Ali Kiba amlalamikia Sallam SK kuwa anahusika na kuzimika kwa 'mic' Mombasa

Ali Kiba amlalamikia Sallam SK kuwa anahusika na kuzimika kwa 'mic' Mombasa

Mbona jibu liko wazi tuuuu.... Wakat kiba anaperform chriss brown alikuwa anasubilia backstage... Sasa ulitaka SK aonekane wapi zaidi ya uko uko backstage alipokuwepo Chris brown?????!!! Kibakuli aache uswahili
 
hahahahaha sababu za kiba ni za kitoto alitakiwa kuzipeleka lawama zake kwa mhandinsi wa sauti wa hiyo show si salam sk kama Salama sk alikuwepo back stage na akaachwa basi ni wazi hakukuwa na tatizo ndio maana hawakumuondoa....
Nilitegemea lawama ziende kwa waandaaji wa show na si kwa Salam sk
 
Huyu jamaa anafeli sana kwa wivu usio na msingi. It's obvious kuna foul play, ila Diamond na team yake hawana juice ya kufanikisha kitu kama, nor do they have a reason to anyway.

Kilichotokea, ni technical foul-play kutoka kwa waandaaji. Ni wazi hawakujipanga, na Kiba akatolewa kafara.

Cha kufanya, ni Kiba kuwabana waandaaji kupitia makubaliano yao(kama yapo), na jamaa watoe report ya kilichotokea na kumsafisha mshkaji, pengine wamlipe fidia. Otherwise, hili ni doa kubwa kwa msanii wa level yake, na anazidi kuchafua kwa kutoficha upumbavu wake.
Leo ndio nimeamini jamaa hayuko sawa kichwani yani kuzimika mic unatoa lawama kwa Salam wakati ulitakiwa kuwalaumu waandaaji wa show,,
 
Tatizo ni ssalaam alifata nini backstage.... alienda kama nani.. na kufata nini. Na ili iweje.. aliiitwa? Alikiba keep cool ur talented than one they compare to...
Kama uwepo wake ulikuwa sio ruhusa basi wala asingalikuwepo pale... kwa hiyo bado naziona sababu za kiba ni za kijinga na kitoto, hivi salam ndio alikuwa mhandisi wa sauti wa hiyo show?
 
Huyo meneja wa Diamond alikuwa ana kazi gani backstage?

Kama hakuna sababu ya msingi yeye kuwa huko then kwa nini alihusishwe na huu uhuni?

Hao waandaaji nao wenge kweli,mtu asiyehusika anafanyaje huko backstage?
 
hivi kiba na Simba na Yanga wana undugu?
maaan miaka nenda rudi wanategemea mapato ya milangoni
 
Wakuu mnakumbuka tukio la Kiba kuzimikiwa na mic kwenye tamasha la Mombasarocks?

Akihojiwa na kipindi cha Mseto Citizen na mzaz Willy Tuva, Kiba alidai kuzimika kwa mic yaweza kuwa ni figisu za Sallam SK yule meneja wa Diamond coz kipindi anapafomu SK alikuwa nyuma ya stage.







Inafika wakati tuseme tu kuna baadhi ya wanamuziki hapa hawajitambui, tena wana fikra za kitoto sana. Wamezoea kuongea chochote wanachojisikia, bila hata ya kujua wao ni kina nani. Wanachokisema kina uhakika gani na kitaleta athari ipi. Yaani unaficha ukweli na kuongea kingine ambacho huna uhakika nacho. Alikiba wewe ni msanii mkubwa hapa Tanzania, ila katika siku niliyokudharaua na kukuona hujitambui basi ni baada ya kungea kitu kama hicho.

Unastaajabu Meneja wa Diamond kuwa kule backstage, ilihali inajulikana wazi yule Bwana yupo kimazungumzo na Msanii wa nje. Kazi ya Meneja inambidi atafute fursa kwa Msanii wake ndiyo maana akawepo kule. Hebu ifike kipindi masuala ya kushuku vitu tuache jamani, pale ni kioo cha nchi yako. Mawazo uliyoyatoa ya kuhisi, ndiyo wazawa wa nchi ile pamoja na wengine kutoka sehemu tofauti wanatuhisi watanzania wote tuna akili zile. Si unajiaibisha bali tu unalitia choo Taifa lako .

Hebu jiulize Maikrofoni kama ile ataweza vipi azime, kipaza sauti kisicho na nyaya yeyote. Si vipazasauti va kipindi cha DDC Mlimani pack au enzi zile Bi Patricia Hillary anavuma na kibao cha Njiwa peleka salamu.

Kifaa kama kile kina betri ndani yake hiyo ndiyo inayoifanya iwake, kuzima pale kuna swichi yake chenyewe. Kifaa hiki hadi kije kupata mawimbi ya kuleta asauti, basi inabidi kuwe na 'connector' yake iliyopo kwenye miksa. Hiyo ndiyo inachomekwa kwenye miksa na kuonoza zaidi ya vifaa vingi vya aina ile. Hapo utajua kabisa Mikasa inakaa kwa nani? Hivyo DJ ndiyo kafanya yote yale, au kama si yeye basi ni Sound Engineer.
Je Sallam SK alifika huko kilipo hicho kiunganishi cha Maikrofoni?
Hebu ungepata uhakika kwanza kabla hujaongea, ukumbuke ile si show ya kawaida bali ni ya kimataita. Huko vilipo vitu vyote kuna walinzi, hadi wahusika wenye kuongoza ratiba ya shughuli nzima. Je Walinzi walimuacha tu azime badala ya kumkamata?


Jamani hivi si Msanii wetu alihitajika ashuke jukwaani, Chris Brown alikuwa na haraka. Ndiyo maana waongozaji show nzima wakaamua kumzimia Maikrofoni. Hapa inaonesha wazi alipewa taarifa ila hakusikiliza, ndiyo maana wakaamua kutumia uamuzi huo. Wadau mimi ninapenda niangushe lawama zangu zote kwa waandaaji wa show ile. Kiasi cha kumvunjia mtu ratiba kisa tu jamaa wa nje anataka kuondoka, tena afanye show wakati ambao si ratiba yake. Hapa inaonesha ni kiasi gani mnawatukuza hao, si mlikubaliana ufike muda fulani ndiyo apande jukwaani. Vipi mtaenda kinyume na mapatano wenu. Yaani Alikiba ashuke kisa yeye aimbe halafu baadaye aje kupanda kumalizia show yake, ama kweli waafrika bado sana tunaendeshwa.


Mwisho, huyo Mtajwa na kuhisiwa hakuwa na hatia yeyote ile. Vioo vya Mbari alimarrufu kama wasanii. Tukiongea kitu basi tufikiri, jamii imewapa nafasi ya kipekee wengine mkiongea mnaonekana ni wenye uwezo mkubwa kimawazo. Hadi watu wanakaa kukusikiliza utasema nini, kuropoka huko kujishusha hadhi na kuaibisha nchi yako. Majagina wa tasnia hivyo, hawakuwa hivyo hebu walau mjifunze kupitia wao



Hassan O Mambosasa
Dar es salaam
Tanzania
 
Kuna mambo mengine kama haya ndio huwa tunasema uswahili. Alikiba anashangaa meneja wa Diamond kukaa backstage, na eti anahoji kwa nini asingekaa VIP kama ishu ni kuona shoo. Hivyo kwa mtazamo wake yeye Alikiba anahisi meneja wa Diamond ndiye aliyezima Mic. Katika hali ya kawaida tu hivi inawezekana meneja wa Diamond akazima Mic kwenye hughuli isiyo yake? Anyway tuachane na uswahili wa Alikiba na pengine ndio maana anashindwa kufanya mambo makubwa katika muziki pamoja na ukongwe alionao katika muziki.

Kazi ya kuwa meneja wa mwanamziki ni kubwa sana kama unamua kujishughulisha na kuhakikisha mwanamziki wako unayemsimamia anafika mbali. Sote tunaelewa ni jinsi gani WCB walivyo wanzuri wa kutumia kila aina ya upenyo wanaopata katika kuhakikisha kazi zao zinafika mbali. Chris Brown kaja Kenya pamoja na uongozi wake, hivi mlitegemea Sallam akae tu ametulia, au akae VIP ametulia anangalia shoo badala ya kutengeneza contacts na uongozi wa Chris Brown? Hivi Alikiba anajua kweli namna connections na wasanii wa nje zinavyopatikana? Anajiuliza why Sallam akae backstage, heee sasa alifikiri Sallam ataongea na uongozi wa Chris Brown wapi? Mwenzake anahangaika kufanya connections na wasanii wakubwa yeye anakaa kufikiria kwamba mtu anaweza kusafiri kutoka Dar hadi Mombasa kwa ajili ya kwenda kuchomoa Mic. Huu ufinyu wa mawazo ndio unamfanya kila siku aishie kulalamika na kuhisi anahujumiwa. Leo tunapopewa ratiba ya tour ya Diamond na Neyo UK si kazi ambayo imefanyika kitoto, bali watu wametumia fursa na nafasi zinazojitokeza kuweza kutengeneza connections kama hizo. Au tumeshasahau ni namna gani Neyo na Diamond walikutana? Au hatujajua ni namna gani Diamond na Swiss Beats wamekutana?

Kifupi Alikiba ana safari ndefu ya kujifunza kuhusu namna ya kutafuta soko la muziki. Akiendelea kuwa na fikra mgando kama hizo ataishia kulalamika tu na mwishowe atashindwa kufanya vinzuri kwa sababu ya kutaka kushindana na Diamond. Mwenzake Diamond sasa hivi anafocus kwenye soko ya Ulaya maana Afrika ameshamaliza, America ameshaingia, ila yeye Alikiba anawaza kwamba mtu atapoteza hela zake kwenda Mombasa kuchomoa Mic. Daaah kweli tunatofautiana .
Umemaliza yote mkuu
 
so kiba anahisi sallam alienda kuangalia show Mombasa!
if so,ina maana angekuw anatumbuiza diamond yeye meneja wake (hivi anae?)
angekaa VIP kutumbuizwa na chris brown!
NO WONDER HENDI HARUDI!
 
sababu amesema ni 'muda" wa Chris sasa salam ndo alipanga ratiba?
Alifuata nini back stage,ukijua mtu atatafuta sababu kupitia wewe muepuke...ni sawa na wazazi wanapowaambia watoto usicheze na mtoto yule mtakolofishana tu..kwa hiyo ni jukumu lako kumpitia mbali
..
 
Alifuata nini back stage,ukijua mtu atatafuta sababu kupitia wewe muepuke...ni sawa na wazazi wanapowaambia watoto usicheze na mtoto yule mtakolofishana tu..kwa hiyo ni jukumu lako kumpitia mbali
..
alitakiwa akae wapi??
 
Alifuata nini back stage,ukijua mtu atatafuta sababu kupitia wewe muepuke...ni sawa na wazazi wanapowaambia watoto usicheze na mtoto yule mtakolofishana tu..kwa hiyo ni jukumu lako kumpitia mbali
..
Ally Kiba ana matatizo na management yake ina matatizo zaidi
 
Back
Top Bottom