Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Fundi...
Wewe huipendi historia hii lakini wengi wameipenda na kunipa tuzo zinafika tano:

View attachment 3311703

Tafsiri ya kwanza ya Kiswahili haikuchukua muda vitabu vyote vilivyokuwa
sokoni vikamalizika ikabidi vichapwe vitabu vingine India.

Angalia hapo chini:

View attachment 3311704
Mohammed, sio suala la kuipenda au la. Mimi napingana na wewe siku zote kwa upotoshaji wako ambao ni hatari kwa sababu jamii yetu ni rahisi sana kuamini chochote kinachoandikwa. Angalia tu waliokupa tuzo na utajua base yako ni ya wakina nani. Unachokifanya sio kizuri. Unawaharibu hao wanaokupa tuzo.

Yaani seriously unataka tukuamini kuwa Mwalimu aliyekuwa mkatoliki mzuri alihitaji ulinzi wa waislamu dhidi ya wakristu wenzake? Kinachosikitisha ni kuwa hao waliokupa tuzo watakuamini.

Unakosea sana unapotaka kufanya kuwa historia ya nchi hii ni ya waislamu peke yenu. Na wanaostahili kutetewa ni waislamu peke yao. Sio vizuri.

Amandla...
 
Jiulize kwa nini Nyerere alikuwa peke yake hakuna Mkristo hata mmoja katika kundi lile la wanachama wa TANU mjini Lindi?

Vuta subira tutakwenda Mikindani In Shaa Allah utaisoma historia ya Mwalimu.
 
Inside10,
Sikutegemea hata kidogo kama post hii yangu itagusa watu wengi kiasi hiki.

Nimeamua In Shaa Allah kukuelezeni historia yote vipi TANU iliingia Lindi na Southern Province yote kama nilivyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes (1998):

TAA mjini Lindi ilikuwa chini ya uongozi wa Suleiman Masudi Mnonji aliyekuwa Rais na Katibu wake alikuwa Mohamed Waziri. Mnonji alikuwa fundi cherahani na Waziri alikuwa mchoraji wa ramani za nyumba. TAA ilichelewa kuanza mjini Lindi. TAA ilianzishwa Lindi mwaka 1953 wakati uongozi wa TAA mjini Dar es Salaam si tu ulikuwa unaigeuza TAA kuwa chama cha siasa bali ulikuwa ukifanya mipango kumpeleka mjumbe wake Umoja wa Mataifa kudai uhuru.

Masudi Mnonji alikuwa na uzoefu wa kutosha katika siasa. Baada ya Vita Kuu ya Pili alikuwa amejaribu kuanzisha vyama vya wafanyakazi katika mashamba mbalimbali ya mkonge kusini mwa Tanganyika. Vilevile aliwakusanya wapishi na madobi mjini Lindi waanzishe umoja wao. Ilikuwa kupitia juhudi zake binafsi TAA ijapokuwa ilichelewa, ilikuja kuanzishwa mjini Lindi na Mnonji alijitolea nyumba yake katika mtaa wa Makonde kama ofisi ya chama.

Mnonji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uongozi ulioelimika vizuri, alimleta Nangwanda Sijaona kutoka Nachingwea aje aishauri TAA jinsi ya kufanya mambo kwa utaalamu. Wakati huo mjini Lindi kulikuwa na chama cha wafanyakazi bandarini Dockworkersí Union chini ya uongozi wa Mussa Athumani Lukundu, chama ambacho kwa kiasi chake kilianzisha vuguvugu la siasa za vyama vya wafanyakazi. Ingawa vyama hivi viwili, yaani TAA na Dockworkersí Union vilikuwepo katika mji mmoja, siasa za hiki chama cha pili cha wafanyakazi bandarini hazikupitia TAA kama ilivyokuwa mjini Dar es Salaam. Hii kidogo ilidhoofisha mwamamko wa siasa kwa wananchi.

Jimbo la Kusini lilikuwa katika usingizi mzito wakati sehemu nyingine Tanganyika zilikuwa zikipiga hatua kwenda mbele zikiandaa vita dhidi ya utawala wa kikoloni. Chanzo cha usingizi huu mzito huko kusini ulikuwa na asili yake katika historia ya Tanganyika.

Vita vya Maji Maji vilipoanza kusini ya Tanganyika mwaka 1905 kwa nia ya kuwafukuza Wajerumani kutoka Tanganyika, zile sehemu zenye Wakristo wengi zilikataa kujiunga na vita na badala yake wakajiunga na majeshi ya Wajerumani na kupigana bega kwa bega na dhidi ya wazalendo.

Hii ilitokana na sababu ya kuwa uasi dhidi ya dhulma wa Wajerumani ulianza katika maeneo yenye Waislam wengi na vita vikachukua sura ya vita vya Kiislamu dhidi ya Wazungu ambao dini yao ni Ukristo. Kwa kuwa wamishonari walikuwa washirika wa wakoloni, walichukuliwa kama maadui na hivyo ikawa vituo vyao vinashambuliwa na wapiganaji wa Maji Maji.

Kutokana mashambulizi haya, Wakristo walivichukua Vita Vya Maji Maji kama vita dhidi ya Ukristo. Harakati za Maji Maji zilishindwa na Wajerumani walifanya ufisadi kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wao. Jambo hili liliacha kovu kubwa katika fikra za wananchi na kwa upande wa Wakristo ambao walinusurika na ghadhabu ya Wajerumani, wengi wao wakajiweka mbali na aina yoyote ya kupinga ukoloni.

Kufuatia historia hii Waafrika waliokuwa kusini ya Tanganyika sasa wakiwa chini ya utawala wa Waingereza na kuwa chini ya himaya ya wamishonari walipumbazwa kiasi kiasi kwamba waliogopa siasa. Baada ya Waafrika kushindwa vita kwa silaha kali za Wazungu sasa Kanisa likaona ndani ya fadhaa ile fursa yao kutawala sehemu hiyo kwa kutoa vishawishi kama vile shule na hospitali.

Kwa hiyo Wamishionari na Waingereza walionekana kama mabwana wema wenye kuwajali raia zao kinyume na serikali katili na ya kidhalimu ya Wajerumani. Vuguvugu la siasa kama ilivyokuwa Vita vya Maji Maji, lilianza katika maeneo ya Waislam kufuatia mfumo ule ule kama ilivyokuwa katika upinzani wa ukoloni wa Wajerumani. Wakristo katika Jimbo la Kusini waliiona TANU kama walivyoviona Vita Vya Maji Maji, kama harakati nyingine za Waislam zilizokuwa zinakuja tena kwa mara ya pili kuvuruga amani na utulivu.

TANU ilipoanza ikawa inavuma kuwa safari hii Waislam walikuwa wamemua kuanzisha vita dhidi ya Waingereza kama walivyoanzisha vita na Wajerumani.

View attachment 3311647
Tafsiri hii ya Kiswahili ya kwanza imechapwa na Phoenix Publishers, Nairobi 2002.

(Itaendelea...)
Cc Kalamu Pascal Mayalla
 
huyo mzee ni 'specialist' wa kuamsha hisia za udini kila anapo andika chochote. naona huo ndio wito wa maisha yake!
Kalamu,
Hapana siamshi hisia yoyote iwayo ile.

Niandikayo ni mambo ya kweli yaliyotokea yote yamo ndani ya kitabu cha Abdul Sykes.

Hii ni historia ambayo haikupata kufahamika kwa miaka mingi sana.

Matokeo yake ikawa kuwa na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika iliyokuwa na upungufu mkubwa mno.
 
Mzee Said, yote haya tulisha jibishana wewe na mimi miaka michache iliyopita humu humu JF. Msimamo wangu katika maandishi yako unaeleweka, na sioni sababu ya kurudia tena tuliyokwisha malizana kati yetu.
 
Ukristo Lindi na Mtwara ulikuwa mgeni kwenye miji ya Pwani. Mara nyingi makanisa yakijengwa nje ya miji, na Wakristo wakikaa huko!

Anachoshangaa Mzee MS ni huyu Mjeruman Wolfgang kutia kibesi kwenye miji ambako yeye ni mhamiaji tu!

Anyways, inawezakana hayo ni historia, lakini kwenye hili TEC wanapandikiza chuki na udini mkali,!

Walipoongoza WAISLAM harakati kama hizi TEC na mazezeta yao humu JF mliwaita majina mabaya , vipi Leo?

Kuna ujinga unarudiwa humu karibu Kila post kuwa sijui hawa Maaskofu wamesoma sijui PhD, watu hawajiulizi ni PhD za nini? Mfano wa wazi ni Slaa mwenye PhD ya canonical law! Maana yake sheria ya kanisa ! Hii inatofauti Gabi na sheikh mbobezi kwenye FIQH? Hiyo PHD ibachukua miaka 4 tu lakini kupata ijaza ya FIQH kutoka kwa vyuo kama Al Azhar utakula mpaka miaka 20!
Hakuna dini inaitwa uislam wala hakuna dini inaitwa ukristo

Historia inaonyesha walioanza kuandika mambo ya uislamu ilikuwa mwishoni mwa karne ya tano yaani miaka 500 BK.Sasa kabla ya japo hizo karne ya 3,4 yaani miaka 300, 400 kulikuwa na kitu gani?

Na maeneo hayo ya Mecca wakati huo watu hawakujua kusoma wala kuandika isipokuwa watu wawili tu

Soma historia vizuri

Huko Vatican Roma ndiko kuna fichwa kumbukumbu na ukweli halisi wa historia za haya mambo ya uislam na ukristo
 
Kwa maoni yangu naona Mzee Saidi anaongelea mchango wa dini hasa viongozi wa dini ya kiislamu katika kupigania uhuru wa nchi yetu dhidi ya ukoloni, hivo anatukumbusha kuwa wanachokifanya Maaskofu kutetea Haki za wananchi ni sawa na kilichofanywa na waislamu kwa wakati huo.
Hivyo mchango wa viongozi wa dini si wa kupuuzwa. Kama sipo sawa mnaweza kunisahihisha au hata yeye mwenyewe Mzee Saidi anaweza kuendelea kutuelewesha zaidi ili tuelewe maantiki yake, badala ya kumshambulia kuwa ni mdini.
Sure
 
Fundi...
Jiulize kwa nini Nyerere alikuwa peke yake hakuna Mkristo hata mmoja katika kundi lile la wanachama wa TANU mjini Lindi?

Vuta subira tutakwenda Mikindani In Shaa Allah utaisoma historia ya Mwalimu.
Wafanyakazi katika serikali ya mkoloni walijiunga na TANU kwa kujificha kwa kuogopa kupoteza ajira. Wao ndio walikuwa makarani, walimu, wauguzi n.k. Hata Nyerere ilibidi aache kazi ya ualimu ili afanye siasa. Ni kama vile ilivyo leo ni vigumu sana kumkuta mwanachama wa Chadema au ACT-WAZALENDO wa waziwazi serikalini. Lakini ukisema kuwa serikalini hamna mwanachama au mpenzi wa Chadema au ACT-WAZALENDO utakuwa umekosea.

Amandla...
 
Mzee Said, yote haya tulisha jibishana wewe na mimi miaka michache iliyopita humu humu JF. Msimamo wangu katika maandishi yako unaeleweka, na sioni sababu ya kurudia tena tuliyokwisha malizana kati yetu.
Kalamu,
Mzee Said, yote haya tulisha jibishana wewe na mimi miaka michache iliyopita humu humu JF. Msimamo wangu katika maandishi yako unaeleweka, na sioni sababu ya kurudia tena tuliyokwisha malizana kati yetu.
Kalamu,
Ukiwa umehitimisha na mie usinitaje.
Nimekujibu kwa kuwa umenitaja.
 
Wafanyakazi katika serikali ya mkoloni walijiunga na TANU kwa kujificha kwa kuogopa kupoteza ajira. Wao ndio walikuwa makarani, walimu, wauguzi n.k. Hata Nyerere ilibidi aache kazi ya ualimu ili afanye siasa. Ni kama vile ilivyo leo ni vigumu sana kumkuta mwanachama wa Chadema au ACT-WAZALENDO wa waziwazi serikalini. Lakini ukisema kuwa serikalini hamna mwanachama au mpenzi wa Chadema au ACT-WAZALENDO utakuwa umekosea.

Amandla...
Fundi...
Hebu nipe majina ya hao watumishi wa serikali waliokuwa wanachama wa TANU nikupe majina ya wanachama waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo Hall Agosti 1954.
 
Anasema lindi ulikua mji wawaislam anasahau huo uislam wenyewe uliletwa nawawaarab lindi ulikua mji wamababu zetu ukiwa naiman zakiafrika
Unajua Ibn Batuta alipita Lindi akielekea Kilwa na Sofala mwaka gani na alikuta misikiti ya Waajemi.
Ndio faida ya kwenda shule na kujua historia
 
Sipendelei mijadala inayohusu dini, kwasabu kwangu nasisitiza hayana ishu, ishu kwangu ni kuwa na uhusiano mzuri na Mungu na kutenda mema baaas....

Hayo ya sijui mkristu na muislamu kuna bora kuliko mwingine sio ishu, quran ni bora kuliko biblia sio ishu.....nasisitiza tena HAYANA ISHU

Kwahiyo inapaswa mambo tuyaadress kwa hivi??

"Nyerere rais wa kwanza ambae alikua ni mkristu alitupigania tukawa huru"
"Rais kikwete muislamu alijitahidi sana upande wa ajira watu waliajiriwa kwa wakati"
"Rais mkapa mkristu blablabla"
"Waziri gwajima mkristu anajitahidi kushughulikia mambo ya kijamii"

Itoshe kusema ni UPUMBAVU!!!!!
Tungekua proud na nchi yetu kuliko dini zetu tungefika mbali sana aisee.

Ila serikali ililijua hilo, mkiipenda sana nchi yenu hamchelewi kupindua serikali, ikajaza udini pomoni.
 
Changamoto ni kwamba anachoandika hakina reference zaidi ya yeye mwenyewe
Castr:
Rejea kubwa niliyotumia ni Nyaraka za Sykes.

Nenda Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam East Africana kuna Seminar Paper A.D. Sykes, "The Life of Kleist Sykes," Ref. No. JAN/HIST/143/15 (1968).

Labda useme huzitambui.

KIPINDI CHA KENNETH DAVID KAUNDA TBC

Angalia kipindi hiki cha TBC kisha tafadhali soma makala hapo chini kuna mengi katika historia ya TANU watu hawayajui:

Leo Kenneth Kaunda katimiza miaka 97.

Nimeangalia picha ya Kenneth David Kaunda na picha hii ikanikumbusha uhusiano wa Kaunda na Ally Kleist Sykes wakati Afrika ilipokuwa katika harakati ya kupigania uhuru wake.

Usiku umekuwa mwingi In Shaa Allah kesho nitaeleza vipi Ally Sykes na Kenneth Kaunda walifahamiana miaka ya 1950 wakati Northern Rhodesia sasa Zambia na Tanganyika zilipokuwa zinapigania uhuru wake.

Ally Sykes mzee wangu nimemvulia kofia katika kutunza kumbukumbu.

Faili la safari yake yeye na Dennis Phombeah kwenda Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano wa vyama vya siasa Kusini ya Ikweta naamini ndilo faili mwenyewe akilipenda kuliko mafaili yake yote yenye taarifa za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ndani ya faili hili kuna ''cuttings'' ya magazeti zikieleza mkasa mzima wa safari yake kutokea Dar es Salaam hadi Salisbury ambako yeye na Phombeah walitiwa mbaroni na makachero wa Kikaburu kama ''Waafrika Wakorofi,'' na kufungiwa ndani ya banda nyuma ya nyumba ya Mzungu usiku kucha.

Asubuhi wakaachiwa na kuamriwa kurudi Tanganyika kama wahamiaji wasiotakiwa.

Hii ni movie ni ''block blaster,'' ambayo itahitaji waigizaji mahiri kucheza nafasi ya Ally Sykes, Denis Phombeah, Kenneth Kaunda, Harry Nkumbula, Charles Mzengele kachero, kibaraka wa Wazungu walowezi wa Southern Rhodesia, kachero kibaraka wa Waingereza Tanganyika, Alexander Thobias, Trevor Huddleston Mwingereza muungwana aliyekuwa rafiki wa Waafrika.

Mwaka wa 1953 Harry Nkumbula alikuwa amechaguliwa rais wa ANC na Kenneth Kaunda aliteuliwa Katibu Mwenezi wa Jimbo la Kaskazini.

Mwezi Agosti Kaunda akawa Katibu Mkuu wa ANC.

Hapa ndipo Kaunda akaanza kuwatafuta wanasiasa wenzake waliokuwa Tanganyika, Kenya na Afrika Kusini na kuwaalika kwenye mkutano Lusaka, Northern Rhodesia ambao ungewakutanisha wapigania uhuru kutoka nchi za Afrika chini ya Ikweta.

Hivi ndivyo Kenneth Kaunda na Ally Sykes walivyokuja kufahamiana kwa kuandikiana barua ambazo Ally Sykes alizihifadhi hadi mimi kuja kuzisoma miaka mingi baadae.

Katika kusoma nyaraka kama hizi ndipo nikamwelewa Ally Sykes pale alipokuwa akiniambia, ''Hawa walioandika historia ya TANU hawana moja wanalolijua.''

Mkasa wa safari hii ya Ally Sykes na Denis Phombeah kuhudhuria mkutano wa Lusaka ni kisa kirefu sana lakini chote nimekieleza katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Nimeweka picha ya Charles Mzengele kachero kibaraka wa walowezi ikifuatiwa na picha ya Kenneth Kaunda na Harry Nkumbula kama walivyokuwa katika miaka ya 1950.

Ally Sykes alikuwa akitamka jina hili kama ''Mzengele,'' lakini usahihi wa jina la huyu kachero ni Mzingeli.
 
Na hichi ndicho nimekisema. Umeiandika Historia ambayo wengi hatuijui ila kwa kumuuliza Abdul Sykes na wanachama wenzake.

Hii inatoa wigo kuongeza au kupunguza chumvi na hakuna wa kucounter hoja.
 
Fundi...
Hebu nipe majina ya hao watumishi wa serikali waliokuwa wanachama wa TANU nikupe majina ya wanachama waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglo Hall Agosti 1954.
Hilo swali halina mantik. Hata nikikutajia, utathibitisha vipi kuwa ninasema ukweli? Nikikuambia kuwa rafiki yake mjomba wangu alikuwa anafanya kazi hospital na alijiunga na TANU mwaka 1958 utathibitishaje kuwa nasema uongo?

Hivyo hivyo nitathibitisha vipi kuwa hao utakaosema ndio walihudhuria ni kweli au umechakachua? Na ukiwataja, haithibitishi kuwa hakuna watumishi wa serikali walikuwa wanachama mpaka pale tulipopata uhuru 1961. Tatizo lako siku zote unataka tuchukue simulizi zako kuwa ni "gospel truth" bila kuwa ushahidi wowote. Siko tayari kucheza mchezo wako.

Amandla...
 
Back
Top Bottom