Alichoandika Amri Kiemba kwa Msemaji wa Simba Ahmed Ali juu ya Lameck Lawi

Mwanamichezo mstaafu na mchambuzi wa michezo Amri Kiemba ameandika maoni ambayo yamenifanya niwaze na kukaa chini kutafakari juu ya kauli na maneno ya msemaji ambayo kila siku yanazidi kushangaza na kumshushia tu Professional wake.

AMRI KIEMBA ANAANDIKA:

Kuna vitu unaweza kuviangalia halafu ukatafakari kisha ukacheka ukajiuliza kwa nini Msemaji wa moja ya Klabu Kongwe nchini anababaisha?

Wote tunajua Lameck Lawi kaenda Ubelgiji kwa ajili ya kutafuta malisho bora ya maisha yake ya soka, kuna stori za kuwa alikuwa anaenda kusajiliwa moja kwa moja KAA Gent ndio hata sababu ya Coastal kurudisha pesa za Simba SC na kuna stori kuwa baada ya kufika alitakiwa kufanya majaribio na timu za vijana kitu ambacho sio kibaya.

Mchezaji kutoka katika kituo chake cha kazi kwenda nje ya nchi kwa timu nyingine kusajiliwa, kufanya majaribio hilo sio suala lake binafsi ni suala rasmi la Klabu.

Msemaji anamkosea sana Lameck Lawi kauli hizi na kama ni kweli hajafuzu majaribio unamfanya kijana ahisi kama amefeli maisha baadala ya kuongea ukwelii tu mambo hayajaenda sawa na kumpa moyo, unaamua kubabaisha, Lawi ana jambo gani binafsi Ubelgiji ambalo alisemeki? mke kajifungua? Familia au mtoto?

Ni vyema tujifunze kutoa habari za kweli au kuachana na kuzungumzia jambo kama hamko tayari kutoa taarifa za ukweli kwa hadhara.

Mwisho kufeli majaribio sio dhambi na wala haina maana huwezi kuinuka au kufika mbali.

Yaya Toure amewahi kufeli majaribio ya kujiunga na Arsenal na miaka baadae alikuja kuwa sio tu Mchezaji wa Man City bali Mchezaji anayelipwa zaidi EPL.

Ipo mifano mingi sana ila Lawi hupaswi kuvunjika moyo rudi home ujipange au tafuta timu nyingine.

Well said...wahusika somo wamelipata
 
Bado anaendelea kufanya majaribio katika klabu kadhaa za ulaya na tumuombe afanikiwe maana ni mchezaji mzuri wa kupeperusha bendera ya nchi
Sina shaka wewe ni UTOPOLO PLUS!
Chukulia, umeposa sehemu, na kutoa sehemu ya mahali. Ghafra, unarudishiwa hiyo mahali, sababu kuu, kapata BWANA MWINGINE! Yamshinde kule, na kutakiwa kurudi kwao, wewe UTASIKITIKAAA!?
 
Weka hoja yako kama mdau wa michezo na ondoa ushabiki
 
Mwanamichezo mstaafu na mchambuzi wa michezo Amri Kiemba ameandika maoni ambayo yamenifanya niwaze na kukaa chini kutafakari juu ya kauli na maneno ya msemaji ambayo kila siku yanazidi kushangaza na kumshushia tu Professional wake.

AMRI KIEMBA ANAANDIKA:

Kuna vitu unaweza kuviangalia halafu ukatafakari kisha ukacheka ukajiuliza kwa nini Msemaji wa moja ya Klabu Kongwe nchini anababaisha?

Wote tunajua Lameck Lawi kaenda Ubelgiji kwa ajili ya kutafuta malisho bora ya maisha yake ya soka, kuna stori za kuwa alikuwa anaenda kusajiliwa moja kwa moja KAA Gent ndio hata sababu ya Coastal kurudisha pesa za Simba SC na kuna stori kuwa baada ya kufika alitakiwa kufanya majaribio na timu za vijana kitu ambacho sio kibaya.

Mchezaji kutoka katika kituo chake cha kazi kwenda nje ya nchi kwa timu nyingine kusajiliwa, kufanya majaribio hilo sio suala lake binafsi ni suala rasmi la Klabu.

Msemaji anamkosea sana Lameck Lawi kauli hizi na kama ni kweli hajafuzu majaribio unamfanya kijana ahisi kama amefeli maisha baadala ya kuongea ukwelii tu mambo hayajaenda sawa na kumpa moyo, unaamua kubabaisha, Lawi ana jambo gani binafsi Ubelgiji ambalo alisemeki? mke kajifungua? Familia au mtoto?

Ni vyema tujifunze kutoa habari za kweli au kuachana na kuzungumzia jambo kama hamko tayari kutoa taarifa za ukweli kwa hadhara.

Mwisho kufeli majaribio sio dhambi na wala haina maana huwezi kuinuka au kufika mbali.

Yaya Toure amewahi kufeli majaribio ya kujiunga na Arsenal na miaka baadae alikuja kuwa sio tu Mchezaji wa Man City bali Mchezaji anayelipwa zaidi EPL.

Ipo mifano mingi sana ila Lawi hupaswi kuvunjika moyo rudi home ujipange au tafuta timu nyingine.

Binafsi, naona kama Lawi ni beki wa kawaida Sana, ila ni mtu mwenye juhudi. Hana skills za kibeki let's say labda Kama za Ibra bacca au Job.

Lawi Hana tofauti na kina Abdulmajik Mangalo wa Singida au Makame.

Watu wake wa karibu wamempaisha Sana kiasi kwamba ameanza kyjiona Bongo bahati mbaya.

Akili za Lawi zimekuwa Kama za George Mpole ambaye baada ya kupata Top scorer akajiona bongo bahati mbaya, na kukimbilia kucheza Congo, ambako ni Bora tu angecheza NBC. Na Sasa hivi anacheza Pamba Jiji eti anasikilizia ofa kubwa.

Tuwaambie wachezaji wetu ukweli, maana umri wao pia ni mkbwa, umri wa mchongo wa kwenye passport usiwadanganye
 
Ni kweli kama utalinganisha na hao uliowataja lakini kama unafuatilia ligi kuu ya NBC unaweza ona kuwa msimu uliopita Lameck Lawi amekuwa beki mzuri sana ukiwaondoa wa timu kubwa na mwenye umri wake pamoja na beki mzawa, kwaiyo nafikiri juhudi zake na kujituma ndio zimemletea matokeo ya kuhitajika na klabu kubwa ya Simba Sports Club pamoja kupata ofa kadhaa toka ulaya kwa majaribio. Nakwambia muda mwingine juhudi na bidii ushinda kipaji.
 
Ni kweli kama utalinganisha na hao uliowataja lakini kama unafuatilia ligi kuu ya NBC unaweza ona kuwa msimu uliopita Lameck Lawi amekuwa beki mzuri sana ukiwaondoa wa timu kubwa na mwenye umri wake
Umri tusidanganyane bana. Hapa tunajenga hatuharibiani. Lawi Hana miaka 18.

Binafsi, ni shabiki wa Yanga lakini kwa Mzize huwa nasema ukweli. Anapaswa kuwa na juhudi kunwa kufanya improvement kwasababu ndio wakati huu, kuliko kuishi kwa matumaini ya kuwa umri wake bado mdogo, anakuwa wakati kiuhalisia umri wake siyo mdogo hivyo.
pamoja na beki mzawa, kwaiyo nafikiri juhudi zake na kujituma ndio zimemletea matokeo ya kuhitajika na klabu kubwa ya Simba Sports Club pamoja kupata ofa kadhaa toka ulaya kwa majaribio. Nakwambia muda mwingine juhudi na bidii ushinda kipaji.
Kwa Simba na beki mzawa ni Jambo zuri. Ila Ulaya sidhani kama alipata ofa, watu wake siyo wakweli. Itakuwa alialikwa kufanya majaribio ndio maana baada ya Gent, kaalikwa tena Sweden.

Sioni kama Coaster walipata ofa ya Ulaya
 
Back
Top Bottom