Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

Asilimia kubwa ya wapenda burudani Afrika Mashariki kwa sasa wanazungumzia kuhusu ujio wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Kiba, maarufu kama Alikiba, kwa watu wanaojua historia ya Bongo Flava wanakumbuka kijana alikuwa tishio, kwani amekuwapo kwenye gemu tangu mwaka 2004 na kufanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimtambulisha uliojulikana kama Cinderella.

Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2004, alianza kujituma katika muziki na kufanikiwa kuandika wimbo wake wa kwanza, ‘Maria'. Mwaka huohuo Alikiba alianza kutengeneza albamu yake ya kwanza. Ilipofika mwaka 2005, alipata ofa ya kwenda kuchezea soka la kulipwa nchini Uganda, lakini baadaye aliachana na mpira ili kuendeleza kipaji chake cha muziki.

Mwaka 2007 alifanikiwa kuachia albamu iliyopewa jina la ‘Cinderela', sambamba na kuachia wimbo huo redioni, ambao ulivuma na kusababisha albam hiyo kuuzika zaidi sokoni. Albamu hiyo ilikuwa ni kati ya albamu bora na iliyouza zaidi mwaka 2007 Afrika Mashariki. Tangu hapo akaanza kupokea mialiko mingi kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi.

Aliifanya Afrika Mashariki kumjua kwa muda mfupi kupitia vibao kadhaa vilivyokuwepo katika albamu hiyo kama MacMuga, Nakshi Mrembo, Njiwa na Mali Yangu. 2008 Alikiba aliachia albamu ya pili ‘Alikiba 4 Real' na wimbo wa kwanza kuachia ulikuwa ‘Usiniseme' na wakati huu alikuwa ameshatangaza jina lake Afrika Mashariki na kwingineko.

Albamu hiyo ilimfanya aanze kuaminika zaidi, mwaka huohuo akateuliwa na kushinda tuzo za Kilimanjaro Music Awards kupitia wimbo wake wa Cinderella. Aliendelea kutafutwa kwa ajili ya kusakata kabumbu ambapo mwaka 2009, alipokea maombi kwa ajili ya kuichezea timu ya African Lyon ya Tanzania lakini alikataa na kuamua kuingia kwenye mitindo ambako hakukumchukulia muda mwingi.

Akutana na R Kelly;

Ilipofika mwaka 2010 ndipo alipopata dili la One 8 na kufanikiwa kufanya kazi na wanamuziki wa kimataifa akiwamo R Kelly na wengine saba kutoka Afrika. Alipokutana na R Kelly alimsifu kwamba ana sauti nzuri na ya kipekee, hivyo kupendekeza sauti yake iwe ya kwanza kuimba katika singo ya pamoja ‘Hands Across the World'.

Kupitia wimbo huo, mtandao maarufu wa kimuziki duniani Billboard walilitangaza kundi la One 8 kama "Best Bet of 2011" kupitia orodha ya nyimbo zao bora duniani. Mwaka huohuo Alikiba aliteuliwa na kushinda tuzo ya BEFFTA London Awards kama ‘Best International Artists' (ACT) na kumshinda mwanamuziki 2 Face Idibia. Pia alifanikiwa kurudi na tuzo ya Sexiest Male Artist.

Historia yake;

Alikiba alizaliwa Iringa Novemba 26, 1986 kutoka kwa mama yake Tombwe Njere na Saleh Omari. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wane katika familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba. Muziki ni kati ya vitu ambavyo zimekuwa vikipendwa na mwanamuziki huyu tangu utoto wake.

Kwa sasa Alikiba anatamba na wimbo wake wa Mwana alioutoa mwezi Julai 2014, kabla ya kutoa video yake Desemba 19, 2014. Ni moja video zake bora kabisa na inayotarajiwa kufanya vizuri Kimataifa. Huku ukiwa gumzo kwenye tovuti mbalimbali za kijamii na majukwaa ya mijadala.

Ova
 
video ilipotoka tu mpaka zile bwembwe za promo za white party ya UG zikawa haisikiki tena,haters wamepanic mno,
kuna mdau jana alisema video ikipata views laki moja anajiua now ni #63336 ndani ya siku mbili,matamko mengine ya kijinga sana,mtu katulia ili wasanii wapya nao wapate nafasi wasikike halafu anakuja kuwafunika tena.
Ninachosubiri kiba afanye colabo za nguvu now na wasanii wa nje na asiwe anachelewesha video zako
 
Binafsi namkubali sana Alikiba tangu nimeanza kumuona kwenye nyimbo ya SIKUONI napenda vile anavobadilika na kutupa radha tofauti tofauti za muziki.
He's keeping it real mazee!
 
Watu wengi sana husoma trends humu ndani (JF) bila ku-comment na mi ni miongoni mwao. Braza Mdakuzi napenda sana uandishi wako wa hekima.

Napenda ujio wa king alikiba. Tulikua tumekosa vitu adimu, vitamu kutoka kwake.

Mi nipo kenya. We waona Kwanini alikiba alikua msanii pekeyake aliyekuwa searched Mwaka huu 2014 kushinda msanii yoyote yule nchini kenya? We love him more than he thinks!!!

Thanks
 
Last edited by a moderator:
Binafsi namkubali sana Alikiba tangu nimeanza kumuona kwenye nyimbo ya SIKUONI napenda vile anavobadilika na kutupa radha tofauti tofauti za muziki.
He's keeping it real mazee!

Kila shabiki wa kweli wa muziki, ni ngumu sana kutomwelewa Kiba. Mungu amempa kipaji kikubwa sana kwa kweli, na sauti nzuri, anajua kuimba na anajua sana kuandika. Lakini kama uko kwenye muziki kwa ajili ya kupenda watu tu, basi huwezi mwelewa. Ndio mashabiki wa muziki tunamwelewa sana.
Hata kama ikiwa humpendi, lakini Mungu ameshampa kipaji hicho na hutaweza mnyang'anya hadi atakapoingia kaburini. Nimesoma comments za watu wa nchi jirani kwenye majukwaa wanawashangaa sana Watanzania kwa kuponda video ya Mwana. Tunaonekana watu wa ajabu sana.
Ova
 
video ilipotoka tu mpaka zile bwembwe za promo za white party ya UG zikawa haisikiki tena,haters wamepanic mno,
kuna mdau jana alisema video ikipata views laki moja anajiua now ni #63336 ndani ya siku mbili,matamko mengine ya kijinga sana,mtu katulia ili wasanii wapya nao wapate nafasi wasikike halafu anakuja kuwafunika tena.
Ninachosubiri kiba afanye colabo za nguvu now na wasanii wa nje na asiwe anachelewesha video zako

Kiba ujio wake mpya umefana saaana kwaivo asiache kujitendea haki.
 
Binafsi namkubali sana Alikiba tangu nimeanza kumuona kwenye nyimbo ya SIKUONI napenda vile anavobadilika na kutupa radha tofauti tofauti za muziki.
He's keeping it real mazee!
mi huo wimbo wa sikuoni huwa ndo naupenda sana,chorus kaimba vizuri halafu aliyemshirika naye alikuwa vizuri
 
Watu wengi sana husoma trends humu ndani (JF) bila ku-comment na mi ni miongoni mwao. Braza Mdakuzi napenda sana uandishi wako wa hekima.

Napenda ujio wa king alikiba. Tulikua tumekosa vitu adimu, vitamu kutoka kwake.

Mi nipo kenya. We waona Kwanini alikiba alikua msanii pekeyake aliyekuwa searched Mwaka huu 2014 kushinda msanii yoyote yule nchini kenya? We love him more than he thinks!!!

Thanks

Asante sana ndugu yangu. Najua mnavyojivunia talents za wana wa East Africa, mapema nimepitia majukwaa yenu kule nimeshangaa mnavyokubali video ya Mwana, lakini majukwaa ya hapa nyumbani kwake Kiba kuna vita ya kuiponda video, hadi jukwaa limechafuliwa kabisa.
Nafurahi sana kwa kunipongeza hadharani, itanisaidia sana kuhakikisha kwamba siipotezi pongezi hii kwa kuanza kutukana watu au kugombana na watu hapa jukwaani, nilizoea kupokea PM tu za wanajukwaa kunipongeza kwa uandishi, lakini leo nimepata ya hapa hadharani, asante sana.

shukran sana. Kiukweli JF ingekua ya-bore mkikosekana watu wenye ushawishi na hekima katika uandishi kama wewe. #loveJF #lovealikiba .
 
video ilipotoka tu mpaka zile bwembwe za promo za white party ya UG zikawa haisikiki tena,haters wamepanic mno,
kuna mdau jana alisema video ikipata views laki moja anajiua now ni #63336 ndani ya siku mbili,matamko mengine ya kijinga sana,mtu katulia ili wasanii wapya nao wapate nafasi wasikike halafu anakuja kuwafunika tena.
Ninachosubiri kiba afanye colabo za nguvu now na wasanii wa nje na asiwe anachelewesha video zako
Mwacheni apumzike Kiba muda wake ilishaisha msimlazimishe kushindana wati mwenyewe alishakubali kushundwa.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Ndugu.....tulieni.....kama kiba anapendeka.....anapendeka tu. Kama hana ushawishi tena...pia sio ajabu. Nani asomjua P. Funk majani enzi zake....lakini Leo tuzo za maproduzer bora znaenda kwingineeeeee. Mpaka Leo mm naamini ndo produzer bora ila This thing we call DESTINY,hahhaaaaa. Iam speech less.
 
Nampenda sana Ali Saleh Kiba kutokana na mziki wake mzuri,sauti yake na hasa utunzi wake makini katika tungo zake mbalimbali mfano mzuri ni huu wimbo wake wa mwana unaotamba kwa sasa.
Video yake aliyoiachia jana ni nzuri sana,nimeipenda.
Ushauri wangu kwa Kiba,yeye ni msanii mkubwa sana,anatakiwa abadilike afanye mambo makubwa kama lilivyo jina lake.Asifanye mziki kwa mazoea kisa ana kipaji kikubwa.Aijue thamani yake sasa maana nakumbuka aliwahi kusema kua amekua surprised kwa mashabiki wake kumuulizia hadi walitaka kufanya maandamano japo alikaa kimya kwa zaidi ya miaka miwili!

Pia Kiba fans wenzangu huu ndio wakati wa kumsapoti Kiba,yeye kaonesha juhudi na sisi hatuna budi kumsapoti katika mziki wake ili naye apate mafanikio kulingana na kipaji chake kikubwa ambacho kiukweli hakiendani na mafanikio yake kimuziki.
 
Back
Top Bottom