Ali Kiba ni msanii anayekuzwa kuliko uwezo wake (Overrated)

Kwaiyo Mr Judge una hisi promotion ndo inayomuangusha kiba mbona zaman ngoma zke zilikuwa zinapenya je zaman tuseme alikuwa anajua ku promote kazi zke au tuseme zama zimebadilika uku yeye akiendelea kutumia strategey ya promotion ya zaman.?
 

Hilo la promotion hata mimi kuna mdada mmoja nilikutana naye Iringa nikamwambia hivyo hivyo.

[Kiba] Anaonekana yuko passive kiaina....almost nonchalant.

Na nikaongeza kwamba, relatively speaking pia hana charisma....mtaani huitwa nyota.

Lakini talent wise, dogo anawaacha wengi sana nyuma.
 
Kwaiyo Mr Judge una hisi promotion ndo inayomuangusha kiba mbona zaman ngoma zke zilikuwa zinapenya je zaman tuseme alikuwa anajua ku promote kazi zke au tuseme zama zimebadilika uku yeye akiendelea kutumia strategey ya promotion ya zaman.?
Waswahili walisema "Kipya kinyemi, japo kidonda".

Unapoanza jina jipya ukitoa kitu kizuri una hit halafu watu wana mshawasha wa kukujua zaidi kwa sababu jina jipya.

Lakini kadiri siku zinavyozidi, inabidi ufanye kitu Waingereza wanasema "reinvent yourself" kila siku uwe magazetini. Ukiangalia kina Michael Jackson, Madonna,Prince, Fela Kuti, Bob Marley utakuta wote walikuwa kwenye headlines constantly. Ama kwa deliberate promotion au kwa lifestyles zao tu. Ukiwa mwanamuziki unakuwa bidhaa. Unauza mpaka image yako na habari ya maisha yako.

Ali Kiba hataki kufanya hivyo. Anataka kuishia kwenye muziki tu.

Ndiyo maana utasikia mara Diamond anamfanyia mtoto birthday, mara hiki, mara kile, mara Diamond kaanza ku sign wanamuziki kwenye Wasafi etc. Hayo yote ni mazuri kumkeep mtu kwenye headlines na kumkuza kibiashara. Lakini ukiongelea muziki kama muziki hayo si lazima.

Diamond na wengine wanajitahidi kufanya promotion. Ali Kiba anafanya muziki.
 
Kwakuwa nimeona comments zenye akili subiri nitie neno. ..unajua promo kibongobongo ni kuwatisha watu kimafanikio kitu ambacho kiba hafanyi...vijana wengi wakipiga pesa watazipost au mali zao hapo huyo msanii ataongelewa. ..mfano hivi majuzi kiba kavuta dollar 25,000 kufanya tu collabo na mkenya hiyo ni audio tu. .staki kusema atavuta kiasi gani katika video. ..ndivyo alivyo si kiki seeker ila mziki unamlipa kuliko wadhaniavyo wengi kachagua tu njia za kifaza flani which is good
 
TEam wema, team tiffah, team zari, huko insta hapa maendeleo.... Angalia mbele,... jenge uchumi akusaidie kulipa kodi
 
Kama ni hivyo fananisheni nyimbo Zake za zamani na za sasa.

Msimlinganishe na Diamond maana wote wana style tofauti za uimbaji.
Mkuu umeongea point kabisa, watu wanawafananisha hawa watu lakn hawajui kwamba style yao ya uimbaji ni tofauti kabisa
 
Ali Kiba ni msanii mzuri tu kama walivyo wengine. Lakini huwezi kumlinganisha na Mondi. Mwanamuziki hapimwi kwa maneno tu ya nyimbo. Ni vitu vingi ambavyo vinamfanya Mondi ashindwe hata kumtimulia vumbi Kiba kwa kuwa Kiba yupo mbali sana nyuma kiasi kwamba hata vumbi la Mondi halioni.
 
Mmh bila ya aibu unamuita D'mond mwanamuziki?
 
Kwa hits zipi jamani?
Hizi habari za vijiweni unataka kuleta huku sasa.
Mambo ya Salome sijui Handsome utamletea nani kwa sasa?
Yani sasa hivi hata unipigie Dhahabu ambayo kwangu mimi ndio track kali zaidi ya Dully sishtuki.
Wewe ndio hustuki.
 
Asante Kiranga [emoji8] [emoji122]
 

Huyu jamaa anapenda ligi kweli kweli majuzi alikuja na bandiko lake Arusha si lolote ni overrated bado hajaja na lingine mke wangu si mzuri ni overrated.Haaa haaa anataka kutuambia anachokione kizuri yeye ni lazima kwa wengine ni kizuri pia.
 
kusema ukweli bongo ndo maana hatuendelei hakuna msema kweli kila kitu ni kujadili utadhan siasa ingawa na siasa ni zero tangia alikiba atoe muziki mmoja tu ndo kapatia video ile alotoa majuz lakin uteam ndo umetujaa na watu walivyo jifunza kuedit picha ndo bas yaan nlishaangaa sana kumpa alikiba tuzo ya wimbo bora wa mwaka wakati maudhui hayalingan na wimbo wa ben pol jikubali wakampa mtumbuizaji bora angalau wangempa mensen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…