Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?

N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.

Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.

Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.

DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.

Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.

Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.

Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.

Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.

Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.

Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.

Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.

Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.

TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

Kama hakukuwa na waumini walimjrngea nani kabisa? Kwanini kila political move ijengwe dini na nasaba? Kwanini hoja ya huyo Askofu iletwe kwenye mizania ya uhuru unaonasibishwa na uislam?
 
Mohammed Said ,mara zote ni Anti-Christ na anti Christianity.
Nia yake siku zote ni kwamba Nyerere hakuwa lolote wala si chochote.
Huwa haongelei kabisa shule za kikristo zilizotaifishwa ili waislamu wasome.
Mohammed Said kalemaa.
Mkapa kawapa chuo kikuu Morogoro, wao wemyewe hawaongelei hilo na chuo kimedumaa.

Sisi tuliopo DSM siku nyingi tunajua Mwalimu aliwakaribisha Wamisri wakati huo tukiwa na uhusiano mzuri na Gamal Abdel Nasser, rais wa Misri.
Mwalimu aliwaomba Misri 1968, kujenga chuo cha waislamu pale Chang’ombe(opposite DUCE).
Leo miaka 57 baadaye hakuna chuo cha waislamu, badala yake pamegeuzwa Container Yard ya wafanyabiashara wa kihindi.
Hii nahadithia nimeona kwa macho yangu toka 1968.

Mohammed Said huwa ni mchochezi wa mfarakano wa kidini, ilhali yeye mwenyewe hana mchango wowote kwa waislamu ila kuwalalamikia wakristo kwa kudumaa kwake.
 
Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?

N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.

Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.

Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.

DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.

Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.

Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.

Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.

Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.

Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.

Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.

Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.

Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.

TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

Sijaona point yoyote inayo endana na tamko la maaskofu. Mtoa maada kabla ya kuleta maada humu, yakupasa usome vizuri na uwe na uhakika wa muunganiko wa fikra na kichwa cha habari.
 
Anasema lindi ulikua mji wawaislam anasahau huo uislam wenyewe uliletwa nawawaarab lindi ulikua mji wamababu zetu ukiwa naiman zakiafrika
LINDI NA KUSINI haikuwa nchi ya kiisalamu, hiyo dini ililetwa na waarabu wakifanya biashara ya kununua na kuuza watumwa, Mtwara-mikindani ilikuwa ni depot ya biashara ya watumwa (slave trade DEPORT), ili kuwapeleka Zanzibar and beyond
 
Mjahidina ameandika takataka (rubbish)...Sio kila jambo ni lakuandikia/kuzungumzia, mengine aache yajipitie.

Wacha leo CCM iwatandike , waTanganyika mnaanza kuelewa kidogo kidogo , mtaelewa tu .

Wazanzibari yametufika mengi zaidi ya hayo na yanakuja tu kidogo kidogo . Mlishindwa kutetea haki mkaona ni sawa tu kwa wazanzibari yawafike , leo yameanza kuwafika nyinyi .

Hao maaskofu walikuwa wakiona raha wakati wazanzibari wakikandamizwa na Mkapa na nyerere wake .
Maelfu ya watu waliuliwa katika uvamizi wa Nyerere.

Chama cha upinzani cha CUF /ACT , muda wote kinakuwa kinapigwa vita vibaya na watu kuuliwa na viongozi kupigwa na kubambikiziwa hizo kesi za uhaini.

KANISA LENU NA MAASKOFU WAKE , WAKATI WOTE LIKO KIMYA , na unapozungumza kuhusu madaraka kamili na kuhoji huu uvamizi uliopewa jina la muungano, jawabu zao ni hizi za kifedhuli na jeuri

Kardinali Pengo: Muungano si bahati nasibu
 
Ni kumbukumbu nzuri sana kuhusu Uhuru wetu lakini nadhani wengi wetu kama hatupendi hivi kuisikia na wakati mwingine tunawaona au tunamuona mwandishi kama muongo.
👇👇👇👇
Makosa yalifanyika wapi kiasi watu kutokupenda historia kusikia historia yao ya uhuru?

Uhuru wa Tanganyika haupo na Chama cha TANU kilichopigania uhuru hakipo .
TANU na Tanganyika havipo na uhuru wake umepitea ndio maana nchi ya Tanganyika haina dira zaidi ya matakwa ya mtawala na zama zake.

Wale waislam Wa Tanganyika waliokuwa wakarimu wenye upendo na uzalendo walitea baada ya Azimio la Zanzibar kuletwa na Mwinyi . Pakaibuka uislam wa kujitenga na kuona kuwa uislm bora ni ule wa kujifunza Kareti ,judo na kutumia silaha . Ndio maana watu hawana tena ule uzalendo wa kupigania haki bali wanaangalia maslahi yao
 
Sijaona point yoyote inayo endana na tamko la maaskofu. Mtoa maada kabla ya kuleta maada humu, yakupasa usome vizuri na uwe na uhakika wa muunganiko wa fikra na kichwa cha habari.
Na hii ndio point kubwa nadhani mzee wangu Mohamed Said atusaidie uhusiano wa tamko la askofu na andiko lake juu ya historia ya uislamu na uhuru hapo Lindi. Alitaka kumaanisha nini hasa au kusema nini?!

Maana kauli ya askofu ipo wazi juu haki za raia ktk uchaguzi na kuteswa kwa wapinzani.
Cc Kalamu Pascal Mayalla
 
Mohammed Said ,mara zote ni Anti-Christ na anti Christianity.
Nia yake siku zote ni kwamba Nyerere hakuwa lolote wala si chochote.
Huwa haongelei kabisa shule za kikristo zilizotaifishwa ili waislamu wasome.
Mohammed Said kalemaa.
Mkapa kawapa chuo kikuu Morogoro, wao wemyewe hawaongelei hilo na chuo kimedumaa.

Sisi tuliopo DSM siku nyingi tunajuaMwalimu aliwakaribisha Wamisri wakati huo tukiwa na uhusiano mzuri na Gamal Abdel Nasser, rais wa Misri.
Mwalimu aliwaomba Misri 1968, kujenga chuo cha wais,amu pale Chang’ombe(opposite DUCE).
Leo miaka 57 baadaye hakuna chuo cha waislamu, badala yake pamegeuzwa Container Yard ya wafanyabiashara wahindi.
Hii nahadithia nimeona kwa macho yangu toka 1068.

Mohammed Said huwa ni mchochezi wa mfarakano wa kidini, ilhali yeye mwenyewe hana mchango wowote kwa waislamu ila kuwalalamikia wakristo.
Jidu...
Huijui historia hii.
 
Basi tufanye Waislamu ndio walio upigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Na kama Watanzania tumekubali hizo juhudi za Waislamu:

Kwasasa nini kifanyike ?
Kwako Muhamed said
 
Na hii ndio point kubwa nadhani mzee wangu Mohamed Said atusaidie uhusiano wa tamko la askofu na andiko lake juu ya historia ya uislamu na uhuru hapo Lindi. Alitaka kumaanisha nini hasa au kusema nini?!

Maana kauli ya askofu ipo wazi juu haki za raia ktk uchaguzi na kuteswa kwa wapinzani.
Cc Kalamu Pascal Mayalla
Inside10,
Uhusiano ni hilo kanisa na historia yake na Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Julius Nyerere.

Ndiyo nikauliza Askofu anaijua historia hiyo?

Kwengine nilikopata kuieleza historia hiyo swali la kwanza huwa, "Kwani TANU Lindi haikuwa na wanachama Wakristo?"
 
Ni kumbukumbu nzuri sana kuhusu Uhuru wetu lakini nadhani wengi wetu kama hatupendi hivi kuisikia na wakati mwingine tunawaona au tunamuona mwandishi kama muongo.
👇👇👇👇
Makosa yalifanyika wapi kiasi watu kutokupenda historia kusikia historia yao ya uhuru?
Kwa sababu tunajua kuwa historia ya Tanganyika na waliopigania uhuru wake ilipindishwa maksudi kuwatenga waliokuwa na mawazo tofauti na Nyerere
 
Kwani uwongo wa alichosema ni upi hapo.Mababu zetu tunasema hawakuwa na dini rasmi.
Kama ni dini rasmi basi uislamu ndio wa mwanzo maeneo yote ya nchi yetu.Na kila harakati ilianza na waislamu iwe ni kilimo au biashara
Mzee wetu ndio maana kaamua kuhamia facebook zaidi baada ya kuona JF kuna wapuuzi wengi.
Maoni niliyasoma fb yamenisikitisha wote wanamuinga mkono hakuna reasoning hata kidogo..
Kifupi fb kuna watu wenye mdogo wengi au waliopo wanashindwa kuamsha mjadala.
 
Ndugu Muhamed said, wewe pendekeza tu:
Labda kama unataka sisi wa dini nyingine tuhamie Kongo mmbaki wapigania uhuru Waislamu hapa Tanzania wewe pendekeza tu:

Au kama unapendelea Tanzania ifuate Islamic Laws muwe mnachinja Mashoga na Wazinzi kila Ijumaa baada ya swala wewe sema tu.

Tatizo lako ndugu Muhamed Saidi, kila andiko lako ni la kulalamika tu:

Sisi tunao kufuatilia tunataka sasa utoe hitimisho (Conlusion)

Na kuna hitimisho Mbili tu:

Mosi, tuwa achie Wapigania uhuru Waislamu hii nchi, kwakuwa ndio walio uleta Uhuru:

Pili, tugawane mikoa,
Waislamu mpate mikoa yenu ili muishi kwa kutekeleza Sharia zenu kwa kushirikiana na waasisi wa dini yenu Waarabu:

Sisi Wakristo tupewe mikoa yetu na ni marufuku kwa Mkristo au Mwislamu kuishi katika mkoa usio wake:

Kati ya hitimisho hizi mbili Mzee Msomi Muhamedi Saidi unachagua ipi ?

Tumechoka na maandiko yako yaleyale ya kila siku:
Sema unataka nini?

Utafiti bila hitimisho ni kama Pumba tu:
 
Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?

N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.

Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.

Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.

DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.

Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.

Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.

Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.

Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.

Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.

Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.

Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.

Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.

TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

mbona kanisa katoliki Iindi liko Mtanda huko juu kilimani?
 
Back
Top Bottom