Nakubali hakuna linaloshidikana ila kwa muziki wetu kwenye soko lilivyokaa kutoboa kwenye world cup 2022 ni ngumu, wa Nigeria nao wana lobbyist wao na wamefanikiwa kuaminisha ulimwengu kuwa ukija Africa mziki mzuri utakaoukuta ni ule wanaoimba, Ali Kiba kwa album yake hii alistahili angalau hata wimbo mmoja upenye Billboard hot 100 lakini ni ngumu sana kwa hilo kutokea, sasa hivi Nigeria wana Wizkid Essence # 11 na Ckay Love Nwantiti #50, ila Ali Kiba akikaa nao hao kina Wizkid, Ckay, Burna Boy etc. studio ana uwezo wa kwenda nao spidi moja kama sio kuwakalisha kabisa, ila ndio hivyo soko waliolishikilia ni wengine.