Mbalizi feedstuff
JF-Expert Member
- Feb 23, 2025
- 238
- 269
Hiki kizee sijui kimeahidiwa mabikira wangapi huko jehanamu
Mbalizi...Hiki kizee sijui kimeahidiwa mabikira wangapi huko jehanamu
Huyu Mzee ni mdini kupitiliza alitaka Tanganyika iwe Islamic Republic lakini kashindwa kabisa.Anasema lindi ulikua mji wawaislam anasahau huo uislam wenyewe uliletwa nawawaarab lindi ulikua mji wamababu zetu ukiwa naiman zakiafrika
Sina tatizo na fikra zako.Tatizo lako hupendi mawazo kinzani.
Mimi sijawahi kukutukana popote ingawa nimeona wengine wanakuambia kuwa ni Mdini.
Mimi sijaghadhibika ila nakupa iliyo kweli:
Historia yako inalenga kutubagua kidini:
Historia ya ujumla tumekubaliana kuwa Watanzania wote tulishirikiana kuleta Uhuru na Umoja ili kudumisha mshikamano kwa vizazi vijavyo:
Historia yako inasema ni Waislamu pekee ndio waliopigania Uhuru wa Tanzania:
Kwa historia yako hii unaitengenezaje Tanzania ijayo kama msomi ?
Hivi vita ya Majini maji ya kumtaa mkoloni ilipiganwa na Waislamu pekee ?
Au Mtemi Mkwawa wa Iringa alipigana na Mjerumani kwakuwa tu alikuwa Mwislamu ?
Kama sivyo hao watawala hawakuwa chachu ya kupigania uhuru wa Mtanzania?
Watu wa Pwani walipambana kumwondoa mkoloni kama watu wa Bara:
Bila ya kuangalia kabila au dini zao:
Wote walishikamana kumwondoa mkoloni:
Habari za Waislamu pekee ndio waliofanya jitihada za kumwondoa mkoloni Mzungu hazina manufaa kwa Watanzania wasasa na wajao:
Kila eneo la Tanganyika lilipambana kumwondo mkoloni katika eneo lao na sio watu wa Dini fulani:
No Reform no Election!Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?
N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.
Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.
Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:
Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.
Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.
Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.
Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.
Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.
Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.
Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.
Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.
Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.
Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.
DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.
Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.
Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.
Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.
Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.
Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.
Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.
Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.
Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.
TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.
www.facebook.com
Habari ya Kanisa la Lindi inahisiano vipi matamshi ya Askofu Jumapili?!Sina tatizo na fikra zako.
Mimi nimefafiti historia ya uhuru na akili yangu imeniambia kuwa
kukosekana kufamika kwa historia ya hao wote waliokuwa hawako
katika historia ya uhuru si sawa.
Ndiyo nimeandika kitabu cha Abdul Sykes.
Watu wengi wanashtuka wanaposikia historia kwanza ya babu yake,
Sykes Mbuwane aliyeingia German Ostafrika na Herman von Wissman,
baba yake Kleist Sykes na wazalendo wengine wa wakati ule kama Sheikh
Hassan bin Ameir, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Earle Seaton kwa
kuwataja wachache.
Kwa kazi hii nimealikwa vyuo vikuu vingi ndani na nje ya mipaka yetu kutoa
mihadhara.
Ikiwa wewe hupendezewi wala mimi sikubughudhi.
Naheshimu msimamo wako.
Angalia picha hapo chini Al Jazeera wamekuja kutoka Qatar kufanya mahojiano
na mimi mwaka wa 2007:
View attachment 3314146
Makulaga,Habari ya Kanisa la Lindi inahisiano vipi matamshi ya Askofu Jumapili?!
JaribWagalatia ni shida sana, yaani mtu akiandika uislam haraka sana mnambandika udini, ila ukiandikwa ukristo kila mmoja anafurahia,
Kwa ushahidi tu wa mazingira nani mdini?
Alishindwa firauni nfio mtaweza nyie?
Inside10
Baba yangu mimi naomba unisaidie jambo moja dogo tu..Sina tatizo na fikra zako.
Mimi nimefafiti historia ya uhuru na akili yangu imeniambia kuwa
kukosekana kufamika kwa historia ya hao wote waliokuwa hawako
katika historia ya uhuru si sawa.
Ndiyo nimeandika kitabu cha Abdul Sykes.
Watu wengi wanashtuka wanaposikia historia kwanza ya babu yake,
Sykes Mbuwane aliyeingia German Ostafrika na Herman von Wissman,
baba yake Kleist Sykes na wazalendo wengine wa wakati ule kama Sheikh
Hassan bin Ameir, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Earle Seaton kwa
kuwataja wachache.
Kwa kazi hii nimealikwa vyuo vikuu vingi ndani na nje ya mipaka yetu kutoa
mihadhara.
Ikiwa wewe hupendezewi wala mimi sikubughudhi.
Naheshimu msimamo wako.
Angalia picha hapo chini Al Jazeera wamekuja kutoka Qatar kufanya mahojiano
na mimi mwaka wa 2007:
View attachment 3314146
Waarabu wanaojulikana na kanisa kuwa walileta uislamu walikuja karne ya Saba kutoka Oman , uislamu uliletwa na waafrika wenyewe , kwani mwanzo uliletwa nchi ya Ethiopia na ukasambaa mpaka kufika huku kwetuUliletwa na nani mkuu?!
Basi tufanye Waislamu ndio walio upigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Na kama Watanzania tumekubali hizo juhudi za Waislamu:
Kwasasa nini kifanyike ?
Kwako Muhamed said
Mkuu 'inside10', umegonga penyewe hasa. Sina la ziada la kuongezea hapa. Ni wazi hawa waTanzania wenzetu wana ajenda nyingine zaidi ya kujenga umoja na mshikamano kati yetu.Na hii ndio point kubwa nadhani mzee wangu Mohamed Said atusaidie uhusiano wa tamko la askofu na andiko lake juu ya historia ya uislamu na uhuru hapo Lindi. Alitaka kumaanisha nini hasa au kusema nini?!
Maana kauli ya askofu ipo wazi juu haki za raia ktk uchaguzi na kuteswa kwa wapinzani.
Cc Kalamu Pascal Mayalla
..ni moja ya wadau walioeneza na kuimarisha uislamu
Naona amekwepa sana kunijibu na nimemkumbishia tena kwenye post #188Mkuu 'inside10', umegonga penyewe hasa. Sina la ziada la kuongezea hapa. Ni wazi hawa waTanzania wenzetu wana ajenda nyingine zaidi ya kujenga umoja na mshikamano kati yetu.
Jarib
Baba yangu mimi naomba unisaidie jambo moja dogo tu..
Lengo lako hasa la andiko hili nini?!
Maana tamko la askofu huyo wa Lindi lilikuwa ni kuzungumzia uchaguzi wa huru na haki, pia kuachiwa kwa wanasiasa (lissu) ambae anadai taratibu sahihi za uchaguzi na mwenendo wake?
Sasa wewe umekuja na historia uhuru lindi nà mambo ya lindi kuwa mji wa kiislamu, uhusiano wake na tamko la askofu ni nini?!
Ahsante ukinijibu hili moyo wangu utakuwa umesuhuzika.
Lengo lake ni kueleza historia ya TANU Lindi.Jarib
Baba yangu mimi naomba unisaidie jambo moja dogo tu..
Lengo lako hasa la andiko hili nini?!
Maana tamko la askofu huyo wa Lindi lilikuwa ni kuzungumzia uchaguzi wa huru na haki, pia kuachiwa kwa wanasiasa (lissu) ambae anadai taratibu sahihi za uchaguzi na mwenendo wake?
Sasa wewe umekuja na historia uhuru lindi nà mambo ya lindi kuwa mji wa kiislamu, uhusiano wake na tamko la askofu ni nini?!
Ahsante ukinijibu hili moyo wangu utakuwa umesuhuzika.
Inside10,Naona amekwepa sana kunijibu na nimemkumbishia tena kwenye post #188
KalamuLengo lake ni kueleza historia ya TANU Lindi.
Naeleza kile kilichotokea ndani ya Kanisa Katoliki, Lindi wakati
wanachama wa TANU walipomsindikiza Mwalimu Julius Nyerere
ndani ya kanisa hilo kwa ajili ya Misa ya Jumapili.
Hapakuwa na mwanachama hata mmoja Mkristo kumsindikiza
Mwalimu Kanisani.
Hii ikasababisha Mwalimu asindikizwe na Waislam.
Nakuongezea mengine hapo chini katika historia ya TANU Lindi:
''Salum Mpunga alimsisitizia Nyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANU kupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya TANU.
Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU.
Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wote waliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili.
Baada ya kufikia makubaliano, Mpunga na Ali Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari ya Nyerere.
Ziara ya Nyerere ilikuwa ianze muda mfupi kutokea hapo kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku za mwisho za kiangazi.
Barabara sehemu ya kusini ya Tanganyika zilikuwa hazipitiki wakati wa masika, zikiitenga kabisa kusini toka sehemu zilizobaki za nchi.
Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi na woga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.''
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Kwanza historia hiyo anayodai ndiyo sahihi, inaorodhesha majina tu. Hata siku moja hutasikia akitoa maelezo ya hao watu walifanya nini. Hata mikutano kama ilikuwepo haielezwi ilifanyika wapi na kilizungumzwa kitu gani kinachoonyesha kupigania uhuru!Jarib
Baba yangu mimi naomba unisaidie jambo moja dogo tu..
Lengo lako hasa la andiko hili nini?!
Maana tamko la askofu huyo wa Lindi lilikuwa ni kuzungumzia uchaguzi wa huru na haki, pia kuachiwa kwa wanasiasa (lissu) ambae anadai taratibu sahihi za uchaguzi na mwenendo wake?
Sasa wewe umekuja na historia uhuru lindi nà mambo ya lindi kuwa mji wa kiislamu, uhusiano wake na tamko la askofu ni nini?!
Ahsante ukinijibu hili moyo wangu utakuwa umesuhuzika.
Hawezi kuwa na jibu la hoja hiyo, kwa sababu nia ya maelezo yake haikulenga kabisa kilichosemwa na yule askofu. Yeye alikuwa na lengo tofauti kabisa; lengo la kusambaza yale anayo yapigania maisha yake yote.Kalamu
Jibu la ile hoja yako ambayo niliikazia kwenye #131 ndio hili..
Swali la ziada mzee wangu..
Kulikuwa kuna haja gani nakuambatanisha na kauli ya askofu wakati ni vitu viwili tofauti?!
Ukiacha suala la historia yake na wazee wake..Kwanza historia hiyo anayodai ndiyo sahihi, inaorodhesha majina tu. Hata siku moja hutasikia akitoa maelezo ya hao watu walifanya nini. Hata mikutano kama ilikuwepo haielezwi ilifanyika wapi na kilizungumzwa kitu gani kinachoonyesha kupigania uhuru!
Vikao vingi inaonyesha vilikuwa kama vya 'club' eneo la Kariakoo pekee, hakuna mahali pengine popote hao wanaotajwa katika historia hiyo walipafikia kwa lengo la kueneza habari za kutafuta uhuru.
Kiufupi, maelezo ya huyo mzee ni utapeli mtupu.
Anachoweza kujivunia ni ujuzi wake wa kupangilia mambo katika hali inayoweza kuvuta hisia za mwasomaji, hasa wale ambao akili zao tayari zimejiegemeza katika uamini wa anayoyasimulia.