Ali kiba azungumzia suala la Cheed na Killy kujitoa Kings Music

Wangapi tujuane ili twende chuo cha alkiba cha kukuza sanaa, bila kusainishana.

Yoooooo yeeebaba, hapendi show off na pia hataki pesa, ila anataka awe international artist haitokaa iwezekane.

Mwenye picha ya wacheza na majeneza naitafuta jmn, anitag #zuchu
 
Wameshare Hana pesa ya Kumiliki
Media labda Youtube chanel na blog

Kwahiyo kama anashare ndio hana haki ya kuitwa mmiliki wa hiyo media?? nyie watu mna wivu sana na chuki zimewajaa...ajabu sasa hapohapo mnasema Majizo ndio mmiliki wa Efm lakini mnajisahaulisha na yeye ni ana share tu pale Efm hapohapo Mnamuita kusaga ni mmiliki wa clouds lkn mnajisahaulisha kuwa nae ni mwanahisa tu pale clouds...
 
Waambie hao ni kampuni chache sn zina mmilik .mmoja
 
Darlin hawezi kukuzwa kisanii na Diamond.
Darlin ni msanii way back 2000's huko keshaimba na Ali kiba, abby skills(nafikiri huyu ndo mzazi mwenzake) Nafikiri Domo alikuwa anahangaika na mitumba.
Enzi hizo ukiongelea Alikiba na Sharobaro rexords balaa.
Kwin dalini amekuzwaje kisanaa na ndugu yake Diamond, au unaropoka tu
 
Kitu nisichokielewa ni sababu rasmi za hao kujitoa na walikuwa wanapata hasara gani na faida gani huko Kings na King naye anapata hasara gani au faida gani kwa kujitoa hao.watu wanapata shida kuchangia coz wahusika na km ilivyokawa Kiba haweki mambo wazi sana
 
Naona kuna shida kubwa hawataki kusema hivi usiku kama huo unaniamsha et nikutoe kwenye lebo? Kwan ulivamiwa?au kuna mtu kakujaza ushawishi umeona kabla hujasahau uje haraka? Nimejiuliza tu hivi naona wanamumunya maneno
 
Huwezi kusaini contract kama huna elimu, hapa ndiyo tunapo ona wabongo wengi wakilia lia wanadhulumiwa...

hata Huko serikalini ndiyo ujinga ujinga mfano angalia mikataba ya madini..
 
Ukiskiza interview yake kwa makini utagundua kuwa jamaa kakasirika sana wao kujitoa na hata kwenye mazungumzo yao ya kujitoa yalikua mafupi mno, wala hakukua na negotiation ni kama alishtukizwa hivi, na kasema hataki warudi kwenye label yake tena. Sasa najiuliza ile ilikua ni biashara ya muziki au ni kitu gani?
 
Diva chawa sana kamgeuka Alikiba naskia huko insta Diva ametuma screenshot ya Alikiba akimtongoza ili tu amuumbue na inaelekea hii mipango ya madogo kuondoka kaisuka yeye mwanamke mbaya sana yule...mdogo wetu Konde boy ajiangalie sana kuwa na marafiki wa sina hii aisee
 
Wameshare Hana pesa ya Kumiliki Media labda Youtube chanel na blog
mwenzako ana shares wasafi radio, TV, na anamiliki label kubwa ya muziki - WASAFI. Yeye Kiba ana share wapi? Na hiyo label yake isiyoweza kutoa hata video ya kutambulika MTV [emoji1] [emoji1] hiyo tu label yake inamshinda hata makao makuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yawezekana interview ni nzuri, ila haijanivutia kuiangalia yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…