Alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda kwa Pierre Mzee wa Liquid ni udhalilishaji na kinyume cha haki za binadamu

Alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda kwa Pierre Mzee wa Liquid ni udhalilishaji na kinyume cha haki za binadamu

By @professorjaytz | 👉Isoookey Isoookey @pierelikwidi, Hata Mbuyu ulianza kuota mdogo Mdogo Kama MCHICHA, Na ili Dhahabu iweze kung’aa ipasavyo ni lazima ipitie kwenye MOTO Mkali sana, Keep ya Head UP! Ni Marufuku kabisa kukata TAMAA na Mapambano lazima yaendelee, PIGA kazi Zaidi na Zaidi kwa kutumia hicho Kipaji chako na Neema ambayo Mungu ameiweka Ndani yako, kwani yeye ndiye anayejua Fungu la kila mmoja wetu na yeye ndiye anayejua kesho yetu, Endelea Kumtanguliza Mungu kwa kumuomba, Kumtukuza na kumshukuru kwa kila Jambo Utaendelea kuwa JUU, Utaendelea kuwa MAWINGUNI🔥🔥 CHIIIIIIIIII, Everybody SAY YEEEAH😂😂 Nawatakia wote JUMAPILI Njema🙏🏻🙏🏻
 
Udharirishaji uliofanywa na Makonda jana kwa Pierre Liquid, si jambo la heri. Kwamba watu wa 'hovyo' kama Pierre ndio wanao pata umaarufu. Huu ni uwivu wa hali ya juu kama si udhahifu aliouonyesha jana.

Mbona yeye alitangaza 'nusu bei', kwa hiyo hakuona kwamba huu ni ulevi? Huyu mtu anatabia fulani ambayo inaudhi na inakera. Kila mtu anayo njia ya kujipatia ridhiki. Pierre si mlevi wa kutupwa kama vile tunavyoambiwa, lakini amejipatia umaarufu, na anatengeneza pesa. Sasa we Makonda anawashwa na nini?

Nimegundua kitu. Katika psychology, kuna kitu kinaitwa 'defence mechanism', kwamba mwili au wewe mwenyewe unafanya kitu ili kuficha udhaifu fulani. Makonda hana vyeti, na tunajua historia yake ya elimu hadi kutumia jina la mtu, na hili amewahi kukili mwenyewe nyakati fulani jinsi alivyokuwa anaitafuta elimu hadi kuchoma mkaa huko Mbezi Luis. Sasa jana kwa kuwa ilikuwa ni harambee ya Jokate Mwegelo ya 'Tokomeza Zero', akakumbuka historia yake ya elimu, akahisi huenda watu wanamuwaza yeye, hivyo akatafuta pakufichia udhahifu wake, ikawa ni kwa Pierre. Huu si uungwana hata kidogo.

Pierre si Amba Rutty kwamba ameigiza video za ngono. Pierre siyo Jambazi wanaotusumbua na kuhatarisha amani yetu. Pierre si kahaba kwamba anajiuza. Pierre si malaya kwamba anaeneza magonjwa. Pierre si nabii wa uongo kwamba anatapeli watu kama ilivyo kwa wengi. Pierre si mwanasiasa anayefanya mikutano ya siasa. Pierre anatafuta ridhiki kama yeyote yule. Anatumia kipaji na umaarufu wake. Umaarufu katika dunia hii ndiyo pesa. Au tatizo ni kwamba ametangazwa na kuwa maarufu kuliko yeye? Tunajua, hapendi mtu amzidi umaarufu. Amwache Pierre atafute pesa.

Tunaomba Makonda atoe boriti ndani ya jicho lake kabla yakutoa kibanzi katika jicho la Pierre. Na unapomnyooshea mwenzako kidole, hakikisha vyako viko safi.

NB: Mods,naomba huu uzi usiunganishwe na mwingine wa tukio la jana. Haya ni maoni huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piere baada ya kulewa umaarufu, akihojiwa na mwandishi wa habari alimwita "taka taka" "we ni taka taka tu".
Leo waandishi wa habari wanapewa nasaha kuachana na Pierre ambaye RC amemtambua kama "mtu wa hovyo hovyo". Karma is Bitch
Japo watanzania bado wako upande wa Pierre, na hii ni bahati isiyo ya kawaida...kumfurahisha mtanzania!....Pierre achukue hii kama alert juu ya namna gani anapaswa kua na adabu na ukarimu pasi na kujikweza kisa tu ni maarufu na anapata deals...watanzania ni species za ajabu sana..watamshusha na kumpuuza hatoamini.
Natamani ningesikia mwanzo mpk mwisho kwann amemwita mwandishi hivyo...
 
Huwa simuungi mkono Makonda lakini jana kaongea point. Nchi imekuwa ya wajinga hii, mambo yakipumbavu ndio tunayapa kipaumbele.

Kwanza huyo Pierre ni msanii wa kitu gani? Yan Taifa linaacha kujielekeza katika hoja zinazojenga na kuendeleza vizazi vijavyo, elimu, afya na ustawi wa jamii, tunakaa kusifia pombe na kukuza majina ya walevi.

Hapa jirani Kenya tu hawana trend za kipumbavu hivi. Juzi niliona Msanii wa Kenya anashangaa wa Tz wanavyo comment kwenye post za watu maarufu "wanauza uchi na wanawake kwenye magroup" ndiko taifa la wapumbavu likikofika na wafuasi wa vitu hivi wengi na vitoto vya sekondari na chuo wanaolia kila siku hawana ajira.

Kesho kabinti kamemaliza form 4 kanafungua akaunti ya kukaa uchi akiuza **** kwasababu tu ukifanya hivo Nchi hii ndio una trend

Naunga mkono kabisa kemeo la Makonda

Dumelang
Haya yatabaki kuwa maon yako lakin ukweli ni kwamba bia ni eneo linalochangia mapato ya nchi kwa kiwango kikubwa.Hata wew mwenye unaweza ukawa mlevi wa ngono ambao hauna faida yoyote kwa taifa.Ulevi wa pombe unafaida kwa taifa.
 
Ni upepo tu utapita. Heshima na adabu si kwa wadogo hata wakubwa zetu. Ingekuwa Nigeria huyu Pierre angepewa support ili awe mlipa Kodi mzuri kwenye kazi zake za marketing na advertising.

Hi ndio akili ya viongozi wetu tunahitaji hili heshima la wasiokuwa na ajira tuliexport nchi za watu lakini akili zao ni kuwaza kuongeza ugumu wa kuwapa passport vijana. Hatuwezi kuendelea kwa kukandamizana hivi.

Konki Ana trend Sana hi pengine inawaumiza wanaopenda sifa na umaarufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anafanya kazi ipi nzuri?Hiyo isiyokuwa na job description na performance indicator?Huyu Bwana ni zero zero kweli.Konki wa watu kamkosea nini zaidi ya wivu wa kitoto na kutopenda maendeleo kulikochagizwa na family background.Huyu bwana siku cheo chake na hao wanaompa kiburi wakidondoka atapata taaabhu kweli kweli.Yaani kuna watu watamf#$%@a
Angekuwa anatoka kanda pendwa angeheshimika. Kwakuwa anatoka kanda ambayo haipendwi ndio ivyoooooo
Tanzania ya viwanda
Maendeleo hayana chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piere baada ya kulewa umaarufu, akihojiwa na mwandishi wa habari alimwita "taka taka" "we ni taka taka tu".
Leo waandishi wa habari wanapewa nasaha kuachana na Pierre ambaye RC amemtambua kama "mtu wa hovyo hovyo". Karma is Bitch
Japo watanzania bado wako upande wa Pierre, na hii ni bahati isiyo ya kawaida...kumfurahisha mtanzania!....Pierre achukue hii kama alert juu ya namna gani anapaswa kua na adabu na ukarimu pasi na kujikweza kisa tu ni maarufu na anapata deals...watanzania ni species za ajabu sana..watamshusha na kumpuuza hatoamini.

piere aliambiwa na yule mwandishi azingue tu.. tafuta full video.. aliambiwa aigize anamfukuza
 
Kwa kweli mkuu,sioni kwa nini huyu RC anaonekana kuchukizwa na umaarufu wa Pierre tena hadharani
Ni upepo tu utapita. Heshima na adabu si kwa wadogo hata wakubwa zetu. Ingekuwa Nigeria huyu Pierre angepewa support ili awe mlipa Kodi mzuri kwenye kazi zake za marketing na advertising.

Hi ndio akili ya viongozi wetu tunahitaji hili heshima la wasiokuwa na ajira tuliexport nchi za watu lakini akili zao ni kuwaza kuongeza ugumu wa kuwapa passport vijana. Hatuwezi kuendelea kwa kukandamizana hivi.

Konki Ana trend Sana hi pengine inawaumiza wanaopenda sifa na umaarufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani umaarufu ni nini??

Na nani anapaswa kuwa maarufu??

Hivi Kim Kardashian si maarufu??..do you think ni mtu wa maana sana dunia hii??

Acheni chuki nyie..kuwa maarufu sio lazima iwe kwa uzuri..hata kwa ubaya mtu anaweza kuwa maarufu

Pablo escobar si alikuwa maarufu??
mshamba tu huyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah Ile kita itamshushia sana Piere kipato chake, kuvunjiwa mgataba ni ngumu labda wamlipe kama waliandikishiana, Ila oshu kubwa ni kwamba ni ngumu tena kupata dili zingine, hata kama kuna waliokua wanamfikiria kumpa dili wataahirisha, pia unaarufu wake utashuka kwa kasi.
 
View attachment 1058576"watu kama wakina Pierre sijui,watu wa hovyo hovyo ndio wanakua maarufu watu wa maana hawajulikani,tunajenga jamii ya watu gani?"

Haya ndio maneno ya Makonda wakati anahutubia kwenye tamasha la tokomeza zero Kisarawe,lililofanyika jana Mlimani City,ambalo pia Pierre alikuwa moja kati ya watu waliohudhuria.

Hivi mtu kama Pierre kuwa maarufu yeye inamuuma nini? anaposema ni mtu wa hovyo katika lipi? kati ya Pierre na hao wasanii wake ambao daily wanshinda makahamani kwa kesi za hovyo hovyo,wanatukanana mitandaoni live, wanavujisha picha za ngono mitandaoni, wanabadili wanawake/mabwana kila uchwao na bado anawahusudu na kuwaona wa maana nani ni wa hovyo sasa?

Muache mzee wa watu aingize kipato chake kihalali, ilimradi havunji sheria za nchi.
IMG-20190331-WA0017.jpg
 
Back
Top Bottom