Ali Kiba amlalamikia Sallam SK kuwa anahusika na kuzimika kwa 'mic' Mombasa

Ali Kiba amlalamikia Sallam SK kuwa anahusika na kuzimika kwa 'mic' Mombasa

1476118609568.jpg
 
Msanii wa bongo Fleva Alikiba amemshushia tuhuma nzito meneja wa msanii mwenzie Diamond platnumz maarufu kama Sallam.
Akizungumza na clouds FM katika kipindi cha xxl, alikiba amezumgumza kwa huzuni sana kwamba Sallam ndiye aliyehusika kufitinisha yeye kupokonywa maiki katika jukwaa hilo
Anasema wakati akiwa jukwaani alimuona sallam chini ya jukwaa, hivyo huenda amehusika moja kwa moja katika fitna hiyo.Anasema kama hawana bifu meneja huyo alikwenda Mombasa katika show hiyo kufanya nini?

Haya yamekuja baada ya Alikiba kuperform nyimbo mbili tu na kuzimiwa maiki na kupandishwa msanii mwingine Chriss brown.

Je , tuhuma hizi zinaweza kuwa na ukweli wowote?
SK alienda kumcheck chris wala hakuna sababu ya yey kumlaumu SK
 
Huu ushindani naona sasa si wa kisanaa!! Mnashindana kupanda ila ni vita kuhakikisha mwingine hakubaliki kabisa kisanaa!!

Sasa Salam S. K. alifata nini back stage katika show isiyomuhusu?? Sidhani kama atakwepa hizi tuhuma for sure
Kwani sallam kua back stage kuna muuma nini kiba..?
 
Kuna mambo mengine kama haya ndio huwa tunasema uswahili. Alikiba anashangaa meneja wa Diamond kukaa backstage, na eti anahoji kwa nini asingekaa VIP kama ishu ni kuona shoo. Hivyo kwa mtazamo wake yeye Alikiba anahisi meneja wa Diamond ndiye aliyezima Mic. Katika hali ya kawaida tu hivi inawezekana meneja wa Diamond akazima Mic kwenye hughuli isiyo yake? Anyway tuachane na uswahili wa Alikiba na pengine ndio maana anashindwa kufanya mambo makubwa katika muziki pamoja na ukongwe alionao katika muziki.

Kazi ya kuwa meneja wa mwanamziki ni kubwa sana kama unamua kujishughulisha na kuhakikisha mwanamziki wako unayemsimamia anafika mbali. Sote tunaelewa ni jinsi gani WCB walivyo wanzuri wa kutumia kila aina ya upenyo wanaopata katika kuhakikisha kazi zao zinafika mbali. Chris Brown kaja Kenya pamoja na uongozi wake, hivi mlitegemea Sallam akae tu ametulia, au akae VIP ametulia anangalia shoo badala ya kutengeneza contacts na uongozi wa Chris Brown? Hivi Alikiba anajua kweli namna connections na wasanii wa nje zinavyopatikana? Anajiuliza why Sallam akae backstage, heee sasa alifikiri Sallam ataongea na uongozi wa Chris Brown wapi? Mwenzake anahangaika kufanya connections na wasanii wakubwa yeye anakaa kufikiria kwamba mtu anaweza kusafiri kutoka Dar hadi Mombasa kwa ajili ya kwenda kuchomoa Mic. Huu ufinyu wa mawazo ndio unamfanya kila siku aishie kulalamika na kuhisi anahujumiwa. Leo tunapopewa ratiba ya tour ya Diamond na Neyo UK si kazi ambayo imefanyika kitoto, bali watu wametumia fursa na nafasi zinazojitokeza kuweza kutengeneza connections kama hizo. Au tumeshasahau ni namna gani Neyo na Diamond walikutana? Au hatujajua ni namna gani Diamond na Swiss Beats wamekutana?

Kifupi Alikiba ana safari ndefu ya kujifunza kuhusu namna ya kutafuta soko la muziki. Akiendelea kuwa na fikra mgando kama hizo ataishia kulalamika tu na mwishowe atashindwa kufanya vinzuri kwa sababu ya kutaka kushindana na Diamond. Mwenzake Diamond sasa hivi anafocus kwenye soko ya Ulaya maana Afrika ameshamaliza, America ameshaingia, ila yeye Alikiba anawaza kwamba mtu atapoteza hela zake kwenda Mombasa kuchomoa Mic. Daaah kweli tunatofautiana .
Asante mkuu umemaliza
 
Je kama alibeba hizi alifuata nn na wakati msanii wake hakuwepo kwenye shoo
Alibeba hizi nini..? ...uliambiwa kwenda sehem mpaka hawepo msanii wake..?...unajuaje je kama alienda kwa ajili ya connection ya mziki kwa ajili ya msanii wake...?

Afu kiba analalamika kwani yeye ndo mmliki wa show...mpaka salam kwenda back stage basi alikua na makubaliano na wenye show..kiba aache lawama afanye kazi zake
 
Kiba hana jipya kapagawa na Mic za kenya tu,asepe zake na hizo 43m akazifaidi jojo.
 
Tatizo la kuwa cheap/kulipwa pesa kidogo ndo hilo. Kwa mujibu wa habari ni kwamba wizkid alilipwa 4 mil ktsh na kiba ni 2 mil ktsh. Hapa utaona kwanini mic hakuzimwa kwa wiz na walisubiri mpk amalize kuimba nyimbo zake alizozipanga. Utakavyojiweka ndivyo thamani yako itakavyokua. Kama wote wangelipwa pesa inayofanana nadhani waandaaji wangethamini pia pesa yao kwa kuarrange vema muda wa kuwapandisha jukwaani. Sioni sababu ya kiba kumlalamikia Sallam coz yeye hakuwa muandaaji wa show. Nadhani ingekua muhimu zaid kuwalalamikia walioandaa show ikiwezekana awashitaki ila kumlalamikia Sallam daaah!! umechemka mfalme Kiba.
 
Mhh au ndio mambo ya okokokorobo na papa Wemba!
yanatokea sana hayo mambo ya papa wemba mfano ingetokea tunge mlaumu nani kama sio huyo meneja kilichompeleka nini hiooo inaweza kuwa michongo dunia imebadilika now
 

Kazi ya kuwa meneja wa mwanamziki ni kubwa sana kama unamua kujishughulisha na kuhakikisha mwanamziki wako unayemsimamia anafika mbali. Sote tunaelewa ni jinsi gani WCB walivyo wanzuri wa kutumia kila aina ya upenyo wanaopata katika kuhakikisha kazi zao zinafika mbali.

Chris Brown kaja Kenya pamoja na uongozi wake, hivi mlitegemea Sallam akae tu ametulia, au akae VIP ametulia anangalia shoo badala ya kutengeneza contacts na uongozi wa Chris Brown? Hivi Alikiba anajua kweli namna connections na wasanii wa nje zinavyopatikana? Anajiuliza why Sallam akae backstage, heee sasa alifikiri Sallam ataongea na uongozi wa Chris Brown wapi?

Mwenzake anahangaika kufanya connections na wasanii wakubwa yeye anakaa kufikiria kwamba mtu anaweza kusafiri kutoka Dar hadi Mombasa kwa ajili ya kwenda kuchomoa Mic. Huu ufinyu wa mawazo ndio unamfanya kila siku aishie kulalamika na kuhisi anahujumiwa. Leo tunapopewa ratiba ya tour ya Diamond na Neyo UK si kazi ambayo imefanyika kitoto, bali watu wametumia fursa na nafasi zinazojitokeza kuweza kutengeneza connections kama hizo. Au tumeshasahau ni namna gani Neyo na Diamond walikutana? Au hatujajua ni namna gani Diamond na Swiss Beats wamekutana?

Kifupi Alikiba ana safari ndefu ya kujifunza kuhusu namna ya kutafuta soko la muziki. Akiendelea kuwa na fikra mgando kama hizo ataishia kulalamika tu na mwishowe atashindwa kufanya vinzuri kwa sababu ya kutaka kushindana na Diamond. Mwenzake Diamond sasa hivi anafocus kwenye soko ya Ulaya maana Afrika ameshamaliza, America ameshaingia, ila yeye Alikiba anawaza kwamba mtu atapoteza hela zake kwenda Mombasa kuchomoa Mic. Daaah kweli tunatofautiana .

Maboso,
Yaani watu wasipoelewa ulivyoainisha kazi za meneja wa msaniii au mwanamuziki basi wa-Tanzania tutakuwa na matatizo kama ya AliKiba. Pia hii show haikuandaliwa na Ali Kiba bali ma-sponsor na menejimenti wa Chris Brown wanahusika sana na hapo kuna fursa kibao za kibiashara kufanya contact na WCB kupitia kwa Sallam.
 
Je kama alibeba hizi alifuata nn na wakati msanii wake hakuwepo kwenye shoo
Kuna kitu kinaitwaa connection, breezy msanii mkubwa sana pengine manager wa diamond alitaka au alikua na mazungumzo na msanii huyo, ni mtazamo tuu na sii kingine, kwanza manager wa kiba alkua wapi? Ina maana kiba hana team backstage iwapo ana perform kuangalia mambo yanaenda sawa kama walivyopanga? Au kiba alkua solo kwenye tamasha kubwa kama hili? ....... Ni mtazamo pia
 
Back
Top Bottom