Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Makwizi,
Mimi Kanisa Katoliki, Lindi limenikumbusha safari ya Julius Nyerere
Southern Province na yale aliyokutananayo huko.

Hili la kanisani ni moja.
Yapo mengi nitakutajia lingine.

Hili ni kisomo yaani dua aliyofanyiwa Nyerere na Sheikh Yusuf Badi.

Makwizi,
Mimi Kanisa Katoliki, Lindi limenikumbusha safari ya Julius Nyerere
Southern Province na yale aliyokutananayo huko.

Hili la kanisani ni moja.
Yapo mengi nitakutajia mawili.

Hili ni kisomo yaani dua aliyofanyiwa Nyerere na Sheikh Yusuf Badi.

''Lakini matukio mawili ya kumbukumbu kubwa yalikuwa katika safari
ya pili ya Nyerere alipozuru tena Jimbo la Kusini.

Kumbukumbu ya kwanza ilikuwa tawaswil aliyosomewa Nyerere na
Sheikh Yusuf Badi mwenyewe pamoja na Waislam aliowachagua yeye
sheikh mwenyewe maalum kwa hafla hiyo.

Wakachanganyika na masheikh wengine kutoka vijiji jirani na Lindi.

Kumbukumbu ya pili ni karamu iliyoandaliwa kwa heshima ya Nyerere
na Mussa Athumani Lukundu, kiongozi wa Dockworker’s Union.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
View attachment 3314598
Sawa mzee, shida yangu ni hi, "Ni upi uhusiano wa uzi wako na hotuba ya baba askofu"? Swali langu lipo hapo.
 
Sawa mzee, shida yangu ni hi, "Ni upi uhusiano wa uzi wako na hotuba ya baba askofu"? Swali langu lipo hapo.
Makwizi,
Nimejibu nimesema kuwa Kanisa Katoliki Lindi limenikumbusha wakati TANU inaasisiwa Southern Province na Nyerere alipokwenda Lindi akasindikizwa kuhudhuria misa ya Jumapili katika kanisa hilo kasindikizwa na Waislam.

Kutokana na kisa hiki ndiyo nikaandika makala hiyo.
 
Usiku mwema mzee wangu
 
Makwizi...
Ahsante sana.

MHANDO WAWILI KATIKA HISTORIA YA TANU: STEVEN NA PETER MHANDO NANI KAPATA KUWASIKIA WAKITAJWA POPOTE?

KITABU KIPYA: WATU MASHUHURI KATIKA UHURU WA TANGANYIKA - SALUM MPUNGA, YUSUF CHEMBERA NA PETER MHANDO
KITABU CHA PILI

TANU ilikuwa na historia ya pekee sana ambayo bado inahitaji kufanyiwa utafiti.

TANU ilikuwa na ndugu wote wanachama, TANU ilikuwa na marafiki wote wanaTANU na kadhalika na kadhalika.

Abdul, Ally na Abbas Sykes, Julius na Joseph Nyerere, Steven na Peter Mhando, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tosiri na Sheikh Mohamed Ramiyya hawa ndiyo niwajua mimi lakini naamini walikuwa ndugu na marafiki wengi waliokuwa ndani ya TANU wakiunganishwa kwa nasaba na urafiki.

Kitabu kipya kufuatilia cha kwanza kilichoeleza mchango wa Sheikh Rashid Sembe, Tewa Said Tewa na Zuberi Mtemvu kitakuwa Ibn Hazm Media Centre, Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 22 November 2019.

Kitabu hiki kinaeleza maisha ya marafiki wawili kutoka Lindi Salum Mpunga na Yusuf Chembera wote wanafunzi wa Sheikh Yusuf Badi jinsi walivyoweza katika hali ngumu ya ukoloni uliokuwa Southern Province (Mkoa wa Kusini) ambako serikali ya kikoloni na mshirika wake mkuu walikuwa wanawatisha wananchi wasijiunge na TANU lakini juu ya vitisho hivi wazalendo hawa kutoka tabaka la chini kabisa waliweza kuwahamasisha wananchi wa mikoa ya kusini kujiunga na TANU.

Wakaweza pia kumuingiza na mwalimu wao Sheikh Yusuf Badi kujiunga na TANU na kujiunga na TANU kwa Sheikh Yusuf Badi kukaipa TANU nguvu kubwa ya kuweza kukieneza chama kote hadi Peramiho, Masasi na kusini yote.

Safari ya kwanza ya mafanikio aliyofanya Mwalimu Nyerere ilikuwa Lindi kwa kuitika mwaliko uliotoka kwa wanachama wa TANU, mwaliko ambao ulifikishwa Ofisi ya TANU wakati wa mkutano wa mwaka wa kwanza wa TANU mwaka wa 1955, na wajumbe kutoka Lindi Salum Mpunga na Ali Mnjale.

Jina la Peter Mhando halijasikika katika historia ya TANU.

Peter ni mdogo wake Steven Mhando ambae na yeye kama kaka yake jina lake halipo katika historia ya TANU ingawa mchango wake ni mkubwa kiasi wakoloni wakamuitikadi kuwa ni Mkomunisti.

Peter Mhando ndiye aliyepelekwa Makao Makuu ya TANU, New Street kutoka Tanga kuja kuongeza nguvu katika uongozi wa TANU uliokuwa Makao Makuu.
Peter Mhando sasa kutoka Dar es Salaam akatumwa Tabora akamalize mgogoro wa TANU uliokuwa unafanya chama kisipige hatua kusonga mbele.

Peter Mhando katika taarifa yake kwa Rais wa TANU Mwalimu Julius Nyerere, alipendekeza Mkutano Mkuu wa TANU wa mwaka wa 1958 ufanyike Tabora na ikasadifu kuwa ndiyo ukawa Mkutano wa Kura Tatu.

Peter Mhando hakuwa na maisha baada ya kukamilisha kazi hii aliyotumwa na Mwalimu Nyerere.

Peter Mhando alikufa kijana sana na hakushuhudia Mkutano wa Kura Tatu.

Hawa ndiyo mashujaa wa TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika ambao historia imewasahau.

Kitabu hiki cha pili ni muendelezo wa vitabu vidogo vya kuwakumbuka mashujaa hawa.
 
Imekuwa ni kawaida mtu kudharau chake na kuthamini cha mwenzake, mikoa ya Kusini, Kilwa, Lindi na Mikindani Mwara, UIslamu
Uliingia siku nyingi kabla ya ukoloni, mfano Mfanyabiashara tajiri, Hassan Bin Amir alikinunua kisiwa cha Kilwa kwa gharama
ya kitambaa kukizunguka Kilwa
Yote hivyo Kilwa mali yake!.

Sultan Seyyid Said, alipofika Zanzibar aliwakuta wenyeji Wakwezi na Wahadimu chini
ya Mtawala wao Mwinyi Mkuu, sijui
walimfanya nini, mara ghafla akahamishia the sultanet yake from Oman to Zanzibar na ghafla Zanzibar ikageuka mali ya Sultan of Zanzibar, hakuna tena kuwazungumzia wenyeji wa Zanzibar wenye Zanzibar yao, wala hakuna historia popote Sultan alivipataje visiwa hivyo!. Mkutano wa Berlin wa 1884 ukamtambua
Sultan of Zanzibar ndio mmiliki halali!, afadhali Mjerumani, aliinunua Tanganyika kwa Sultan Mangungo wa Msovela, kwa mikataba ya ulaghai, but there was something, Zanzibar Mwarabu has nothing to show ndio mmiliki.

Hivyo Mwarabu alijiona Zanzibar ni yake mpaka ile January 12, 1964 wenye Zanzibar yao walipoamka na kumfurusha, wakaitwaa Zanzibar yao kupitia yale
Mapinduzi
Matukufu
ya Zanzibar na ndio mpaka leo, Zanzibar ni ya wenyewe, kila uchaguzi, wenye vinasaba na Mwarabu ni wengi, kila siku wanashinda uchaguzi lakini hawapewi!.

Hata huku Tanganyika,
wenyeji halisi wa Tanganyika ni Wabantu, wengine wote ni watu wa kuja!.
P

TAKATAKA
 
Ni kweli mambo ya dini hayana inshu?
Maana uhuru ulipiganiwa na watu na watu hao walikuwa na dini. Je ni kosa kusema watu wa dini fulani walipigania uhuru? Au itumike misamiati gani ili walau kuepuka kutaja dini?
Naomba tujadili hili.
Hivi mfano, yaani mfano tu. Sasa hvi tuna vyama vingi, say siku moja Chadema wachukue dola and let assume kwamba watakuja kufanya mapinduzi makubwa sana ya Kiuchumi na historia ije iandikwe na tu assume kwamba Chadema itachukua nchi kizazi hiki hiki, Je? Wakati wa kuandika historia tutaanza kuwataja kina Mbowe (from Lutheran ) Lema (mlokole ) halafu Heche (Msabato ) Lissu (Mkatoliki) halafu Salum Mwalimu (muislamu, sijui kama ni Shia au Suni yule) kina profesa Safari (Mwislamu ) na kina Marando wapagani? Hivi hicho kitabu si kitakua kimejaza kurasa zenye mambo mengi yasiokua na maana yoyote? Why kuchoshana? Can't we identify ourselves in the name of the country instead of these useless issues? Mie ni Mkristo, as far as I know hao Wakristo wa kwanza niliowataja hapo ju, only Mbowe (Mluteli ) ndio anaweza kua moderate kama wakianza kujadiri mambo ya dini, akikaza huenda ata angukia upande wa mlokole Lema but Msabato na Mkatoliki plus madhehebu mengine, tunaujua mziki wake, Salumu Mwalimu labda anaweza kuishi na Msabato tu, wengine hazita IVA. Mambo ya dini yangebaki kama mambo binafsi, sio ya kikundi. Hapa ndio divide and rule inapofanya kazi vizuri sana, tunaya kemee
 
Hili neno "inshu" huwa mnalitoa wapi? Hata kama ni kutohoa kutoka neno "issue" basi muandike "ishu". Kwa hiyo unataka kusema hakuna wakristo waliojihusisha kwenye kupigania uhuru hapa Tanzania?
 
Huyu mzee ndie aliyeongoza waislamu wa magomeni kwenda kuvamia na kubomoa mabucha ya nguruwe pale magomeni,sijui sahivi anajiskiaje akiona magomeni watu wanavyo kula kitimoto bila hiyana,what a shame.
Ni kweli au unatania🤣🤣🤣
 
Che...
Mimi naandika historia naeleza yale ambayo wengi hamkuwa mnayajua.
Ulikuwa unajua kuwa watu watatu ndiyo waliopewa kazi ya kuisajili TANU?

Watu hao ni Abdul na Ally Sykes kadi zao Ally kadi yake ya TANU No. 2 na ya
kaka yake Abdul No. 3 na ya Julius Nyerere TANU Territorial President kadi yake
No. 1 na aliandikiwa na Ally Sykes na yeye ndiye alisanifu kadi na akachapa
kadi 1000 Printpak wachapaji wa gazeti la Tanganyika Standard kwa fedha zake
binafsi.

Haya kwako ni malalamiko?
Hii ya kuhama nchi inakujaje katika kuandika historia ya TANU?

Wapi nimeandika kuhusu sharia na hayo mengine?

Hakika maandiko yangu ni haya haya na laiti kama nisingeandika
mengi katika historia ya Tanganyika yangepotea.

Wewe ulikuwa unajua kuwa safari ya kwanza UNO dhifa ya kumuaga
Nyerere ilifanyika katika Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika?

Jengo la Umoja wa Waislam wa Tanganyika.
Hii si sehemu ya historia ya uhuru wa Tanganyika?

Ulikuwa unamjua Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa Al
Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pia Mweka Hazina wa kwanza
wa TANU.

Kadi yake ya TANU No. 24 na ndiye aliyekuwa mkusanyaji wa fedha
za safari ya Nyerere UNO 1955.

Iddi Faiz ni kati ya watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza
wa TANU Arnautoglo Hall Agosti 1955.

Moyo unakuuma kusoma historia hii?
Acha usiisome kujitesa bure.

Ikiwa wewe unaona historia hii ni pumba sawa hakuna neno acha wengine
waisome kwa furaha.

Huna sababu ya kuja hapa kutukana na kutoa maneno ya ufedhuli.
Mimi kwako ni baba.

Wanao mimi ndiyo babu yao.

View attachment 3313524
Kushoto: Iddi Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi
Taratibu Dodoma Railway Station 1955/56 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
View attachment 3313532
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika
Wewe usingeenda shule ungekuwa mchawi
 
Jarib

Baba yangu mimi naomba unisaidie jambo moja dogo tu..

Lengo lako hasa la andiko hili nini?!
Maana tamko la askofu huyo wa Lindi lilikuwa ni kuzungumzia uchaguzi wa huru na haki, pia kuachiwa kwa wanasiasa (lissu) ambae anadai taratibu sahihi za uchaguzi na mwenendo wake?

Sasa wewe umekuja na historia uhuru lindi nà mambo ya lindi kuwa mji wa kiislamu, uhusiano wake na tamko la askofu ni nini?!

Ahsante ukinijibu hili moyo wangu utakuwa umesuhuzika.
Huyo mzee anazeeka vibaya na uislam umemfanya anakuwa kama taahira. Yaani anatafuta tu kitu ilimradi alete upuuzi wake.
 
Hivi mfano, yaani mfano tu. Sasa hvi tuna vyama vingi, say siku moja Chadema wachukue dola and let assume kwamba watakuja kufanya mapinduzi makubwa sana ya Kiuchumi na historia ije iandikwe na tu assume kwamba Chadema itachukua nchi kizazi hiki hiki, Je? Wakati wa kuandika historia tutaanza kuwataja kina Mbowe (from Lutheran ) Lema (mlokole ) halafu Heche (Msabato ) Lissu (Mkatoliki) halafu Salum Mwalimu (muislamu, sijui kama ni Shia au Suni yule) kina profesa Safari (Mwislamu ) na kina Marando wapagani? Hivi hicho kitabu si kitakua kimejaza kurasa zenye mambo mengi yasiokua na maana yoyote? Why kuchoshana? Can't we identify ourselves in the name of the country instead of these useless issues? Mie ni Mkristo, as far as I know hao Wakristo wa kwanza niliowataja hapo ju, only Mbowe (Mluteli ) ndio anaweza kua moderate kama wakianza kujadiri mambo ya dini, akikaza huenda ata angukia upande wa mlokole Lema but Msabato na Mkatoliki plus madhehebu mengine, tunaujua mziki wake, Salumu Mwalimu labda anaweza kuishi na Msabato tu, wengine hazita IVA. Mambo ya dini yangebaki kama mambo binafsi, sio ya kikundi. Hapa ndio divide and rule inapofanya kazi vizuri sana, tunaya kemee
Historia ya harakati kuunda African Association inaanza 1924 miaka 100 iliyopita pale Dr. Kwegyir Aggrey kutoka Ghana, Achimota College alipokutana na Kleist Sykes Dar es Salaam.

Dr. Aggrey alimuuliza Kleist endapo Waafrika wana jumuiya yao kama Wazungu, Waasia na Waarabu.
Jibu lilikuwa hawana.

Dr. Aggrey akamuuliza Waafrika wanawakilishwa vipi?
Kleist akamwambia mwakilishi wa Waafrika ni Mzungu kutoka Minaki Mission jina lake Father Gibbons.

Dr. Aggrey akamshauri Kleist kuwa ni lazima Waafrika wawe na jumuia yao wajiwakilishe wenyewe.

Kazi hii Kleist aliifanya na akaasisi African Association 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 akajenga ofisi ya African Association hapo leo ilipo CCM, akajenga jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Kabla hajafariki 1949 alikuwa keshaandika historia hii ya maisha yske na mswada wa kitabu cha maisha yake akamwachia mwanae Abdulwahid Sykes.

Historia hii imehifadhiwa Dar es Salaam University Library, East Africana na ipo kama sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians (1973).

Historia hii mimi nimeiandika upya katika, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968), The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," London 1997.

Kitabu hiki kimefanyiwa book review tatu zote zikachapwa kwa wakati tofauti katika Cambridge Journal of African History.

Yapo mengi sana.

1745663463640.png

Dr. Kwegyr Aggrey
1745663582108.jpeg

Kleist Sykes (1894 - 1949)

Tusimame hapa kwa sasa.
Yapo mengi sana.
 
Huyo mzee anazeeka vibaya na uislam umemfanya anakuwa kama taahira. Yaani anatafuta tu kitu ilimradi alete upuuzi wake.
Mwaka wa 1950 mwaka mmoja tu baada ya Kleist kufariki Abdu Sykes na Hamza Mwapachu wakafanya mapinduzi na kuuondoa uongozi wa zamani wa TAA Rais akiwa Thomas Plantan na Katibu Clement Mohamed Mtamila.

TAA ikapata uongozi mpya wa vijana: Rais Dr. Vedasto Kyaruzi na Katibu Abdul Sykes.

Ikaundwa TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa Dr. Vedasto Kyaruzi Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir (Mufti wa Tanganyika), Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Earle Seaton Mwanasheria kutoka Moshi akaambatanishwa kama mshauri wa TAA katika mashauri ya Mandate Territory.

Kamati hii ndiyo iliyoongoza TAA hadi kuundwa kwa TANU 1954.

Yapo mengi sana.
Tusimame hapa kwa sasa.

1745664728605.png

Kulia ni Abdul Sykes (1924 - 1968) na
Hamza Mwapachu (1913 - 1962)

1745665092921.png

1745664850303.jpeg

Thomas Plantan
 
Huyo mzee anazeeka vibaya na uislam umemfanya anakuwa kama taahira. Yaani anatafuta tu kitu ilimradi alete upuuzi wake.
Katoliki Lindi limenikumbusha wakati TANU inaasisiwa Southern Province na akina Suleiman Masudi Mnonji, Salum Mpunga, Yusuf Chembera, Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Shariffa bint Mzee kwa kutaja wachache Nyerere alipokwenda Lindi akasindikizwa kuhudhuria misa ya Jumapili katika kanisa hilo kasindikizwa na Waislam.

Kutokana na kisa hiki ndiyo nikaandika makala hiyo.
 
Wewe usingeenda shule ungekuwa mchawi
Prof. Haroub Othman alikuwa kahuzunika sana siku tulipokutana na akaniuliza kuhusu historia ya TANU na uhusiano wake na ukoo wa Sykes.

Hakika kitabu cha Abdul Sykes ni uchawi.

Hukisomi ukakosa kuathirika na utakayosoma humo.
 
Historia ya harakati kuunda African Association inaanza 1924 miaka 100 iliyopita pale Dr. Kwegyir Aggrey kutoka Ghana, Achimota College alipokutana na Kleist Sykes Dar es Salaam.

Dr. Aggrey alimuuliza Kleist endapo Waafrika wana jumuiya yao kama Wazungu, Waasia na Waarabu.
Jibu lilikuwa hawana.

Dr. Aggrey akamuuliza Waafrika wanawakilishwa vipi?
Kleist akamwambia mwakilishi wa Waafrika ni Mzungu kutoka Minaki Mission jina lake Father Gibbons.

Dr. Aggrey akamshauri Kleist kuwa ni lazima Waafrika wawe na jumuia yao wajiwakilishe wenyewe.

Kazi hii Kleist aliifanya na akaasisi African Association 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 akajenga ofisi ya African Association hapo leo ilipo CCM, akajenga jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Kabla hajafariki 1949 alikuwa keshaandika historia hii ya maisha yske na mswada wa kitabu cha maisha yake akamwachia mwanae Abdulwahid Sykes.

Historia hii imehifadhiwa Dar es Salaam University Library, East Africana na ipo kama sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians (1973).

Historia hii mimi nimeiandika upya katika, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968), The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," London 1997.

Kitabu hiki kimefanyiwa book review tatu zote zikachapwa kwa wakati tofauti katika Cambridge Journal of African History.

Yapo mengi sana.

View attachment 3316287
Dr. Kwegyr Aggrey
View attachment 3316291
Kleist Sykes (1894 - 1949)

Tusimame hapa kwa sasa.
Yapo mengi sana.
Mzee wangu mimi nakuelewa sana tu, sikiliza swali au ushauri wa Dr. Aggrey kwa mzee Sykes (according to yourself) mnayo jumuia yenu? Jibu lilikua ni HAPANA, sasa yeye (sijui ni makusudi au bahati mbaya kwa mujibu wa tafsiri za sasa) yeye akaunda umoja wa KIDINI na sio wa Watanganyika; naweza kuhisi why TAA ilibidi ife na kuzaliwa TANU, umoja wa kidini ubakie makanisani na misikitini, huko ndio wajadiri umoja wao na wa deal na mambo yao ya dini. Kwani mzee, haiwezekani mimi na wanao tunawa na jambo letu tukalifanya kwa pamoja ambalo halina uhusiano na mambo ya dini? Mfano kuna biashara tunataka kufanya kwa pamoja labda Zambia, halafu ikifika Ijumaa mwanao anaenda zake msikitini kusali na mimi Jumapili naenda zangu church? I'm sure huo ndio ushauri wa Dr. Aggrey to your brother Sykes, misikitini jadirini namna ya kusikimisha watu, kanisani as well but huku mtaani tujadiri kuhusu maisha na future yetu na watoto katika nchi yetu
 
Nakushauri usome kitabu cha Abdul Sykes.
Sykes aliunda African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Vyama viwili tofauti malengo tofauti ingawa kuna wakati President African Association alikuwa Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Abdallah Sykes na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika President Mzee bin Sudi na Secretary Kleist Abdallah Sykes.

Vyama viwili tofauti lakini viongozi ni walewale.
Hii hstoria ilipowekwa hadharani watu walishtuka.

Hawa mimi babu zangu si "brother" historia hii ni historia ya nyumbani kwetu.

1745676761795.jpeg

Kulia Kleist Sykes na Mzee bin Sudi
 
Back
Top Bottom