Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Na hichi ndicho nimekisema. Umeiandika Historia ambayo wengi hatuijui ila kwa kumuuliza Abdul Sykes na wanachama wenzake.

Hii inatoa wigo kuongeza au kupunguza chumvi na hakuna wa kucounter hoja.
Castr,
Historia ya African Association vipi iliasisiwa mwaka wa 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 iliandikwa na Kleist Sykes baba yake Abdul Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Historia hii ipo Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam, East Africana kama Seminar Paper ya Idara ya Historia (1968).

Seminar Paper hii imeandikwa na mjukuu wa Kleist, bint wa Abdul Sykes jina lake Aisha Daisy Sykes akiwa mwanafunzi University of East Africa 1968 akisoma History and Education.

Zipo pia Nyaraka za Sykes ambazo ndizo nilizotumia kuandika historia ya TANU kupitia maisha ya Abdul Sykes.

Nyaraka hizi zinarudi nyuma miaka 100.
 
Ni facebook huku akinakili video ya tamko la Askofu Wolfang Pissa Ambaye Pia Ni Rais Wa Baraza La Maaskofu Katoliki Tanzania.
--------------------------
ASKOFU ANAIJUA HISTORIA YA KANISA KATOLIKI LINDI TANU ILIPOINGIA SOUTHERN PROVINCE 1955?

N miaka mingi sasa toka nilipofika kuliona Kanisa Katoliki Lindi wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Kanisa hili lina historia nzuri sana baina ya Salum Mpunga, Yusuf Chembera na Waislam wengine wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Nakuwekea hapo chini kipande nilichoandika kuhusu kanisa hili mwaka wa 1955 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika:

Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la fahari lililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi.

Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbali na mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa na kile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa.

Watu wachache waliokuwa wakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemu nyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali.

Ghafla mahala hapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawa muhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja ya kuhudhuria ibada pale kanisani.

Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindi aliyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yao aliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale.

Uongozi wa TANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyerere kanisani ili kumpa ulinzi.

Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimaye iliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazima wamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisa Katoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa na Salum Mpunga, dereva wa lori shupavu.

Misa hii ‘’maalum,’’ ilidumu katika fikra za wale Wakristo waliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sana Wakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi.

Hii huenda ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwa amesimamiwa na Waislam.

DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanya mkutano wa hadhara.

Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wa dharura wa tawi la TANU uliohudhuriwa na Nyerere na Ali Mwinyi Tambwe.

Baada ya mkutano huo Tambwe alikwenda kumwona DC.

Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili, katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmoja uliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyo Waafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara.

Kamwe haijapata kutokea kabla ya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hicho kujumuika mahali pamoja.

Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwa wamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerere akihutubia.

Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliweka askari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano.

Nyerere aliwafikishia watu ule ujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazima wadai uhuru wao.

Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwa niaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhi nchi kwa wananchi wenyewe.

TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

The principle of rule of thumbs is: don't quote your self- PLO Lumumba
 
Ila huyu mzee apumzike bas, udini unamtafuna mno. Lol
Coca...
Nimeandika historia iliyorekebisha historia ya TANU kwa uhakika wake.
Katika ukweli huu ndipo unapojitokeza mchango wa Waislam.

Ikiwa historia hii huipendi kwa kuwa unawasoma Waislam hiyo ni bahati mbaya sana kwako.
 
The principle of rule of thumbs is: don't quote your self- PLO Lumumba
James...
Huu ni mwanzo wa "serialisation" ya sehemu ya kitabu cha Abdul Sykes inayoeleza vipi TANU iliingia Southern Province mji mkuu wake ukiwa Lindi.

Hii siyo "quotation."

Naweka sehemu ya pili In Shaa Allah tuendelee kusoma historia hii.
 
Anasema lindi ulikua mji wawaislam anasahau huo uislam wenyewe uliletwa nawawaarab lindi ulikua mji wamababu zetu ukiwa naiman zakiafrika
Kwani uwongo wa alichosema ni upi hapo.Mababu zetu tunasema hawakuwa na dini rasmi.
Kama ni dini rasmi basi uislamu ndio wa mwanzo maeneo yote ya nchi yetu.Na kila harakati ilianza na waislamu iwe ni kilimo au biashara
Mzee wetu ndio maana kaamua kuhamia facebook zaidi baada ya kuona JF kuna wapuuzi wengi.
 
Huu ukweli alioandika Mzee Mohammed Said unawababua na kuwatia wahka wale wapindisha historia ya nchi. Historia haifichiki au kupotoshwa , ukweli utatoka tu.
Mzee angusha nondo tu tujifunze.
 
Huu ukweli alioandika Mzee Mohammed Said unawababua na kuwatia wahka wale wapindisha historia ya nchi. Historia haifichiki au kupotoshwa , ukweli utatoka tu.
Mzee angusha nondo tu tujifunze.
Percival,
Tunaendelea na historia ya TANU ilivyoingia Southern Province:

Mikindani
Tukio dogo la kiburi cha askari mpumbavu wa mkoloni ndiko kulisababisha watu wa Mikindani wafungue tawi la TANU.

Askari mmoja mpita njia aliingia katika ubishi na kijana mmoja wa pale mjini, akiitwa Hassan Masudi Vuni. Akitumia mamlaka yake ya kukamata mhalifu, askari huyo alimpiga Vuni kwa kumuonea. Miongoni mwa watazamaji wa tukio hilo alikuwa Rashid Ali.

Rashid Ali alikwenda kusimulia tukio hili kwa Mohamed Ali Abdallah. Alipokuwa akisimulia mkasa ule, pamoja naye alikuwa Suleiman Hassan Msepele. Walipokuwa wakijadiliana Msepele alitamka kwamba tukio kama hilo kamwe lisingeweza kutokea Dar es Salaam kwa sababu Mwafrika mmoja kwa jina lake Julius Nyerere alikuwa ameanzisha chama cha siasa kupigania uhuru.

Rashid Ali na Mohamed Ali Abdallah walitamani kujua mengi zaidi kuhusu Mwafrika huyu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Nyerere na chama chake cha siasa, lakini Msepele hakuwa na mengi ya kueleza kuhusu Nyerere na chama chake. Kwa hiyo basi, hawa watu watatu waliamua kumtuma mtu Dar es Salaam kupata habari zaidi kuhusu chama hicho. Mohamed Ali aliandika barua na kumpa Msham Awadh na Ali Muhidin kumpelekea Nyerere. Ndani ya barua hiyo Mohamed Ali alimweleza Nyerere kwamba ukoloni ulikuwa bughudha kubwa katika Jimbo la Kusini, na wangependa kufungua tawi la TANU mjini Mikindani ili kupigania uhuru wa Tanganyika.

Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake. Mshama Awadh alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili. Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba. Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni. Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya kimagharibi. Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Rupia, Chamwenye, Kambona na Dossa katika makao makuu ya TANU, New Street.

Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani. Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda Lindi kukutana na Mnonji na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU. Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali na akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe watu kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.
 
Mantiki yake ni nini?!
Huyo Mzee huwa anaandika chochote ilimradi ataje Nyerere, Sykes, Waislam na Uhuru.

Na anachoamini maisha ya dunia hii, yalianza baada ya Uislam.

Yaani watu wote anaotaja , hawajawahi kuwa na maisha nje ya Uislam.

Nadhani anatamani, badala ya neno watu itumike neno Waislam.
 
Ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa CCM pia ni chama cha upinzani lakini watanzania walio wengi wanaamini CCM ni chama walichoumbiwa kutawala Tanzania milele.
Siku dhana hii ikitoka watauona mwanga ukiliangazia taifa hili na kuondoka wakoloni hawa wenye ngozi nyeusi wasiopenda kuona watanzania wakifurahia upendeleo wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu juu ya nchi yao.
 
Ipo siku huyu mzee atakuja na makala yenye kichwa,Mchango wa Waislam katika kuijenga chadema.
Inspector...
Unadhani mie ni mtu wa wewe kunifanyia kejeli?:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES

The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi, 2006

Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.

Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.

Uamuzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No. 1, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam.

Watu Mashuhuri Katika Uhuru wa Tanganyika No.2, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dar es Salaam na Wazalendo Wake Mashujaa Katika Kupigani Uhuru wa Tanganyika Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaaam

Watu Mashuhuri Katika Kuulingania Uislam Tanzania, Sheikh Ilunga, Ibn Hazm Media Centre 2018, Dar es Salaam

Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania, Ibn Hazm Media Centre, 2018, Dar es Salaam

The School Trip to Zanzibar, Africa Proper Education Network 2020, Dar es Salaam

Rajabu Ibrahim Kirama, Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam, Readit, 2020, Dar es Salaam

In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).

Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).

Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).

Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).

Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).

Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).

Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, Nairobi.

Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg.

Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

Awards: Several Awards

Visiting Scholar: (2011)

University of Iowa, Iowa City, USA

Northwestern University, Chicago, Illinois, USA

Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.

OTHER COUNTRIES VISITED​

Zambia, Ethiopia, Great Britain, Swaziland, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Sudan, Egypt, Saudi Arabia, United Arab Emirates, Oman, Yemen, Uganda, Switzerland, Iran, France, Netherlands, Turkey and Abu Dhabi.
 
Punguza Udini babuu, pokea huu ukweli.
Cocastic,
Kitabu cha Abdul Sykes kwa mara ya kwanza kilichapwa London mwaka wa 1997.
Kitabu hiki kiliamsha fikra za wasomi wengi ulimwenguni mabingwa wa historia
ya Afrika mfano wa hao hapo chini.

Maprofesa hawa wakafanya ''book review'' - John Iliffe (University of Cambridge),
Jonathon Glassman (Northwestern University) na James Brennan (University of
Champaign).

Hizi ''reviews'' zote zikachapwa katika Cambridge Journal of African History.
Hawa wote hakuna aliyesema nimeandika udini.

Walishangazwa iweje miaka yote hii wao wakisomesha historia ya Tanganyika
ambayo ilikuwa na mashimo mengi.

Sasa angalia uzito wa wasomi hao na vyuo wanavyosomesha na angalia uzito
wa journal ambalo lilichapa ''review'' ya kitabu changu.

Mimi naandika kuelimisha jamii siko hapa kufanya maskhara.
Nimekuwa Mwandishi Bora hapa JF miaka miwili mfululizo.

Kwako mimi ni baba si babu.
Wanao mimi ndiyo wanaweza kuniita babu.

Kama ni watoto wa kike nitawatania kuwaita wake zangu.
Kama ni wanaume mke wangu atawaita waume zake.

Hizi ndizo adabu zetu.
Ufedhuli hauna manufaa kwa yeyote.

1745418407259.jpeg
 
Huyo Mzee huwa anaandika chochote ilimradi ataje Nyererere, Sykes, Waislam na Uhuru.

Na anachoamini maisha ya dunia hii, yalianza baada ya Uislam.

Yaani watu wote anaotaja , hawajawahi kuwa na maisha nje ya Uislam.

Nadhani anatamani, badala ya neno watu itumike neno Waislam.
Mpwimbe,
Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya TANU Nyerere ametajwa sana.

Aliyekosekana katika historia hiyo alikuwa Abdul Sykes na wengine wengi wao
Waislam.

Kitabu changu kimesahihisha kosa hili.
Mimi si mtu wakuandika chochote.

Fanya uchunguzi kiasi kidogo hili utalitambua.
 
Cocastic,
Kitabu cha Abdul Sykes kwa mara ya kwanza kilichpwa London mwaka wa 1997.
Kitabu hiki kiliamsha fikra za wasomi wengi ulimwenguni mabingwa wa historia
ya Afrika mfano wa hao hapo chini.

Maprofesa hawa wakafanya ''book review'' - John Iliffe (University of Cambridge),
Jonathon Glassman (Northwestern University) na James Brennan (University of
Champaign).

Hizi ''reviews'' zote zikachapwa katika Cambridge Journal of African History.
Hawa wote hakuna aliyesema nimeandika udini.

Walishangazwa iweje miaka yote hii wao wakisomesha historia ya Tanganyika
ambayo ilikuwa na mashimo mengi.

Sasa angalia uzito wa wasomi hao na vyuo wanavyosomesha na angalia uzito
wa journal ambalo lilichapa ''review'' ya kitabu changu.

Mimi naandika kuelimisha jamii siko hapa kufanya maskhara.
Nimekuwa Mwandishi Bora hapa JF miaka miwili mfululizo.

Kwako mimi ni baba si babu.
Wanao mimi ndiyo wanaweza kuniita babu.

Kama ni watoto wa kike nitawatania kuwaita wake zangu.
Kama ni wanaume mke wangu atawaita waume zake.

Hizi ndizo adabu zetu.
Ufedhuli hauna manufaa kwa yeyote.

View attachment 3313203
Sawa baba, nakubaliii
 
Back
Top Bottom