Ali kiba kajiandae vs Diamond kokoro

Ali kiba kajiandae vs Diamond kokoro

Njia je?..pita njia za kiba uchanike koo Hahahaaaa kambaaaaf
Usipende kutukana tukana kama huna hoja hujalazimishwa kuni quote......

Kutukana ni ishara tosha ya kuonyesha ni jinsi gani ulivo mweupe kichwani
 
Hiyo mistari ya Ali Kiba unasikiliza hata ukiwa na wazee,huyo mwingine hakuna kitu aibu tupu.

Na hii inadhihirisha kiwango cha busara baina yao.
Period
Amina mtumishi amina sanasana.
 
Hao wazee kuna nyimbo za Sikinde "Ngoma ya ukae" pia DDC Mlimani zinawafaa sana tutawapa wasikilize ila hapo ukiangalia kiuandishi Diamomd ameonekana yupo vizuri zaidi ya Kiba ila mkijifanya hamuoni na hamuelewi na sisi tunajifanya tunaona na kuelewa yetu.Kuna nyimbo kama Nitarejea,Mbagala nk unaweza ukasikiliza na wazee pia
kuna shairi linaitwa "Mfereji Maringo" limeandikwa na Theobald Mvungi katika kitabu cha Chungu Tamu na wanafundishwa wanafunzi mashuleni na wazee hao hao wanasahihisha mitihani.
[HASHTAG]#kwanianjematu[/HASHTAG]
ALIKIBA hakuna nyimbo au video yake ambayo ikipigwa huku upo sebulen na wazaz wako itabid uindoke au ubadili Chanel siyo huyo Mtandale hakawii kuvua nguo hahahaaaa...
 
Hujanya umeharaaa...uandishi barnaba ,bele,Ali kiba unawaacha wapi?..naona anakunyakunya tu hapo hamna kitu.
Embu nakuomba ukazie macho kwenye uzi ulipoanzia na sio kuleta ushabiki wa kijinga,hapo umeona wapi ameandikwa Belle 9 au huyo Barnaba.Zimewekwa pande mbili,mistari ya Ali Kiba na Diamond na mimi nikaelezea Diamond yupo vizuri kwa vigezo vyangu sasa wewe unakuja kimagurue unaanza kuandika mambo ya ajabu.Kama Ali Kiba ni zaidi kiuandishi onesha ukirejea hayo aliyoandika mleta mada na huku ukizingatia vigezo.Kama utashindwa na kuleta blah! blah! zingine itamaanisha wewe ni mmojawapo ya nyani watiifu wa mfalme nyani.
 
ALIKIBA hakuna nyimbo au video yake ambayo ikipigwa huku upo sebulen na wazaz wako itabid uindoke au ubadili Chanel siyo huyo Mtandale hakawii kuvua nguo hahahaaaa...
Acha kuwadharalilisha wazazi wako.Sasa huo wa muda wa kukaa na kuangalia tv na wazazi wako kwanini usiutumie kujadili mambo ya familia au kwanini wadogo zako wanafeli na kumtajataja Diamond tu kuliko kutumia nguvu kushika remote control na kusubiri nyimbo za Diamond zikipigwa wewe ubadilishe channel......eti! Kumbuka hakuna sehemu Diamond aliyoandika kuwa ni lazima ufuatilie nyimbo zake,sasa kwanini unajichosha?
 
mjadala huu hautaleta maana kama hakutawekwa vigezo vya kujua nani mshindi;

Mfano: Ujumbe mzima wa muziki husika... Hauwezi kuweka mashairi ya mapenzi kwenye wimbo wa kuomboleza
Ujumbe wa mashairi husika wa msanii.... Ikilinganishwa na kusudio la wimbo.
Mpangilio wa mashairi kwa kuzingatia vina vya urari na mizani.
Utumiani wa maneno.
Sauti za wasanii.

sasa kabla hatujatoa mshindi yawekwe masharti tutayotumia kupata mshindi.
 
Mashairi yasiyo na vina pia yanaruhusiwa katika utunzi, huo huitwa utunzi wa kimapokeo. Hivyo naona wote wako sahihi tuu. [emoji117][emoji117][emoji126][emoji126]
 
Guys 2ache uxhabiki.....platinumz n moto Wa kuotea mbal
 
Diamond sijui anaimba vitu gani siku hizi..

Nyimbo zake ni tungo za kufanana na matusi tu!

Tangu atoe ule wimbo unaelezea maisha yake mara atakapifilisika hakuwahi kutoa wimbo wenye nidhamu tena!

Sijui labda ndio soko linavyotaka!
 
Back
Top Bottom