Kwa mjadala ulioletwa na majirani zetu jana inaonesha wazi kwamba wana uelewa mdogo sana kuhusu tuzo hasa za vituo vya TV, kwa maana ya kutoa tuzo kwa video walizozipokea.
Lakini kwa ulimwengu wa sasa hali ni tofauti, kinachotazamwa zaidi na matokeo ya moja kwa moja ya mashabiki, ndio maana Adele aliweka rekodi kwa kutwaa Tuzo nyingi za Grammy kwa wimbo wa miaka ya 80 wa Van Morrison wa Someone like you ambao aliurudia.
Lakini hata hivyo, aliyeuza sana album ni Nicki Minaj ambaye pia alipata heshima kubwa kwa kuvunja rekodi ya Michael Jackson kwa kuwa na nyimbo nyingi kwenye chart ya Billboard.
Na ndio maana Davido ndiye msanii wa Nigeria aliyepata tuzo nyingi mwaka huu, lakini aliyeuza nakala nyingi za albamu yake ni 2 Face Idibia, na bado P Square ndio wanamuziki wanaopendwa zaidi Nigeria.
Kwa kawaida Tuzo za vituo vya TV zina sarakasi zake, kwanza timing ya kutoa wimbo kwa kalenda ya Tuzo za kituo husika, kuwafanya wa kwanza kupata wimbo wako na kuupiga kwa mara ya kwanza na mambo mengine.
Na ndio maana SA wanaona Tuzo za Channel O ni kama za kwao coz kituo kiko SA na Nigeria wanaona Tuzo za MTV Base ni kama zao kwa sababu kituo kiko Nigeria.
Pia, wanapaswa kuelewa kwamba Tuzo ni matokeo ya mambo yaliyopita na sio yaliyopo, na ndio maana Nassib kapata tuzo za wimbo ambao aliutoa kabla Gurumo hajafariki, tangu yuko na Penny.
Sasa kwa wakati huo Kiba hakuwa akifanya muziki, alikuwa katika kipindi chake cha miaka mitatu na nusu ya kupumzika.
Ova