Dah! Jamaa utakuwa unanikubali sana, yaani kwa kuandika hivyo tu umeona nimetumia akili nyingi sana. Asante kwa kunikubali, lakini ukweli wala sikutumia akili nyingi, kwani wakati naandika hiyo ndo nilikuwa nimetoka kulala.
Kwa huku niliko niliiandika saa 8 usiku, after kupokea Simu ya familia na kuzungumza nayo. Huwa natumia akili nyingi kwa kazi zilizonileta huku, kwangu muziki ni burudani tu kama ilivyo soka.
Ukweli upi uliopindishwa? Kwamba maelezo yangu yamesema Nassib hakupata tuzo? Si kweli kwamba studio kuu ya Channel O iko SA? Si kweli kwamba studio kuu ya MTV Base iko Nigeria? Si kweli kwamba CHOAMVA ni Tuzo za kituo cha TV?
Kwa taarifa yako Tuzo zina sarakasi nyingi sana, unajua kama Kanye West aliwahi kupanda ghafla jukwaani na kuponda Beyonce kunyimwa Tuzo aliyokuwa akiwania na Taylor Swift? Yote hiyo ni kwa sababu ya sarakasi za Tuzo.
Matola kakueleza kwamba Westside Connection walikuwa wakali watupu na walitoa nyimbo kali tupu na hawakuwahi kupata tuzo?
Ova