Ali Kiba dharau zitakuponza, heshimu kitu cha bure

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
INAGHARIMU SHILINGI 0.00 KUWAHESHIMU WATU WENZAKO

Kujiheshimu na kuheshimu wengine ni mmoja ya nguzo kuu katika mafanikio, Hii imedhihirishwa tena baada ya msanii Ali kiba kuwa katika skendo mbali mbali za kudharau watu wengine na kujiona yeye ndio mwamba kitu ambacho kimehaaribu sana muziki wake.

Ikumbukwe ya kwamba Ali Kiba hayupo socially interractive lakini hili pekee sio la kumfanya asiweze kuheshimu wenzake, Naposema huyu hayupo socially interractive ni kwamba sio mtu wa kujichanganya changanya na watu na ndio maana kuna kipindi menejimenti yake ilimwambia ajaribu kupata mashabiki zaidi kupitia kuwa socially interractive, Hatua ya kwanza hii walianza kumfanya Ali Kiba apande dala dala ajimix na watu lakini ilikuwa ni dhahiri kaisa huyu kaka mkubwa alikuwa anavumilia tu kuwemo kwenye dala dala,,,Tizama hapa
Kuna kipindi msanii mwenzake Harmorapa alienda kumpokea airport na alikuwa ame mwandali alikiba t-shirt kaisa lakini unajua kilitokea nini, Unaambiwa ali kiba aliikataa akafunga kioo cha gari ila baada ya muda kidogo inadhaniwa kwamba management yake ilimlazimisha tu aichukue hio t-shirt
Wiki kadhaa zilizopit tulishuhudia live bila chenga msibani, Msanii Diamond alipofika mibanid na kuanza kusalimiana na wenzake kwa heshima ya kupeana mkono kwa mkono hali ilikuwa tofauti kwa Ali kiba ambae alitoa kiganja pale alipopewa mkono wa salamu, Hili tukio lilikuwa ni wazi kabisa kaka braza ana dharau mno
Ali Kiba ni Mswahili na amekulia Uswahilini ila cha ajabu hawezi kuishi Kiswahili.
Kubwa zaidi wanaomzunguka hawampi Ushauri wa kumjenga ama hakubali kushauriwa.
Hivi anapungua nini akijishusha kwa Jamii inayomzunguka ambao ndo Mashabiki zake? Au kuitwa King ndo anaona amemaliza kila kitu?
Bado anahitaji kujifunza zaidi lasivyo atazidi kupoteza Mashabiki zake!
 
Acheni uchawi wenu na timu yenu ya kishetani mnatumia nguvu kumshusha kiba ila hamuwez, kila MTU ana mapungufu yake maana kiba naye kaumbwa kama binadamu yeyote .. Labda tukuulize wewe mtoa mada wewe umekamilika?? Tena inawezekana ikawa afadhali ya kiba kuliko ww ni vile tu hujulikan..Mkamilifu ni Mungu pekee
 
Kwa hiyo unataka Ali hawe na tabia za hovyo hovyo kama Dimond ndio umpende?!

Au unataka na yeye adhalilishe wanawake zake?!
 
Kama nakuona, unaandika huku unakohoa kohoa, acha fitina wewe.
 
Kiba kweli anajisikia sana
Alaf ukiangalia
Ni msanii wa kawaida sana sema tuuu ule ushindani na domo ndo unampush sana..

Ka alivyo ray na kanumba kipind kile.
Ray alikua wa kawaida sana sema ushindan ukawa unampandisha baada ya kanumba kufa ray saiv kapotea
 
umeandika point moja kubwa sana
 
Kuna video nyingine alikua anatembea mitaa ya Lumumba au Posta ile kuna mmachinga akamkimbilia kumsalimia alimpotezea kiroho mbaya ila jamaa akaforce
 
Sikupanga kusema kitu. Ila Kiba kweli hana ushirikiano na ata wasanii wenzake.

Angalia ata Instagram. Alikiba hajam-follow ata mtu mmoja. Ana followers Mil 3+ ila following 0.

Ok inaweza kua personal lakini wasanii wanatabia ya kutangazana ndio maana ukiona Mtu katoa wimbo, basi wenzie wanampa shavu kwa kusema Link on his/her bio.

Huyu jamaa waliomtangaza ni CMG peke yao ambao hakuna ata mmoja mwenye followers ata 1M.

Alikiba abadirike, ajaribu interact na wasanii wenzake basi maana sisi washabiki hawezi kabisa.
 
Mkuu umesahau kipindi cha show ya tigo music pale leaders ambapo jamaa alikataa kuwasalimia wasanii wenzake akiwemo mwana FA ambae walikuwa wamefanya nae kolabo ya kiboko yangu, alafu akamaliza akaruka ukuta akasepa
 
CMG wapo wenye 1m followers mkuu,usipotoshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…