Uandishi wa makala za kuwachambua Ali kiba na diamond umepitwa na wakati
Kwa sababu mashabiki wa pande zote mbili wanajua uzuri na ubaya wa msanii wanao mshabikia na ndo mana diamond hata akukuruke vp afanye collabo hata na Beyonce hawezi kumfanya shabiki wa kiba kuwa wake mfano kila mtu anauona kupitia mafanikio yake na collabo zake lkn bado mashabiki wa kiba wanaongezeka
Hali kadhalika kwa kiba nae sauti yake hata iwe nzuri kiasi gani bado hawezi kumfanya shabiki wa diamond kuwa wake mfano mzuri tunauona kiba alivyotulia akiwa na live band lkn bado mashabiki kwa diamond wanaongezeka
Makala hizi zinalenga tu kutengeneza civil war kwa mujibu wa koment zilizopo kwenye huu uzi,ni makala ya kutaka kummweka mmoja juu sana zaidi ya mwingine au kumfanya mmoja kati ya hawa aonekane hajui,wanaijeria wenyewe hawakosi usingizi kipindi cha MTV awards kikifika wanajua kule kuna yemi alade,davido,tekno,star boy mwenyewe,tiwa savage na wengine wengi so tuzo lazma zije Lagos na ndo mana kila category lazma ukute wanigeria wa2 au wa3 au category zingine utakuta tu wenyewe,lkn hapa watu hawalali kumfanyia upatu mtu mmoja wakiona mwingine zaidi ya huyo mmoja yupo kwenye tuzo za mtv basi watamponda km vile huyo mtu ni mkimbizi kutoka burundi kumbe ni mtz mwenzetu tu
Kwa hiyo haya maswala mara nyingi yanapotupiwa maeneo km haya yanalenga zaidi ushabiki na si vingine