakiendeleza huu utoto baada ya mwaka mmoja watajikuta mtaani watu wanabishana kiba na harmonize nani mkali?? Hata Rayvany hadhi yake atajikuta iko juu kuliko yeye..
Mwanaume ukishindwa kufikia malengo unakaa chini unajitathimini sio kutupia wengine lawama.!!

Steve Jobs aliwahi kuwaambia wafanyakazi wa Apple kuwa wanatakiwa waache mawazo mgando kuwa ili Apple ifanikiwe inabidi Microsoft wafeli! Hayo ni mawazo finyu coz Apple inaweza kufanikiwa hata Microsoft nayo ikiwa inafanikiwa..
The same nawaasa team kiba, waache kufikiria kuwa ili kiba awe juu ati inabidi WCB washuke! Mimi nasema hapana, kiba anaweza akafanikiwa hata WCB ikiendelea kuwa juu.. Pia achukue WCB kama mfano kwake jinsi wenzake wanavyopanga mikakati na kuitekeleza! Hiyo ndio positive mentality
Amekuelewa
 
Mleta uzi ungefanua vizuri kuhusu vigezo vinavyozingatiwa...pengine kura ni moja ya vigezo ila vipo vingine zaidi.
Japo sio mfuatiliaji sana ila kuna kitu inautwa MAJAJI..Pia wana nafasi kubwa
 
Habari wakuu!

Ule msemo kuwa mziki umetawaliwa na kila aina ya ghilba, fitna ,figisu na kila aina ya uchafu sasa umetimia.

Itakumbukwa mwaka jana msanii wa Bongoflava Alikiba aliandika ujumbe kwenye page yake instagram kuwa "kuna watu wanajaribu kupoteza pesa zao kwa kuhonga waandaji wa tuzo ili kumshusha Kiba kimziki",

Kauli hiyo ilipingwa vikali na mahasimu wake kimziki ikiwemo genge la WCB. Lakini kwa wenye akili tuliamua kuchukulia suala hilo for profit na kuanza kutafutia ukweli juu ya hilo.

Ni mwezi August 2016 ambapo waandaaji wa tuzo za Afrimma walitoa majina ya wasanii waliochaguliwa kushiriki huku Diamond na Alikiba wakiwa ni watanzania waliokuwa wapo katika category ya "Best east Africa male", Kama tulivyoshuhudia juzi matokeo yake yamegubikwa na ukungu mzito hasa ukizingatia Msanii alikiba ndiye aliyekuwa anaongoza kwa kura kwa zaidi ya robo na kuwapiga gap washiriki wenzake wote katika category hiyo. Mshindi aliyetangazwa si halali na hilo limebainika baada ya miongoni mwa vijana wazalendo wa IT waliokuwa wakiendesha zoezi hilo kufichua siri hiyo kupitia mtandao wa perscope.

Swali la kujiuliza, hawa wanaonunua tuzo wanapata faida gani? Maana kama graph ya msanii wao kimziki inashuka je njia sahihi ni kufanya fitna za namna hii?

Mhusika mkubwa wa hujuma hizi ni ni promoter mtanzania anayeishi USA anayejulikana kwa jina la DMK ambaye yeye na Alikiba ni mwaka sasa wamekuwa na mgogoro wa kimaslahi baada ya Alikiba kukataa kutumika kama rubber stamp kwa kupiga show zenye maslahi madogo, kwahiyo hii inasadikiwa kuwa ni sababu ya promoter huyo kumuhujumu Alikiba, hivyo msitarajie hata siku moja mkamsikia Alikiba akiwa ameshinda kwenye tuzo zozote zilizopo chini ya promoter Dmk, tuzo kama Afrimma USA, AEUSA.

[HASHTAG]#JusticeForKiba[/HASHTAG] [HASHTAG]#SolidarityForever[/HASHTAG]
MONDI AKA DOMO ANAJULIKANA KWA FITINA HILO LIPO WAZI
 
Mleta uzi ungefanua vizuri kuhusu vigezo vinavyozingatiwa...pengine kura ni moja ya vigezo ila vipo vingine zaidi.
Japo sio mfuatiliaji sana ila kuna kitu inautwa MAJAJI..Pia wana nafasi kubwa
Ukipata jibu la hili swali with reference, tafadhali naomba uni-tag ili nije kuongeza ilmu!
 
Hebu tusaidie hiyo link inayoonesha idadi ya kura kwa kila mshiriki. Other wise ni maneno ya mkosaji tu.
 
Hebu tusaidie hiyo link inayoonesha idadi ya kura kwa kila mshiriki. Other wise ni maneno ya mkosaji tu.
Nimemuomba Tmuller ani-tag akipata jibu la swali lake! Tafadhali Mkuu; na wewe ukipewa hiyo link naomba uni-tag ili nami nipate darsa!
 
Wenzenu WCB na Navy Kenzo wana group zaidi ya 20 za kupiga kura, na kila member wa group anapiga kura 20 kwa siku. Nyie team Kiba mnaishia lawama na kuona mnaonewa. Mziki wa sasa siyo wa mazoea tena. MZIKI UNATAKA YAFUATAYO.
1. Promotion.
2. Good management.
3. Creativity.
4. Team work.
5.Interaction and
6. Cooperation.
Sasa Kiba hayo yote hayupo anategemea miujiza. Abadilike na aache lawama, akubali kuwa chini ya watu ili afanikiwe. Wenzenu wataimba hadi ngonjera na kung'aa Nyie mtaendelea kutunga na kuimba vizuri mtaishia Kenya.
 
nyie mnaojiita team kiba mtampoteza kabisa huyo star wenu, acheni kumtia moyo kiba kwa kusingizia vigezo visivyo eleweka kama kashindwa kubalini na mumwambie akaze buti na ajiulize kwanini yeye tu kila siku anaonewa sio mnatengeneza hoja zisizo na macho wala miguu kumtetea
 
Eti kiba hajapata nomination hata moja mtvmama, hivi wewe umelewa viroba au? Best collaboration n song of the year

Usipaniki Mkuu na wala hakuna haja ya matusi..
Nazidi kukusisitizia kuwa Kiba hajawa nominated MTV MAMA, hizo nomination ulizozitaja wanaostahili pongezi ni Sauti Sol sio Kiba coz yeye ameshirikishwa tu! Nitashangaa kama Kiba akifurahi na kuruka ruka kwa nomination za Sauti Sol..
 
Mbali tu na mtvmama, jua kiba yupo nominated mtvema tuzo kubwa duniani kuliko hivyo viafrimma vyenu, ndiomana Olamide alisema anaona fahari kuwa nominated MTVEMA kuliko tuzo nyingine yeyote mwaka huu.

kama hujui MTVEMA ni kitu gani, kawaulize mabos wako , yani kiafrica hakuna msanii asiyetaman MTVEMA na BET, take it in your mind usije ukachekwa bure.

Meza mate Mkuu, relax, breathe in..

Now let's talk; sio sahihi kuwalingishia WCB kuwa Kiba ametajwa kuwania tuzo ya MTV EMA coz wenzenu diamond mwaka jana tu sio tu kwamba alikuwa nominated pekee bali pia alishinda tuzo hiyo na kuirudisha Tanzania..

Mkuu narudia tena kukushauri, Menejimenti ya Kiba inatakiwa iwe ni mikakati na mipango madhubuti!! Kiba akiendeleza chuki na Majungu siku si nyingi atapotea kabisa..
 
Eti kiba hajapata nomination hata moja mtvmama, hivi wewe umelewa viroba au? Best collaboration n song of the year

Mbali tu na mtvmama, jua kiba yupo nominated mtvema tuzo kubwa duniani kuliko hivyo viafrimma vyenu, ndiomana Olamide alisema anaona fahari kuwa nominated MTVEMA kuliko tuzo nyingine yeyote mwaka huu.

kama hujui MTVEMA ni kitu gani, kawaulize mabos wako , yani kiafrica hakuna msanii asiyetaman MTVEMA na BET, take it in your mind usije ukachekwa bure.
Wewe ndo unaiona kubwa leo?
Diaomond hiyo mtv ema kachukua 2 ,mtv ema europe na world wide ipo madale pale
 
Eti kiba hajapata nomination hata moja mtvmama, hivi wewe umelewa viroba au? Best collaboration n song of the year

Mbali tu na mtvmama, jua kiba yupo nominated mtvema tuzo kubwa duniani kuliko hivyo viafrimma vyenu, ndiomana Olamide alisema anaona fahari kuwa nominated MTVEMA kuliko tuzo nyingine yeyote mwaka huu.

kama hujui MTVEMA ni kitu gani, kawaulize mabos wako , yani kiafrica hakuna msanii asiyetaman MTVEMA na BET, take it in your mind usije ukachekwa bure.
Kiba hana nomination mtv mama tuzo inatoka moja kama wakishinda inaenda sauti sol, mtv wanajua nyimbo ya sauti sol
 
Bado kuna safari ndefu sana
Alikiba na Diamond wote ni watanzania na wote wanajua Mziki, Wapeni sapoti Vijana wenu.
Kwa kauli hizi ambazo nimeziona humu, hakika bado tuna safari ndefu sana ya kufika kule tuendako.
Mimi nilidhani kama umekwenda shule ukiingia ktk Biashara unaangalia namna ya kuaply SWOT Analysisi,
sasa mara figisu,
Mara uchawi,
Mara Maiki,
Penye riziki hakukosi fitina, hii ni biashara kama biashara nyingine. Kwa hiyo fitina ziwepo au zisiwepo ni changamoto za kawaida, Cha msingi ni kujipanga.
Kama hujifunzi kutokana na makosa usitarajie ipo siku utapiga hatua.
Siku zote watu wanapokufananisha na mwingine JUA bado hujafanya tofauti, Fanya vitu adimu(huwezi kupata kitu ambacho wengine hawana bila kufanya ambacho wao hawajawahi kufanya). Piga hatua kali zaidi!
Ni ngumu sana kukubalika na watu, inabidi upige hatua mpaka wakushangae.
Haya Mambo ya figisu ooh mara anabebwa yalikuwaga primary, wengi wetu tuliyapitia. Lakini unajua kile ambacho tulikuwaga tunafanya,
Unapiga mpaka hakuna wa kukuangalia tena, yani unatengeneza gap mpaka wanaogopa kukuangalia.

Kwa hiyo whether team kiba au team mond, Muhimu ni kushauri Vijana wetu wafanye kazi ambazo hazikuwahi kufanyika ili akitoa ngoma moja inatoboa vizazi na vizazi, mimi nitafurahi sana kama siku moja mtanzania atatengeneza nyimbo kali kwa lugha yeyote ile ili ifikishe VIEWS at least BILLION MOJA. That might be history in Africa as at 21st century Tunakuweka ktk kumbukumbu muhimu duniani.

So tusiwavunje moyo, acheni kuwafananisha kwa sababu kila mmoja is best at his own.
 
Kiba hana nomination mtv mama tuzo inatoka moja kama wakishinda inaenda sauti sol, mtv wanajua nyimbo ya sauti sol

Hahahahaha hapa ndio unafiki wenu unapojulikana, ikitokea huo wimbo upate tuzo mtasema wimbo ni wa sautsol kiba hausiki ila ikitokea huo wimbo ukose tuzo mtasema kiba kakosa tuzo. Hahahahahahahaha wanafiki ninyi, tulia tuwanyooshe coz mlizoea vya kunyonga kwenye vi afrimma vyenu.
 
Back
Top Bottom