Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Makwizi...
Nakushauri usome kitabu cha Abdul Sykes.
Sykes aliunda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Vyama viwili tofauti malengo tofauti ingawa kuna wakati President African Association alikuwa Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Abdallah Sykes na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika President Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Abdallah Sykes.

Vyama viwili tofauti lakini viongozi ni walewale.
Hii hstoria ilipowekwa hadharani watu walishtuka.

Hawa mimi babu zangu si "brother" historia hii ni historia ya nyumbani kwetu.

View attachment 3316503
Kulia Kleist Sykes na Mzee bin Sudi
Baba, mimi naandika kulingana na ulicho jibu wewe mwenyewe, situngi kutoka kichwani mwangu; in other words wewe mzee wangu ndio unanitengenezea maswali. Jioni njema baba, enjoy your pension, wanao bado tunapambana tufikie ndoto zetu
 
Baba, mimi naandika kulingana na ulicho jibu wewe mwenyewe, situngi kutoka kichwani mwangu; in other words wewe mzee wangu ndio unanitengenezea maswali. Jioni njema baba, enjoy your pension, wanao bado tunapambana tufikie ndoto zetu
Niulize chochote katika historia ya Nyerere na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Maktaba yangu ni ya pili kwa nyaraka za Nyerere.

Maktaba ya kwanza ni ya Dr. Salim Ahmed Salim ya tatu ni ya Brig. General Hashim Mbita.

1745689477299.png

Nyaraka za Brig. General Hashim Mbita
1745689532719.jpeg

Na Salim Ahmed Salim nyumbani kwake Masaki.
 
Niulize chochote katika historia ya Nyerere na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Maktaba yangu ni ya pili kwa nyaraka za Nyerere.

Maktaba ya kwanza ni ya Dr. Salim Ahmed Salim ya tatu ni ya Brig. General Hashim Mbita.

View attachment 3316665
Nyaraka za Brig. General Hashim Mbita
View attachment 3316667
Na Salim nyumbani kwake Masaki.
Sorry, nje ya topic. Mzee Hashim Mbita bado yupo hai? Yuko wapi kwasasa? Namkumbuka sana enzi za wapigania uhuru wa nchi za kusini mwa Africa.
 
Katoliki Lindi limenikumbusha wakati TANU inaasisiwa Southern Province na akina Suleiman Masudi Mnonji, Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Shariffa bint Mzee kwa kutaja wachache Nyerere alipokwenda Lindi akasindikizwa kuhudhuria misa ya Jumapili katika kanisa hilo kasindikizwa na Waislam.

Kutokana na kisa hiki ndiyo nikaandika makala hiyo.
Ni sawa umetukumbusha historia lakini ungejikita kwenye tamko la askofu na sio kuleta stori hizi nyinginezo.
 
Ni sawa umetukumbusha historia lakini ungejikita kwenye tamko la askofu na sio kuleta stori hizi nyinginezo.
Inside10,
Mimi nalijua hilo kanisa nimefika na kuhadithiwa yaliyotokea mle ndani mwaka wa 1955.

Hiyo ndiyo kumbukumbu yangu.
 
Inside10,
Mimi nalijua hilo kanisa nimefika na kuhadithiwa yaliyotokea mle ndani mwaka wa 1955.

Hiyo ndiyo kumbukumbu yangu.
Hamna shida..
Ila taizo hujajikita kwenye tamko la askofu.
Kwanini uweke historia ambayo haiusuiani na tamko..
Lazima mtu awe na masha na lengo lako mzee wangu.
 
Hamna shida..
Ila taizo hujajikita kwenye tamko la askofu.
Kwanini uweke historia ambayo haiusuiani na tamko..
Lazima mtu awe na masha na lengo lako mzee wangu.
Inside10,
Ikiwa unataka nikupe jibu unalolipenda hilo haliwezekani.

Mimi kubwa kwangu ni historia ya kanisa na wale Waislam walioingia kanisani na Mwalimu Nyerere 1955.

Ikiwa kwako hili halina umuhimu kwangu si tatizo.
 
Hamna shida..
Ila taizo hujajikita kwenye tamko la askofu.
Kwanini uweke historia ambayo haiusuiani na tamko..
Lazima mtu awe na masha na lengo lako mzee wangu.
Weeh mgalatia hebu tuliza fuvu lako uulize maswali yenye maantiki...mbn hukukaza fuvu Zumaridi aliposema alienda mbinguni kuonana na Yesu
 
Sasa wagalatia mlikua na vugu vugu lolote la kutaka uhuru zaidi mlikua vibaraka vya wakoloni
Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, DRC, Ghana na nchi nyingine nyingi zilipataje uhuru zikiwa na Wagalatia tupu??
 
Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, DRC, Ghana na nchi nyingine nyingi zilipataje uhuru zikiwa na Wagalatia tupu??
Tanganyika mlikua vibaraka...huko unakokutaja mpk leo wamepewa uhuru wa bendera...
Hebu jikaze basi ukaombewe na Zumaridi fuvu lako lijue kudadavua
 
Inside10,
Mimi si wa kuandika historia isiyokuwa na kichwa.

Angalia video hiyo hapo chini:


View: https://youtu.be/p1ZdZl1wwic

Nakuongezea:

View: https://youtu.be/-jgXNkVj-N0

Naongeza tena:
KUMBUKUMBU YA UHURU NA HOFU YA KUANDIKA HISTORIA YA KWELI YA UHURU WA TANGANYIKA

Hayo hapo chini ndiyo niliyoyaona katika kitabu chenye volume tatu kinachoeleza maisha ya Julius Kambarage Nyerere:

HISTORIA YA AFRICAN ASSOCIATION KATIKA ''A BIOGRAPHY OF JULIUS NYERERE"

(Left Review 133 / 134 Jan Apr 2022)
Issa Shivji, Saida Yahya-Othman and Ng’wanza Kamata, Development as Rebellion: A Biography of Julius Nyerere Mkuki na Nyota: Dar es Salaam 2020, £90, hardback
1208 pp, 978 9 9870 8411 1

''For the first twenty years of German colonial rule, ethnic groups waged guerrilla war, culminating in the ruthlessly extinguished Majimaji Uprising of 1905-07; the memory of the repression silenced political action for two decades.''

Katika kitabu cha Mwalimu Nyerere, ''A Biography of Julius Nyerere,'' mwandishi anasema kuwa katika miaka 20 ya utawala wa Wajerumani vikundi vya kikabila walianzisha vita vya msituni vilivyopelekea kuzimwa kikatili kwa Vita Vya Maji Maji.

Kwa uandishi wa namna hii usiotaka muhali mwandishi anakwepa historia muhimu ya mashujaa wa Maji Maji kwa kuwapa nembo ndogo ya kabila (ethnic group) na kukwepa nembo kubwa na muhimu ya dini yao kuwa Wajerumani walipambana kwa silaha na Waislam.

Ushahidi wa ukweli huu utaupata kwenye minara na makaburi katika kumbukumbu za Maji Maji katika miji ya Kilwa na Songea.

Unachotakiwa kufanya ni kusoma majina katika minara hiyo ya kumbukumbu ingawa pamepitika juhudi ya kubadili majina ya Kiislam kama vile Abdulrauf Songea Mbano kuitwa Songea Mbano likaachwa jina la ''Abdulrauf'' na kukwepa jina la ''Khadija'' likatajwa ''Mkomanile,'' akawa anatambulika kwa jina moja tu la Mkomanile.

Haya ni kwa uchache.

Sasa soma hapo chini kuhusu kuundwa kwa African Association mwaka wa 1929:

''Reorganization slowly gathered pace in 1929, a group of teachers and civil servants formed the African Association, the first in a line of organizations that would evolve into Nyerere’s political party, the Tanganyika African National Union (tanu).''

Mwandishi anasema kuwa African Association imeundwa na kundi la walimu na wafanyakazi wa serikali na anamalizia kwa kusema kuwa hii African Association ikamalizikia katika chama cha TANU cha Nyerere.

Kalamu ya mwandishi haitaki muhali imemuuzia Mwalimu Nyerere chama cha TANU kwa gharama ndogo sana baada ya kumuunganisha na African Association kimya kimya.

Lakini muasisi wa African Association Kleist Sykes kaacha mswada wa kitabu kabla hajafa anaeleza kwa kirefu kabisa vipi African Association iliundwa mwaka wa 1929 na kaweka majina ya waasisi wake: President Cecil Matola, Secretary Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi na Rawson Watts.

Ukisoma kitabu hicho hapo chini utaipata historia yote ya African Association kwa uhakika na ukweli wake na vipi kutokana na African Association ikaundwa Al Jamiatul Islamiyya mwaka wa 1933 President akiwa Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Sykes.

Bila ya kuijua historia hii huwezi kuandika kwa uhakika na ukweli wake historia ya Julius Nyerere na historia ya TANU.

(Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) ''Modern Tanzanians,'' Nairobi, 1973, pp. 95-114).
 
Back
Top Bottom