Hahahaaaaa usinikumbushe hiyo zawadi kutoka kwa Mungu jamani nilikua nimeshasahau....
Duu naona ni mtifuano mkali hapa!
Mimi nahitaji wote Diamond na Alikiba waendelee kubaka kwenye peak na waendelee kuwapa burudani wanao wapenda!
Lakini tusikubali mmoja kati yao kuporomoka kimziki bali tuhakikishe wote hawapotei kwa kuwashauri chakufanya kwenye muziki wao na si kuwakatisha tamaa!
Mimi naamini kabisa Alikiba hajafurahishwa na kuzomewa kwa Diamond na wala Diamond hawezi kufurahi Kiba kuzomewa Bali huu ni mtifuano wa Mashabiki tuu!
Me ningependa zaidi ili jambo kama lingekuwa la kibiashara zaidi na Diamond na Kiba wakapiga hela ... unaonaje inaandaliwa live show ya Diamond na Kiba pale Leaders Club na kiingilio kinakuwa 20,000?
Sitegemei Diamond kukata tamaa kwaajili ya ile zomezomea au Kiba kubweteka kwaajili ya zile shangwe bali wote wanatakiwa kukaza buti!
Mimi huu upinzani wa Kiba na Diamond napenda uendelee ili uwape changa moto kwenye kuboresha muziki wao na wasibweteke lakini sipendi watu wafikie kutoana macho kisa D au A!
Mi nafikiri ni wakati kwa Alikiba kuji brand kama msanii kama mwenzie Diamond anavyo Fanya!
Kuanzia mavazi na hadi maandalizi kwenye show zake na wote waache play back!
.........
Nimepata nafasi ya kusikiliza wimbo mpya wa Mwana FA feat Alikiba -Kiboko yangu.
Hakika Alikiba ana sauti nzuri sana kapiga zinga la chorus...duuu hatari
kwani alivyosema amekuja kuchukua kiti chake alimpaga nani amshikie???
mi siwaelewi mbona daimond anadiscussiwa sana mi binafsi mara nyingi nyuzi specialy kumsifia dai huwa siingii maana staki niwaharibie pozi watu wake
asa na wao watuache hata kwa huu uzi
hatukatai dai ana mafanikio ya yake
na sie tuacheni tumshauri kiba
wao wanavyompromoti dai ina maana kibaya chajitembeza?
Ndio alete mapema,kweliii
kwani alivyosema amekuja kuchukua kiti chake alimpaga nani amshikie???
Umbea wa mkesha hata haunogi
Tulikificha stoo ndo kikapata na vumbi.....!!! Mana ndomo alikua anakililia sana!!! Alilia na mengi,akapatwa na mawazo,akajisifu kuwa yeye ni number one ivo tumpe kiti,akalalama eti tatizo kwao mbagala,akaondoka akasema atarejea,akanambia atanihonga Pete,nikamkatalia akasema eti moyo wake umemponza,akajamdogomdogo ili akiibe,lakini alivofika akangusha madumu yake tukaskia bum bum.... Toka hapo tukastukia tukamwambia mfalme njoo tunakuletea kiti chako......... Umeelewa kwenye kiti kilikuwa?????
mi siwaelewi mbona daimond anadiscussiwa sana mi binafsi mara nyingi nyuzi specialy kumsifia dai huwa siingii maana staki niwaharibie pozi watu wake
asa na wao watuache hata kwa huu uzi
hatukatai dai ana mafanikio ya yake
na sie tuacheni tumshauri kiba
wao wanavyompromoti dai ina maana kibaya chajitembeza?
Jamani,Ally K,nomer sana hakika yeye kioo cha jamii!mwanamme haswaa sio lazima mambo yake ya chumbani ayaweke hadharan!hapo tuuu nampendea!Misifa ya kijinga mara oo mara sijui nini yani hana!Hana shombo wala shobo!yani mimi penda sana yeye,atafute management na awe serious na kazi,achukulie mziki kama office atafanikiwa sana,tena asali sana,mganga wa yule domo asije akamchezea!
Watu hawaelewi unajua,hii sio team km za insta za kusapot bifu za kijinga,nadhani matola kaanzsha ili kumsapoti ally k kuzungumza yao,kujenga sio kutok blah blah km za insta,
Hahahaaaa aisee una akili sana dada...