Alichoandika Amri Kiemba kwa Msemaji wa Simba Ahmed Ali juu ya Lameck Lawi

Alichoandika Amri Kiemba kwa Msemaji wa Simba Ahmed Ali juu ya Lameck Lawi

Mwanamichezo mstaafu na mchambuzi wa michezo Amri Kiemba ameandika maoni ambayo yamenifanya niwaze na kukaa chini kutafakari juu ya kauli na maneno ya msemaji ambayo kila siku yanazidi kushangaza na kumshushia tu Professional wake.

AMRI KIEMBA ANAANDIKA:

Kuna vitu unaweza kuviangalia halafu ukatafakari kisha ukacheka ukajiuliza kwa nini Msemaji wa moja ya Klabu Kongwe nchini anababaisha?

Wote tunajua Lameck Lawi kaenda Ubelgiji kwa ajili ya kutafuta malisho bora ya maisha yake ya soka, kuna stori za kuwa alikuwa anaenda kusajiliwa moja kwa moja KAA Gent ndio hata sababu ya Coastal kurudisha pesa za Simba SC na kuna stori kuwa baada ya kufika alitakiwa kufanya majaribio na timu za vijana kitu ambacho sio kibaya.

Mchezaji kutoka katika kituo chake cha kazi kwenda nje ya nchi kwa timu nyingine kusajiliwa, kufanya majaribio hilo sio suala lake binafsi ni suala rasmi la Klabu.

Msemaji anamkosea sana Lameck Lawi kauli hizi na kama ni kweli hajafuzu majaribio unamfanya kijana ahisi kama amefeli maisha baadala ya kuongea ukwelii tu mambo hayajaenda sawa na kumpa moyo, unaamua kubabaisha, Lawi ana jambo gani binafsi Ubelgiji ambalo alisemeki? mke kajifungua? Familia au mtoto?

Ni vyema tujifunze kutoa habari za kweli au kuachana na kuzungumzia jambo kama hamko tayari kutoa taarifa za ukweli kwa hadhara.

Mwisho kufeli majaribio sio dhambi na wala haina maana huwezi kuinuka au kufika mbali.

Yaya Toure amewahi kufeli majaribio ya kujiunga na Arsenal na miaka baadae alikuja kuwa sio tu Mchezaji wa Man City bali Mchezaji anayelipwa zaidi EPL.

Ipo mifano mingi sana ila Lawi hupaswi kuvunjika moyo rudi home ujipange au tafuta timu nyingine.

Nadhani hujaelewa.... kiemba anamsiliba msemaji wa coastal union waala sio ahmed ally. Fatilia Instagram yake vizuri utaona nani kamuweka ktk video aliyoitolea maoni
 
Tuliambiwa kwamba Lawi imeshindikana kusajiriwa Simba kwa Sababu anatakiwa na timu Moja huko Ulaya, kwamba anaenda kucheza huko na kwamba Coastal Union wameshapewa pesa za kumnunua Lawi na hiyo Timu ya Ulaya.... Na hii ikawapa kiburi Coastal mpaka wakaivimbia Simba....

Sasa haya mambo kwamba ameenda kufanya majaribio yanatoka wapi tena?..... Si mlisema ameenda kusajiriwa?????
Hakuna mwenye tahaarifa kamili, kwani ni lazima sana kila mchezaji acheze bongo ?

Tuache lamli chonganishi.
 
Aliyehojiwa mwingine na anayesemwa mwingine hapa Watanzania tuache uchonganishi hata kama mtu humpendi lini Ahmed ameongelea swala la Lawi
 
Kwahyo semaji la caf linafurahia kufeli kwa lawi kisa2 aliwakataa ubaya ubwela? Duuu!! Kweli ngozi nyeusi Bado hatujitambui
Uyo alieleta andiko anataka kutudanganya amri kiemba kamsema msemaji wa cost wala sio ahmed kwenye ilo andiko aliambatanusha na video
 
Nadhani hujaelewa.... kiemba anamsiliba msemaji wa coastal union waala sio ahmed ally. Fatilia Instagram yake vizuri utaona nani kamuweka ktk video aliyoitolea maoni
Kwaiyi msemaji wa Coastal ndio kafurahia Lawi kushindwa Ulaya,,Hujaelewa wewe mzee
 
Uyo alieleta andiko anataka kutudanganya amri kiemba kamsema msemaji wa cost wala sio ahmed kwenye ilo andiko aliambatanusha na video
Kwaiyo wewe ulichoelewa ni kuwa Msemaji wa Coastal ndio anafurahia kuhusu kushindwa kwa Lawi uko Ulaya ?
 
Sema msemaji uwa anatereza sana kwenye kauli zake na inabidi ajitahidi kujitafakari na kuchunga ulimi wake maana anabeba watu wengi nyuma yake asa mashabiki wa Simba na wanamichezo kwa ujumla
Jifunze kuandika.
Alitereza = Aliteleza
Asa = Hasa
Uwa = Huwa
 
Ni kweli ilikuwa asajiriwe baada ya majaribio lakini ameshindwa kufikia ayo kwaiyo saivi anafanya majaribio timu nyingine. Na pia iyo haihalalishi kwa msemaji kumuongelea kauli izo kwa mchezaji mdogo ambae ana ndoto kubwa kwenye michezo
Ayo = Hayo
Kwaiyo = Kwahiyo
Iyo = Hiyo
Kazi kushabikia ujinga tu ila kujifunza kuandika hutaki!
 
Hakuna mwenye tahaarifa kamili, kwani ni lazima sana kila mchezaji acheze bongo ?

Tuache lamli chonganishi.
Kwani wewe taarifa za Lawi kwenda Ulaya ulizipataje? Na kwamba kaenda kufanya Nini?... Au unajizima data mkurugenzi?
 
Ni kweli ilikuwa asajiriwe baada ya majaribio lakini ameshindwa kufikia ayo kwaiyo saivi anafanya majaribio timu nyingine. Na pia iyo haihalalishi kwa msemaji kumuongelea kauli izo kwa mchezaji mdogo ambae ana ndoto kubwa kwenye michezo
Sasa mkuu Coastal wanasemaje walimuuza na ilhali walijua kabisa anaenda kufanya testing????.... Nachojua timu haiwezi kununua mchezaji wa majaribio.....
Au wewe unasemaje mkuu?
 
Huyu Kiemba nae simuelewi, kwani Lawi wakati ana sign Simba alikuwa anafikiria kitu gani?

Kama alijua ana mpango wa kwenda Ulaya kwa majaribio kwanini hakuwaambia Simba mapema?

Kiemba hajui maana ya critical thinking, badala ya kulaumu chanzo cha tatizo, yeye analaumu matokeo ya tatizo, na wote mnaomuunga mkono kwa ujinga alioongea hamna akili pia.
 
Tuliambiwa kwamba Lawi imeshindikana kusajiriwa Simba kwa Sababu anatakiwa na timu Moja huko Ulaya, kwamba anaenda kucheza huko na kwamba Coastal Union wameshapewa pesa za kumnunua Lawi na hiyo Timu ya Ulaya.... Na hii ikawapa kiburi Coastal mpaka wakaivimbia Simba....

Sasa haya mambo kwamba ameenda kufanya majaribio yanatoka wapi tena?..... Si mlisema ameenda kusajiriwa?????
Ungekua wewe ungeacha kwenda kufanya trial Europe ili ucheze Simba?
 
Yan kiemba anajikutaga yeye alikuwaga mchezaji mkubwa kumbe marasta yanamdanganya kila kitu much know
 
Sasa mkuu Coastal wanasemaje walimuuza na ilhali walijua kabisa anaenda kufanya testing????.... Nachojua timu haiwezi kununua mchezaji wa majaribio.....
Au wewe unasemaje mkuu?
Elewa ili kuwa Coastal walipata ofa nono ya moja kwa moja ulaya endapo atafuzu majaribio na iyo timu ikalipia gharama zote za usafiri Pamoja na maradhi kwaiyo kwa hali iyo walikuwa na matumaini ulaya kuliko kwenda Simba kwa dau dogo la unyonyaji,, Kwenye Football iyo ipo sana na ndio walivyotoa taarifa.
 
Back
Top Bottom