Alichofanya Eliya Mtishbi na Tukipasacho Kufanya Dhidi ya Korona: Baada ya Kumwomba Mungu

Tanzania hatuko serious hata kidogo, ni kuanzia kwa viongozi hadi raia wa kawaida!.
- shule zimefungwa lkn watoto wapo mtaani ktk makundi wanapuyanga kwa uhuru wao.
- vijiwe vya kahawa,bao,karata, vipo vinaendelea kama vile hakuna tatizo
- makundi ya wapiga debe kwenye vituo vya daladala ya kutosha kabisa.
- baa bia zinanyweka hapo hapo, vilabu vya usiku biashara zaendelea.
Mamlaka/ serekali - ndo hopeless kabisa wanaishia kusema tu na kufanya siasa kwenye janga la corona, hawawezi hata kusimamia maagizo wanayoagiza yafatwe ktk udhibiti wa ugonjwa huu. Waziri wa afya asishie kutangaza walio ambukizwa tu na vifo v/s walio pona bali ahakikishe pia prescriptions za kudhibiti maambukizi zinafuatwa ( case ya Mwanza ya mtu aliye toka dubai akapitiliza JKINA hadi Mwanza nilitarajia kusikia watu wamewajibika lkn hadi sasa sijasikia, hata mkuu wa mkoa mwenye kujifanya anajali wakaazi wa mkoa wake kwa kutangaza mahasimu wake kisiasa kuwa wana maambukizi ya corona, naye alikaa kimya akabariki watumishi ndani ya mkoa wake wasitekeleze maagizo ya serekali kwa kuruhusu washukiwa wa covid- 19 waendelee na uhuru wao huku wakiambukiza)

Mzee Mwanakijiji ukitaka serekali isimame kidete dhidi ya ugonjwa huu inabidi inabidi covid-19 apewe jina la upinzani specifically Chadema, hapo ndo utaona kuanzia mjumbe wa serekali ya mtaa mpaka rais wanyanyuka wote kupambana, majeshi yote kama ilivyo taja hapo juu yatainuka na kubani na kudhibiti huyo corona/Chadema tena bila kusubiri amri. Nakuhakikishia kabisa tukifanikiwa kumpa corona jina la Chadema, dawa ya corona itavumbuliwa Tanzania!.
 
Mwanakijiji,

Habari ya Detroit mzee!

Laiti kama nguvu ya kunyanyasa na kuua CHADEMA ingetumiwa kuiangamiza corona ingelikuwa imeisha

Mwanzoni Polepole alipatia aliposema corona ni kama upinzani na nilitegemea:

-risasi kama alizopigwa Lissu
-kukataliwa kuombewa
-kukataliwa kulipiwa matibabu
-kunyimwa mshahara
-kutishiwa kifo na Musiba
-kufutwa ubunge

Sasa tutubu kwanza hadharani halafu ndiyo tuanze maridhiano na siyo aridhio la kuwapamba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What if kama ndio manabii wetu ni
Na. M. M. Mwanakijiji

Tunaweza kumwomba Mungu atusaidie kutuepusha na janga la ugonjwa wa korona. Kama binadamu na watu wenye imani tunaelewa wazi kuwa mwisho wa siku mambo yote yako mikononi mwa Mungu. Tunapojiachilia katika huruma na wema wake tunakiri uwezo na uwepo wake lakini pia tunakiri ubinadamu wetu. Kumwomba Mungu hakuwezi kuwa kosa. Nchi zote zilizoendelea ambazo nazo zimepigwa na majanga ya korona watu wake nao wanamwomba Mungu na kumlilia.

Kila siku hapa Marekani kuna watu wanakutana kwenye njia ya simu, Facetime, Skype na njia mbalimbali za mawasiliano kumwomba Mungu. Japo kwenye majimbo mengi ibada za hadhara zimesitishwa lakini siku ya Pasaka kwa mfano kwenye Jimbo Kuu Katoliki la Detroit Askofu Mkuu aliadhimisha Misa Takatifu akiwa na watu wachache tu kwenye Kanisa Kuu. Misa ile ilirushwa moja kwa moja na televisheni na kwenye Facebook na Youtube na sisi waumini tulifuatilia tukiwa majumbani mwetu. Mungu yupo mahali popote.

Kwa Wakristu kuna mstari unaosema kuwa “Wakutanapo wawili au watatu kwa Jina langu mimi nipo kati yao” (Mathayo 18:20). Mstari huu una maana kuwa uwepo wa Mungu katika ibada hauitaji wingi wa watu. Utendaji wake hauitaji mkusanyiko mkubwa wa watu. Katika maandiko tunakutana na mifano kadha wa kadha wa jinsi Mungu alivyoweza kutenda kwa kumtumia mtu mmoja au wawili tu au watu wachache lakini akafanya makubwa.

Mojawapo ya masimulizi makubwa yenye kusisimua katika Biblia ni kile kisa cha Elia Mtishbi. Baada ya watu wa Israeli kudanganywa na Manabii wa Baal, Elia akaamua kuwapa changamoto. Akawaambia kuwa yeye ni mtu mmoja tu aliyebakia akiwa ni Nabii wa BWANA na Baal alikuwa na “manabii” 450. Elia akataka kuwaonesha yupi ni Mungu wa kweli basi; yule mwenye Nabii mmoja aliyebakia au yule mwenye nabii 450 wenye mbwembwe nyingi. Simulizi hili linatuonesha kuwa Elia akawapa nafasi manabii wa Baali kumwomba Mungu wao atekekeze (aunguze) kwa moto sadaka walizoziandaa kwenye madhabahu.

Manabii wale 450 walianza kumwomba mungu Baal na kulia na kujichanja huku wakipiga kelele. Kwa kuwaangaliwa kwa nje unaweza kuamini walikuwa na imani zaidi, na kwa kelele na vilio vyao mungu wao angewasikiliza. Elia aliwadhihaki na kuwaambia labda waongeze sauti inawezekana mungu wao alikuwa amelala! Waliposhindwa ndipo Elia akaingia kazini yeye peke yake na bila sala ndefu tena katika jambo lisilowezekana (aliwaagiza waandalizi wake wamwagie maji zile sadaka mara tatu (alichimba na mfereji wa maji kuzizunguka kabisa). Na kwa sala fupi kabisa na yenye nguvu akamwita Yehova Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Alipomaliza tu sala yake na kabla ya kusema “Amina” Moto ulishuka toka mbinguni na kutetekeza sadaka zile na kuyakausha maji yale!

Ndipo watu wakajua kuwa Yehova ndiye Mungu. Unaweza kusoma kisa hiki kwenye 1 Wafalme 18:20-40.

Ndugu zangu, Rais Magufuli yuko sahihi kutaka Watanzania waliombee Taifa na hata bila yeye kutaka hivyo nina uhakika watu wenye imani wamekuwa wakiliinua taifa letu na watu wetu kwa dua na sala mbalimbali. Huu ni wajibu wetu; lakini siyo tu sisi dunia nzima inamlilia Mungu kumwomba. Hili haliwezi kuwa jambo baya wala la kudharau.

Na inawezekana Mungu ameshaanza kujibu sala na dua hizi. Mwanzoni mwa baa hili kulikuwa na hofu kuwa ugonjwa huu utaathiri zaidi Afrika labda kuliko bara nyingine lolote. Hata sasa maambukizi na vifo kwenye bara letu hayaendani na wingi na mtawanyiko wa watu wetu.

Pamoja na hayo bado Mungu anatupa nafasi ya kujiandaa zaidi. Haitoshi kumwomba Mungu na sisi bila kufanya au kuchukua hatua makini. Tayari taifa limechukua hatua mbalimbali ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sahihi. Baadhi ya hatua zimechelewa sana na matokeo yake ndio tunaona maambukizi yakiongezeka badala ya kupungua. Na yameongezeka kwa haraka zaidi siku hizi za karibuni na tusipoangalia yanaweza kuongezeka zaidi ndani ya siku chache (kama tutafuata kama ilivyotokea nchi nyingine).

Lengo la Mikakati

Sasa hivi, lengo la mikakati yoyote inayochukuliwa na nchi ni kupunguza kasi ya maambukizi, kudhibiti wagonjwa wapya, na kuwalinda watu ambao bado hawajaambukizwa. Katika kupunguza kasi ya maambukizi ndipo panalala kazi kubwa ya kuidhibiti korona. Unaposoma habari mbalimbali duniani kwenye nchi zinazohangaika na ugonjwa huu sehemu kubwa ni kuwa kasi ya maambukizi mapya bado ni kubwa au ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba mifumo ya afya haikuweza kujiandaa nayo. Chukulia kwenye jimbo la Michigan ambako ninaishi.

Mgonjwa wa kwanza wa Corona alitangazwa Machi 10. Leo hii (mwezi mmoja na wiki moja baadaye) jimbo hili lina wagonjwa karibu 30,000 na vifo zaidi ya 2000! Na hapa ni pamoja na ukweli kuwa tumekuwa chini ya “lockdown” kwa karibu mwezi mzima! Watu wengi hawaendi kwenye makazini, michezo, hakuna ibada za hadhara n.k Na inadaiwa hatua zilizochukuliwa Michigan ni miongoni mwa hatua kali zaidi kuchukuliwa na jimbo lolote la Marekani.

Sasa, kama kwenye taifa hili lilioendelea hivi, lenye raslimali za kila namna watu wake wanaambukizwa kwa kasi hivi na kufa itakuwaje kwetu? Bila ya shaka kuna mambo (factors) ambazo zinafanya ugonjwa huu kuwa wa hatari zaidi kuliko nyumbani. Siyo kwamba watu wetu hawaupati ila inawezekana wanaupata kwa njia tofauti na labda kuna mambo ambayo bado hayajaeleweka vizuri kwanini haujaenea kwa kasi ile ile kama ilivyokuwa Hispania, Italia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na China yenyewe ulikoanzia.

Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha kasi yake haiendi kwa kasi hivi. Binafsi nimeshtuka zaidi kuwa kwa siku mbili hizi idadi ya wagonjwa iliongezeka mara mbili. Nasubiria kuona namba mpya kutoka 88 zitatupeleka wapi. Kama ni kweli mtu mmoja aliyeambukizwa (ambaye hana dalili) anaweza kuambukiza karibu watu 40 basi namba yetu inaweza kuwa kubwa zaidi. Lakini pia kwa vile hata ambao hawaoneshi dalili baadaye wanaanza kuonesha dalili hizo basi wagonjwa wanaweza kuongezeka kwa kasi zaidi na kusumbua mifumo yetu ya afya.

Sasa tufanye nini?

Tayari hatua nyingi zilizochukuliwa zimesaidia lakini bado tunaona kuwa hata watu ambao wanatuambia tuchukua hatua wao wenyewe ni kama hawaelewi uzito wa janga hili na uwezekano wa tatizo hili kuendelea kwa muda. Nimesoma na kufuatilia maoni ya wadau mbalimbali na nimefuatilia hatua mbalimbali ambazo serikali imechukua hadi hivi sasa. Maoni yangu ni kuwa ni lazima tufikiri nje ya boksi; tufikirie nje ya boksi hilo kwa sababu mazingira yetu ni tofauti sana na nchi zilizoendelea. SIyo kwamba binadamu ni tofauti bali mazingira ni tofauti.

Hatuwezi Kuiga Yote Yanayofanywa na Nchi Tajiri

Mojawapo ya makosa makubwa ni wale wanaodhani kuwa wakiiga yanayofanyika hapa Marekani basi na sisi hali itakuwa hivyo hivyo. Mojawapo ya mapendekezo makubwa ni kuwa watu wanataka kila mtu akae nyumbani kwa angalau wiki mbili. Kwamba, tuiweke Tanzania nzima chini ya ‘lockdown’ kwa muda wa wiki mbili au zaidi. Hili ni rahisi kulisema kuliko kulifanya. Nitaeleza kwanini.
  • Nchi Tajiri zina uwezo wa kufunga nchi zao na wananchi wao bado wakawa salama. Hapa Marekani mojawapo ya hatua ambazo serikali imechukua kufanya maisha yawe rahisi kidogo ni kutoa fedha taslimu kwa raia wake wote (wenye kustahili). Kila mtu anapewa dola 1200 na mtoto anapewa dola 500. Huu ni mchango wa mara moja na unatarajiwa kurudiwa tena.
  • Mfumo wao wa mafao ye kukosa ajira (unemployment benefits) kwa kawaida ulikuwa unatoa karibu dola 360 hivi kwa kila mtu kwa wiki angalau 26. Lakini sasa hivi wameongeza dola 600 juu ya hilo. Hivyo, licha ya kupewa zile dola 1200 bado mtu aliyeomba fao la kukosa ajira atapata pia dola karibu 900 kila wiki kwa wiki angalau 26! Hii ni sawa na dola 24, 000 hivi kwa miezi sita!
  • Serikali imetoa pia mafao ya kusaidia biashara ndogo ndogo ambapo walipitisha kiasi cha dola bilioni 350 katika raundi hii ya kwanza. Fedha hizi makampuni yaliyoomba kama mkopo unaoweza kusamehewa inadaiwa kufikia jina zilikuwa zimeshakwisha na hakuna aliyepata kiasi chote alichoomba! Sasa hivi wanafikiria kuongeza kiasi cha fedha tena; sitashangaa kama haitofikia dola trilioni 1 ya kusisimua uchumi!
  • Kwa makampuni makubwa kuna fedha nyingi zaidi ambazo zinaenda kutolewa ili kusaidia yasianguke na kusababisha hali ya uchumi ambayo sasa ni mbaya kuwa mbaya zaidi.
  • Mataifa haya Makubwa yana mfumo mkubwa wa mahospitali ambayo yameongezewa uwezo mkubwa zaidi ikiwemo vifaa n.k.
  • Matumizi ya jeshi katika kusaidia kuongeza uwezo wa hospitali na vituo vya afya. Tumeona hili China na Marekani na nchi nyingine ambapo majeshi yao yameenda kuongeza nguvu kwenye taasisi za kiraia. Marekani kwa mfano Brigedi ya Uhandisi (Army Corps of Engineers) ambayo ndio msimamizi mkubwa wa ujenzi unashirikiana kujenga hospitali za medani (field hospitals) kwa haraka na kuwapa uwezo hospitali ambazo zimezidiwa wagonjwa.
Hiyo ni mifano michache tu ya kuonesha ni jinsi gani hatuwezi kumuiga tembo kwa kila kitu vinginevyo tutapasuka msamba. Na wazo la kuifunga nchi nzima kwa wiki hata tatu tu ni wazo linalohitaji kufikiriwa vizuri zaidi. Naamini katika hili Magufuli yuko sahihi. Hata hivyo, naamini kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya.
  • Kwa vile virusi hivi vinaenezwa kwa haraka katika mikusanyiko mikubwa ya watu hasa kwa vile virusi vya koronoa vinaweza kukaa hewani kwa angalau dakika kadhaa kiasi kwamba mtu anaweza kupiga chafya akaondoka na mtu mwingine akapita pale pale na kupumua hewa ile. Haitoshi basi kukaa mita moja tu; tupunguze kabisa mikusanyiko. Makanisa na Misikiti yatangaze kusitisha ibada zao kwa angalau wiki mbili au tatu. Hii itapunguza kusambaa kwa haraka maana hadi hivi sasa hii ndio mikusanyiko mikubwa zaidi inayofanyika nchini. Watu wasali kama Elia Mtishbi! Uamuzi wa kusitisha ibada za hadhara si wa serikali ni wa taasisi za dini.
  • Ni wakati wa JWTZ kushiriki moja kwa moja kwenye kudhibiti wagonjwa na wale wanaofuatiliwa. Tuna kambi za jeshi nchi nzima, wakati umefika kwenye hizi kambi jeshi litengeneze “field hospitals” au kambi za mahema kwa ajili ya kuwahifadhi wale ambao wamekuwa karibu na watu wenye korona ili kuwaangalia kwa karibu na kukata uwezekano wa kuambukiza jamii. Wakati wasafiri tunawaweka karantini kwa sababu hatujui kama wameshaambukizwa au wamekutana na mtu mwenye ugonjwa ni vizuri familia za wagonjwa 88 na wale watu wao wa karibu waangaliwe kwenye kambi hizi za kijeshi ukizingatia pendekezo la tatu. Hadi hivi sasa hatujaona kuhusika kwa jeshi kunakofaa na kutosha.
  • Serikali badala ya kutoa mabilioni ya hela kwa kila mtu huku wakikaa nyumbani itenge kiasi cha fedha kwa ajili ya kuzilisha na kuhudumia familia ambazo zitakuwa kwenye uangalizi wa siku kumi na nne. Naamini hiki kitakuwa ni kiasi kidogo sana kulinganisha na gharama ya kuifunga nchi nzima. Uthubutu wa Rais Magufuli kujenga SGR, Nyerere Hydropower Dam na mengine unatudokeza kuwa hatosita kutenga kiasi cha fedha kwa jambo kama hili itakapolazimu na ninaamini inalazimu sasa. Jeshi na Mageresha (ambayo yapo kila wilaya na mkoa) wanaweza kutumika kuandaa vyakula na mahitaji mengine kwa familia hizi.
  • Wakati huo huo tuongeze uwezo wa kupima, kutenga/karantini na kutibu na kufuatilia maambukizi. Hii ndio kubwa ya kudhibiti. Bila kupima na kutenga itakuwa vigumu sana. Hatuwezi kuwaweka watu wote mahospitali, hizi nchi kubwa tu hazijaweza sisi inatubidi tufikirie nje ya hilo.
  • Kwa vile watoto wako majumbani badala ya mashuleni, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Wizara ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Mawasiliano (na nyingine husika) wafikirie namba ya kuanza kutoa masomo kwa njia ya radio na televisheni kwa ajili ya watoto. Vipindi vya TV na Radio viangaliwe ili watoto wasikae nyumbani tu. Hatuwezi kugawa laptop na kutoa elimu kwa kila shule nchi nzima (wenzetu matajiri wanaweza) sisi turudi kule kule kwenye radio na TV. Tusiwanyime watoto haki ya kupata elimu.
  • Tuwe wabunifu kukabiliana na janga hili tusifuate tu yaliyomo vitabuni. Tuangalie mazingira yetu.
Kwa vile tumeamua Watanzania waendelee kufanya kazi na maisha yao basi na serikali iwapunguzie mazingira ya kupata maambukizi hayo. Tusije kudhani tunaweza kufunga uchumi wetu na watu wakabaki salama na nchi ikawa salama. Sasa hivi huko tunakokwenda hakuna msaada wa wajomba zetu wala wakubwa zetu maana na wenyewe kwao kunaungua. Ni lazima tujiangalie sisi wenyewe na ikibidi tutumie nafasi hii kutengeneza bidhaa ambazo zinahitajika zaidi sasa duniani na kutoa nafasi kwa wajasiriamali wetu nao kunufaika huku jamii zao na familia zao zikiwa salama.

Nilisema mwanzoni katika Makala ya kwanza kuwa tukisubiri mgonjwa wa kwanza tutakuwa tumechelewa; ni kweli tumechelewa lakini hatujachelewa sana. Bado tunaweza kudhibiti. Tusizidi kuchelewa mwisho tutashindwa kabisa. Tusiende kuomba kwenye makundi kama manabii wa Baal! Tutaangamia huku tunalia! Nilisema kwenye Makala ya pili ya Bahati Nasibu ya Magufuli. Hadi hivi sasa bado hajaliwa; inaonekana inalipa lakini ni lazima ilipe kwa watu vinginevyo Watanzania watalipa kwa machozi.

Tunapoenda kumwomba Mungu kwa siku hizi tatu; tutumie siku hizi tatu pia kuja na mikakati mikubwa inayoonesha kweli imani yetu kwa Mungu inatufundisha kuwa Mungu ametupa nafasi ya kudhibiti. Tusije kufikirie Mungu atashusha moto toka mbinguni na kuiteketeza korona! Labda ni jukumu letu sisi kutengeneza mifereji ya maji, na kumwagia maji halafu tuache Mungu awe Mungu. Tukumbuke kuwa huyu Mungu hana upendeleo na wala hajali sura za watu na wala hapokei rushwa! (Rumi 2:11).

Niandikie: [email protected]
What if kama manabii wetu ni Wa Baal? 😂😂😂😂😂 situtapoteza muda tu?
 
Tatizo lipo tena sio dogo ni kwamba tuna serikali ambayo kwake ushauli inaona kama ni kutukanwa kwa sasa inch Nyingi duniani zimesitisha makodi kwenye vibiashara vya wajasilia Mali lakini Hapa kwetu hilo ni ndoto wao kipaumbere ni pesa kwanza mengine mtajua wenyewe je kwa Hali hii utapona?
 
Mzee kuchelewa ni kuchelewa tu acha kuuma na kupulizia! Serikali ya CCM ilileta kiburi tangu mwanzoni hadi kule Bungeni wakamzomea Mchungaji Msigwa aliyeleta hoja ya kujadili issue ya Corona kama dharura. Nilianzisha thread hio.

Tukubali tulifanya makosa hatukutaka kuwasikiliza waliokuwa na mawazo tofauti na sisi, tukiamini hawana akili na hawana uwezo wa kutuelekeza cha kufanya! Leo tuko wapi? Kiburi chetu kiko wapi?

Again, I call upon CCM regime, tuunganishe nguvu, tuweke siasa kando, tuweke majivuno kando, tuweke ukabila kando, tuitishe ule umoja wa kitaifa! Tuwasikilize wengine pia na tuyaheshiimu na mawazo yao pia. Kwa pamoja tutaweza.
Mkuu kupambana na Corona kunahitaji ushirikiano na mshikamano wa wananchi kwa ujumla.
Katika vitabu vitakatifu imeandikwa kuwa Mungu atawaumbua na kuwafadhaisha wale wenye kiburi,majivuno na wanajiona wana nguvu nyingi .
Kama wangekuwa wanafundishika serikali ingekuja na bageti ya Corona sio ile inayojadiriwa sasa Dodoma,kana kwamba Corona siyo tishio kwa uchumi na ustawi wa wananchi.
Sioni kama wanaweza hata kukusanya nusu ya mapato ya bajeti iliopita.Na hata ukusanyaji huo utahitaji kumuangamiza Corona kwanza, kwani dynamics za uchumi dunia nzima zimebadirika.
Weka utu kwanza,jali watu ndio wanatengeza vitu
 
Watasingizia sisi ni nchi masikini duniani hatuwezi kumudu maisha ya watu hao,hapo ndipo utakpo jiuliza,sensa huwa zinafanyika za kazi gani,bajeti zipangwa za nini ?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Tunaweza kumwomba Mungu atusaidie kutuepusha na janga la ugonjwa wa korona. Kama binadamu na watu wenye imani tunaelewa wazi kuwa mwisho wa siku mambo yote yako mikononi mwa Mungu. Tunapojiachilia katika huruma na wema wake tunakiri uwezo na uwepo wake lakini pia tunakiri ubinadamu wetu. Kumwomba Mungu hakuwezi kuwa kosa. Nchi zote zilizoendelea ambazo nazo zimepigwa na majanga ya korona watu wake nao wanamwomba Mungu na kumlilia.

Kila siku hapa Marekani kuna watu wanakutana kwenye njia ya simu, Facetime, Skype na njia mbalimbali za mawasiliano kumwomba Mungu. Japo kwenye majimbo mengi ibada za hadhara zimesitishwa lakini siku ya Pasaka kwa mfano kwenye Jimbo Kuu Katoliki la Detroit Askofu Mkuu aliadhimisha Misa Takatifu akiwa na watu wachache tu kwenye Kanisa Kuu. Misa ile ilirushwa moja kwa moja na televisheni na kwenye Facebook na Youtube na sisi waumini tulifuatilia tukiwa majumbani mwetu. Mungu yupo mahali popote.

Kwa Wakristu kuna mstari unaosema kuwa “Wakutanapo wawili au watatu kwa Jina langu mimi nipo kati yao” (Mathayo 18:20). Mstari huu una maana kuwa uwepo wa Mungu katika ibada hauitaji wingi wa watu. Utendaji wake hauitaji mkusanyiko mkubwa wa watu. Katika maandiko tunakutana na mifano kadha wa kadha wa jinsi Mungu alivyoweza kutenda kwa kumtumia mtu mmoja au wawili tu au watu wachache lakini akafanya makubwa.

Mojawapo ya masimulizi makubwa yenye kusisimua katika Biblia ni kile kisa cha Elia Mtishbi. Baada ya watu wa Israeli kudanganywa na Manabii wa Baal, Elia akaamua kuwapa changamoto. Akawaambia kuwa yeye ni mtu mmoja tu aliyebakia akiwa ni Nabii wa BWANA na Baal alikuwa na “manabii” 450. Elia akataka kuwaonesha yupi ni Mungu wa kweli basi; yule mwenye Nabii mmoja aliyebakia au yule mwenye nabii 450 wenye mbwembwe nyingi. Simulizi hili linatuonesha kuwa Elia akawapa nafasi manabii wa Baali kumwomba Mungu wao atekekeze (aunguze) kwa moto sadaka walizoziandaa kwenye madhabahu.

Manabii wale 450 walianza kumwomba mungu Baal na kulia na kujichanja huku wakipiga kelele. Kwa kuwaangaliwa kwa nje unaweza kuamini walikuwa na imani zaidi, na kwa kelele na vilio vyao mungu wao angewasikiliza. Elia aliwadhihaki na kuwaambia labda waongeze sauti inawezekana mungu wao alikuwa amelala! Waliposhindwa ndipo Elia akaingia kazini yeye peke yake na bila sala ndefu tena katika jambo lisilowezekana (aliwaagiza waandalizi wake wamwagie maji zile sadaka mara tatu (alichimba na mfereji wa maji kuzizunguka kabisa). Na kwa sala fupi kabisa na yenye nguvu akamwita Yehova Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo. Alipomaliza tu sala yake na kabla ya kusema “Amina” Moto ulishuka toka mbinguni na kutetekeza sadaka zile na kuyakausha maji yale!

Ndipo watu wakajua kuwa Yehova ndiye Mungu. Unaweza kusoma kisa hiki kwenye 1 Wafalme 18:20-40.

Ndugu zangu, Rais Magufuli yuko sahihi kutaka Watanzania waliombee Taifa na hata bila yeye kutaka hivyo nina uhakika watu wenye imani wamekuwa wakiliinua taifa letu na watu wetu kwa dua na sala mbalimbali. Huu ni wajibu wetu; lakini siyo tu sisi dunia nzima inamlilia Mungu kumwomba. Hili haliwezi kuwa jambo baya wala la kudharau.

Na inawezekana Mungu ameshaanza kujibu sala na dua hizi. Mwanzoni mwa baa hili kulikuwa na hofu kuwa ugonjwa huu utaathiri zaidi Afrika labda kuliko bara nyingine lolote. Hata sasa maambukizi na vifo kwenye bara letu hayaendani na wingi na mtawanyiko wa watu wetu.

Pamoja na hayo bado Mungu anatupa nafasi ya kujiandaa zaidi. Haitoshi kumwomba Mungu na sisi bila kufanya au kuchukua hatua makini. Tayari taifa limechukua hatua mbalimbali ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sahihi. Baadhi ya hatua zimechelewa sana na matokeo yake ndio tunaona maambukizi yakiongezeka badala ya kupungua. Na yameongezeka kwa haraka zaidi siku hizi za karibuni na tusipoangalia yanaweza kuongezeka zaidi ndani ya siku chache (kama tutafuata kama ilivyotokea nchi nyingine).

Lengo la Mikakati

Sasa hivi, lengo la mikakati yoyote inayochukuliwa na nchi ni kupunguza kasi ya maambukizi, kudhibiti wagonjwa wapya, na kuwalinda watu ambao bado hawajaambukizwa. Katika kupunguza kasi ya maambukizi ndipo panalala kazi kubwa ya kuidhibiti korona. Unaposoma habari mbalimbali duniani kwenye nchi zinazohangaika na ugonjwa huu sehemu kubwa ni kuwa kasi ya maambukizi mapya bado ni kubwa au ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba mifumo ya afya haikuweza kujiandaa nayo. Chukulia kwenye jimbo la Michigan ambako ninaishi.

Mgonjwa wa kwanza wa Corona alitangazwa Machi 10. Leo hii (mwezi mmoja na wiki moja baadaye) jimbo hili lina wagonjwa karibu 30,000 na vifo zaidi ya 2000! Na hapa ni pamoja na ukweli kuwa tumekuwa chini ya “lockdown” kwa karibu mwezi mzima! Watu wengi hawaendi kwenye makazini, michezo, hakuna ibada za hadhara n.k Na inadaiwa hatua zilizochukuliwa Michigan ni miongoni mwa hatua kali zaidi kuchukuliwa na jimbo lolote la Marekani.

Sasa, kama kwenye taifa hili lilioendelea hivi, lenye raslimali za kila namna watu wake wanaambukizwa kwa kasi hivi na kufa itakuwaje kwetu? Bila ya shaka kuna mambo (factors) ambazo zinafanya ugonjwa huu kuwa wa hatari zaidi kuliko nyumbani. Siyo kwamba watu wetu hawaupati ila inawezekana wanaupata kwa njia tofauti na labda kuna mambo ambayo bado hayajaeleweka vizuri kwanini haujaenea kwa kasi ile ile kama ilivyokuwa Hispania, Italia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na China yenyewe ulikoanzia.

Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha kasi yake haiendi kwa kasi hivi. Binafsi nimeshtuka zaidi kuwa kwa siku mbili hizi idadi ya wagonjwa iliongezeka mara mbili. Nasubiria kuona namba mpya kutoka 88 zitatupeleka wapi. Kama ni kweli mtu mmoja aliyeambukizwa (ambaye hana dalili) anaweza kuambukiza karibu watu 40 basi namba yetu inaweza kuwa kubwa zaidi. Lakini pia kwa vile hata ambao hawaoneshi dalili baadaye wanaanza kuonesha dalili hizo basi wagonjwa wanaweza kuongezeka kwa kasi zaidi na kusumbua mifumo yetu ya afya.

Sasa tufanye nini?

Tayari hatua nyingi zilizochukuliwa zimesaidia lakini bado tunaona kuwa hata watu ambao wanatuambia tuchukua hatua wao wenyewe ni kama hawaelewi uzito wa janga hili na uwezekano wa tatizo hili kuendelea kwa muda. Nimesoma na kufuatilia maoni ya wadau mbalimbali na nimefuatilia hatua mbalimbali ambazo serikali imechukua hadi hivi sasa. Maoni yangu ni kuwa ni lazima tufikiri nje ya boksi; tufikirie nje ya boksi hilo kwa sababu mazingira yetu ni tofauti sana na nchi zilizoendelea. SIyo kwamba binadamu ni tofauti bali mazingira ni tofauti.

Hatuwezi Kuiga Yote Yanayofanywa na Nchi Tajiri

Mojawapo ya makosa makubwa ni wale wanaodhani kuwa wakiiga yanayofanyika hapa Marekani basi na sisi hali itakuwa hivyo hivyo. Mojawapo ya mapendekezo makubwa ni kuwa watu wanataka kila mtu akae nyumbani kwa angalau wiki mbili. Kwamba, tuiweke Tanzania nzima chini ya ‘lockdown’ kwa muda wa wiki mbili au zaidi. Hili ni rahisi kulisema kuliko kulifanya. Nitaeleza kwanini.
  • Nchi Tajiri zina uwezo wa kufunga nchi zao na wananchi wao bado wakawa salama. Hapa Marekani mojawapo ya hatua ambazo serikali imechukua kufanya maisha yawe rahisi kidogo ni kutoa fedha taslimu kwa raia wake wote (wenye kustahili). Kila mtu anapewa dola 1200 na mtoto anapewa dola 500. Huu ni mchango wa mara moja na unatarajiwa kurudiwa tena.
  • Mfumo wao wa mafao ye kukosa ajira (unemployment benefits) kwa kawaida ulikuwa unatoa karibu dola 360 hivi kwa kila mtu kwa wiki angalau 26. Lakini sasa hivi wameongeza dola 600 juu ya hilo. Hivyo, licha ya kupewa zile dola 1200 bado mtu aliyeomba fao la kukosa ajira atapata pia dola karibu 900 kila wiki kwa wiki angalau 26! Hii ni sawa na dola 24, 000 hivi kwa miezi sita!
  • Serikali imetoa pia mafao ya kusaidia biashara ndogo ndogo ambapo walipitisha kiasi cha dola bilioni 350 katika raundi hii ya kwanza. Fedha hizi makampuni yaliyoomba kama mkopo unaoweza kusamehewa inadaiwa kufikia jina zilikuwa zimeshakwisha na hakuna aliyepata kiasi chote alichoomba! Sasa hivi wanafikiria kuongeza kiasi cha fedha tena; sitashangaa kama haitofikia dola trilioni 1 ya kusisimua uchumi!
  • Kwa makampuni makubwa kuna fedha nyingi zaidi ambazo zinaenda kutolewa ili kusaidia yasianguke na kusababisha hali ya uchumi ambayo sasa ni mbaya kuwa mbaya zaidi.
  • Mataifa haya Makubwa yana mfumo mkubwa wa mahospitali ambayo yameongezewa uwezo mkubwa zaidi ikiwemo vifaa n.k.
  • Matumizi ya jeshi katika kusaidia kuongeza uwezo wa hospitali na vituo vya afya. Tumeona hili China na Marekani na nchi nyingine ambapo majeshi yao yameenda kuongeza nguvu kwenye taasisi za kiraia. Marekani kwa mfano Brigedi ya Uhandisi (Army Corps of Engineers) ambayo ndio msimamizi mkubwa wa ujenzi unashirikiana kujenga hospitali za medani (field hospitals) kwa haraka na kuwapa uwezo hospitali ambazo zimezidiwa wagonjwa.
Hiyo ni mifano michache tu ya kuonesha ni jinsi gani hatuwezi kumuiga tembo kwa kila kitu vinginevyo tutapasuka msamba. Na wazo la kuifunga nchi nzima kwa wiki hata tatu tu ni wazo linalohitaji kufikiriwa vizuri zaidi. Naamini katika hili Magufuli yuko sahihi. Hata hivyo, naamini kuna mambo mengine tunaweza kuyafanya.
  • Kwa vile virusi hivi vinaenezwa kwa haraka katika mikusanyiko mikubwa ya watu hasa kwa vile virusi vya koronoa vinaweza kukaa hewani kwa angalau dakika kadhaa kiasi kwamba mtu anaweza kupiga chafya akaondoka na mtu mwingine akapita pale pale na kupumua hewa ile. Haitoshi basi kukaa mita moja tu; tupunguze kabisa mikusanyiko. Makanisa na Misikiti yatangaze kusitisha ibada zao kwa angalau wiki mbili au tatu. Hii itapunguza kusambaa kwa haraka maana hadi hivi sasa hii ndio mikusanyiko mikubwa zaidi inayofanyika nchini. Watu wasali kama Elia Mtishbi! Uamuzi wa kusitisha ibada za hadhara si wa serikali ni wa taasisi za dini.
  • Ni wakati wa JWTZ kushiriki moja kwa moja kwenye kudhibiti wagonjwa na wale wanaofuatiliwa. Tuna kambi za jeshi nchi nzima, wakati umefika kwenye hizi kambi jeshi litengeneze “field hospitals” au kambi za mahema kwa ajili ya kuwahifadhi wale ambao wamekuwa karibu na watu wenye korona ili kuwaangalia kwa karibu na kukata uwezekano wa kuambukiza jamii. Wakati wasafiri tunawaweka karantini kwa sababu hatujui kama wameshaambukizwa au wamekutana na mtu mwenye ugonjwa ni vizuri familia za wagonjwa 88 na wale watu wao wa karibu waangaliwe kwenye kambi hizi za kijeshi ukizingatia pendekezo la tatu. Hadi hivi sasa hatujaona kuhusika kwa jeshi kunakofaa na kutosha.
  • Serikali badala ya kutoa mabilioni ya hela kwa kila mtu huku wakikaa nyumbani itenge kiasi cha fedha kwa ajili ya kuzilisha na kuhudumia familia ambazo zitakuwa kwenye uangalizi wa siku kumi na nne. Naamini hiki kitakuwa ni kiasi kidogo sana kulinganisha na gharama ya kuifunga nchi nzima. Uthubutu wa Rais Magufuli kujenga SGR, Nyerere Hydropower Dam na mengine unatudokeza kuwa hatosita kutenga kiasi cha fedha kwa jambo kama hili itakapolazimu na ninaamini inalazimu sasa. Jeshi na Mageresha (ambayo yapo kila wilaya na mkoa) wanaweza kutumika kuandaa vyakula na mahitaji mengine kwa familia hizi.
  • Wakati huo huo tuongeze uwezo wa kupima, kutenga/karantini na kutibu na kufuatilia maambukizi. Hii ndio kubwa ya kudhibiti. Bila kupima na kutenga itakuwa vigumu sana. Hatuwezi kuwaweka watu wote mahospitali, hizi nchi kubwa tu hazijaweza sisi inatubidi tufikirie nje ya hilo.
  • Kwa vile watoto wako majumbani badala ya mashuleni, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Wizara ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Mawasiliano (na nyingine husika) wafikirie namba ya kuanza kutoa masomo kwa njia ya radio na televisheni kwa ajili ya watoto. Vipindi vya TV na Radio viangaliwe ili watoto wasikae nyumbani tu. Hatuwezi kugawa laptop na kutoa elimu kwa kila shule nchi nzima (wenzetu matajiri wanaweza) sisi turudi kule kule kwenye radio na TV. Tusiwanyime watoto haki ya kupata elimu.
  • Tuwe wabunifu kukabiliana na janga hili tusifuate tu yaliyomo vitabuni. Tuangalie mazingira yetu.
Kwa vile tumeamua Watanzania waendelee kufanya kazi na maisha yao basi na serikali iwapunguzie mazingira ya kupata maambukizi hayo. Tusije kudhani tunaweza kufunga uchumi wetu na watu wakabaki salama na nchi ikawa salama. Sasa hivi huko tunakokwenda hakuna msaada wa wajomba zetu wala wakubwa zetu maana na wenyewe kwao kunaungua. Ni lazima tujiangalie sisi wenyewe na ikibidi tutumie nafasi hii kutengeneza bidhaa ambazo zinahitajika zaidi sasa duniani na kutoa nafasi kwa wajasiriamali wetu nao kunufaika huku jamii zao na familia zao zikiwa salama.

Nilisema mwanzoni katika Makala ya kwanza kuwa tukisubiri mgonjwa wa kwanza tutakuwa tumechelewa; ni kweli tumechelewa lakini hatujachelewa sana. Bado tunaweza kudhibiti. Tusizidi kuchelewa mwisho tutashindwa kabisa. Tusiende kuomba kwenye makundi kama manabii wa Baal! Tutaangamia huku tunalia! Nilisema kwenye Makala ya pili ya Bahati Nasibu ya Magufuli. Hadi hivi sasa bado hajaliwa; inaonekana inalipa lakini ni lazima ilipe kwa watu vinginevyo Watanzania watalipa kwa machozi.

Tunapoenda kumwomba Mungu kwa siku hizi tatu; tutumie siku hizi tatu pia kuja na mikakati mikubwa inayoonesha kweli imani yetu kwa Mungu inatufundisha kuwa Mungu ametupa nafasi ya kudhibiti. Tusije kufikirie Mungu atashusha moto toka mbinguni na kuiteketeza korona! Labda ni jukumu letu sisi kutengeneza mifereji ya maji, na kumwagia maji halafu tuache Mungu awe Mungu. Tukumbuke kuwa huyu Mungu hana upendeleo na wala hajali sura za watu na wala hapokei rushwa! (Rumi 2:11).

Niandikie: [email protected]
Umezunguka mno mzee.

Taarifa ya kuandika paragraph 5 fupi fupi wewe umeandika kama gazeti ya Uhuru au Majira.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inaonekana inaogopa kusitisha mikutaniko kwenye nyumba za ibada ndio maana wanadai wamesitisha madrasa na Sunday school huku ikitaka ibada ziwe fupi kumbe hata ibada zikiwa fupi maambukizi yanaweza kutokea tu.
By probability chance wakaingia wenye coronavirus infection katika kundi la watu 50, wakawaambukiza 5, misa ikaisha , wakatawanyika. hao watano nambie watawaambukiza wangapi. Ni ujinga eti ibada iwe fupi, stupid!
 
Formula ya kufanya Maombi ya kitaifa iko Wazi, samehe, sahau, tubu. Leo hii tunataka tufunge kwa ajili ya Corona wakati wananchi wamejaa majeraha mioyoni mwao? Wamepoteza ndugu, wameondoshwa kazini isivyo haki, hakuna salary increments na mengineyo!

Unataka Wafunge? Kweli? Wakifunga kweli tutaambulia laana Maana Mungu hadhihakiwi, hao wa kwenye Bible wote walikua kitu kimoja!

Hivi wale ambao ndugu zao wako mahabusu kwa makosa ya uonevu leo hii ukiwaambia Wafunge, watakuelewa? Si watabadilisha Maombi yawe ya kulaani?

Tutubu kwanza, twende mbele za Mungu tukiwa na mikono misafi! Tutubu kwa uongo, uonevu, usengenyaji na vifo vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine tumehusika na Mungu wa Mbinguni atasikia Maombi na mafungo yetu, kinyume na hayo tutajipalia mkaa mikononi mwetu. Take it from me. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Kiongozi wetu wa nchi
Niliona unaandika vitu vya maana lakini unaanza kuharibu na siasa zako. Basi kwa formula hiyo corona itatumaliza huku hatujapata muafaka.

Unafikiri ukitaka huo utakaso ili Mungu atusikie tutaishia kutibu hayo majeraha tu? Vipi wewe, yule aliyeua ndugu yake kishirikina? Vipi uzinzi unaoendelea? Ndio maana tunaingia kwenye toba kwaajili ya yote hayo.

Hebu tupambane na Corona tuachane na propaganda za maccm na Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tumekuwa watu wa kulaumu kila kitu, kwanini uilaumu serikali kwamba haizuii watu wasikusanyike badala ya wewe mwenyw kujifungia tu ndani????

Tahadhari zote znajulikana ila tu bado hatuchukui kisa serikali haijalazimisha duuuuh 😂😂.
Kila mmoja akiwa muangalifu au akichukua tahadhari tutakuwa salama, tuache lawama zisizo msingi, chukua hatua.
 
Niliona unaandika vitu vya maana lakini unaanza kuharibu na siasa zako. Basi kwa formula hiyo corona itatumaliza huku hatujapata muafaka.

Unafikiri ukitaka huo utakaso ili Mungu atusikie tutaishia kutibu hayo majeraha tu? Vipi wewe, yule aliyeua ndugu yake kishirikina? Vipi uzinzi unaoendelea? Ndio maana tunaingia kwenye toba kwaajili ya yote hayo.

Hebu tupambane na Corona tuachane na propaganda za maccm na Chadema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na mtazamo wako, wala sipingi ila mtazamo wangu ndio huyo, na hakuna pahala nimetaja uccm wala uchadema!
 
Watanzania tumekuwa watu wa kulaumu kila kitu, kwanini uilaumu serikali kwamba haizuii watu wasikusanyike badala ya wewe mwenyw kujifungia tu ndani????

Tahadhari zote znajulikana ila tu bado hatuchukui kisa serikali haijalazimisha duuuuh [emoji23][emoji23].
Kila mmoja akiwa muangalifu au akichukua tahadhari tutakuwa salama, tuache lawama zisizo msingi, chukua hatua.
Tuko hivyo mkuu, ambaye hajafanikiwa lawama kwa baba yake kuwa hajamsomesha, baba nae analalamika hivyo hivyo. Tukianza kutambua nafasi yangu na yako tutaacha kulaumiana na kuchukua hatua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom