Kuna mambo mengine kama haya ndio huwa tunasema uswahili. Alikiba anashangaa meneja wa Diamond kukaa backstage, na eti anahoji kwa nini asingekaa VIP kama ishu ni kuona shoo. Hivyo kwa mtazamo wake yeye Alikiba anahisi meneja wa Diamond ndiye aliyezima Mic. Katika hali ya kawaida tu hivi inawezekana meneja wa Diamond akazima Mic kwenye hughuli isiyo yake? Anyway tuachane na uswahili wa Alikiba na pengine ndio maana anashindwa kufanya mambo makubwa katika muziki pamoja na ukongwe alionao katika muziki.
Kazi ya kuwa meneja wa mwanamziki ni kubwa sana kama unamua kujishughulisha na kuhakikisha mwanamziki wako unayemsimamia anafika mbali. Sote tunaelewa ni jinsi gani WCB walivyo wanzuri wa kutumia kila aina ya upenyo wanaopata katika kuhakikisha kazi zao zinafika mbali. Chris Brown kaja Kenya pamoja na uongozi wake, hivi mlitegemea Sallam akae tu ametulia, au akae VIP ametulia anangalia shoo badala ya kutengeneza contacts na uongozi wa Chris Brown? Hivi Alikiba anajua kweli namna connections na wasanii wa nje zinavyopatikana? Anajiuliza why Sallam akae backstage, heee sasa alifikiri Sallam ataongea na uongozi wa Chris Brown wapi? Mwenzake anahangaika kufanya connections na wasanii wakubwa yeye anakaa kufikiria kwamba mtu anaweza kusafiri kutoka Dar hadi Mombasa kwa ajili ya kwenda kuchomoa Mic. Huu ufinyu wa mawazo ndio unamfanya kila siku aishie kulalamika na kuhisi anahujumiwa. Leo tunapopewa ratiba ya tour ya Diamond na Neyo UK si kazi ambayo imefanyika kitoto, bali watu wametumia fursa na nafasi zinazojitokeza kuweza kutengeneza connections kama hizo. Au tumeshasahau ni namna gani Neyo na Diamond walikutana? Au hatujajua ni namna gani Diamond na Swiss Beats wamekutana?
Kifupi Alikiba ana safari ndefu ya kujifunza kuhusu namna ya kutafuta soko la muziki. Akiendelea kuwa na fikra mgando kama hizo ataishia kulalamika tu na mwishowe atashindwa kufanya vinzuri kwa sababu ya kutaka kushindana na Diamond. Mwenzake Diamond sasa hivi anafocus kwenye soko ya Ulaya maana Afrika ameshamaliza, America ameshaingia, ila yeye Alikiba anawaza kwamba mtu atapoteza hela zake kwenda Mombasa kuchomoa Mic. Daaah kweli tunatofautiana .