Alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda kwa Pierre Mzee wa Liquid ni udhalilishaji na kinyume cha haki za binadamu

Alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda kwa Pierre Mzee wa Liquid ni udhalilishaji na kinyume cha haki za binadamu

Yapata masaa machache, baada ya kusambaa kauli ya mheshimiwa Makonda aliyoitoa katika hafla ya Tokomeza zero!

mjadala Umepinduka, badala kujadili mengi yaliyosemwa pale, watu wameshikia bango "kauli ya makonda kwamba waache kushadadia mambo ya hovyo"
Nimewasiliana na Mheshimiwa makonda asubuhi hii; kasema walimwelewa Vibaya! Hakuwa na maana mbaya juu ya Pierre! kasema hata yeye anampenda Pierre,

alichokisema pale kwenye hafla, Alimaanisha waandishi Wa habari kuliko kujikita kuwapa promo na airtime watu wanaoendekeza anasa na starehe, wafanye na mambo yenye tija kuliinua taifa, kasisitiza, alimaanisha kwamba waandishi wasigemee kutoa promo kwa watu wa starehe tu, waelimishe pia umhimu Wa ELIMU bora kwa watoto wetu"

Pierre kwasababu ni rafiki ake na ni mtani wake, alitoa mfano lakini hainamaana hampendi Pierre!

anatambua mchango Wa Pierre katika uhamasishaji wake Mkubwa alioonesha katika mechi ya mashindano ya AFCON TZ vs UG.

anatoa rai kwa wanasiasa na wanaharakati kushikamana kwa ajili ya maendeleo ya Taifa, waache kudandia mambo yasiyo na tija!

Kasema kwa mfano; Ile hafla yalisemwa mambo mengi sana na ya msingi, lakini kashangaa kuona imetapakaa taarifa hiyo moja tu!

Ingawa pia mheshimiwa pamoja na kutambua kuwa " BAD STORY KWA WAANDISHI KWAO NDIYO GOOD STORY "
Lakini Makonda kasisitiza wananchi Tujikite kwenye mambo ya Msingi!..
Anaomba radhi kwa Pierre na wananchi kwa Ujumla! Mjadala umekwisha!!
INABIDI ASEME MWENYEWE. KAMA JAMAA ALIKATAA KUMUOMBA MSAMAHA LATE RUGE, SEMBUSE PIERRE. HUYU JAMAA KAKUSUDIA 100%
 
We mkojolea nyuma mimi na wewe nani hana kazi za kufanya? Wewe mtoto mdogo uliekuja kuomba namna yakusevu kodi ya nyumba tena umelipa laki 2 miez 6, unaniita mie sina kazi? Respect ur rotten ass pls

Dumelang
Amakweli wajinga mnazidi kuongezeka

In God we trust
 
Comedian
Huwa simuungi mkono Makonda lakini jana kaongea point. Nchi imekuwa ya wajinga hii, mambo yakipumbavu ndio tunayapa kipaumbele.

Kwanza huyo Pierre ni msanii wa kitu gani? Yan Taifa linaacha kujielekeza katika hoja zinazojenga na kuendeleza vizazi vijavyo, elimu, afya na ustawi wa jamii, tunakaa kusifia pombe na kukuza majina ya walevi.

Hapa jirani Kenya tu hawana trend za kipumbavu hivi. Juzi niliona Msanii wa Kenya anashangaa wa Tz wanavyo comment kwenye post za watu maarufu "wanauza uchi na wanawake kwenye magroup" ndiko taifa la wapumbavu likikofika na wafuasi wa vitu hivi wengi na vitoto vya sekondari na chuo wanaolia kila siku hawana ajira.

Kesho kabinti kamemaliza form 4 kanafungua akaunti ya kukaa uchi akiuza **** kwasababu tu ukifanya hivo Nchi hii ndio una trend

Naunga mkono kabisa kemeo la Makonda

Dumelang

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mtu anadharau sana. Hata kuna kikao kimoja katika ziara yake ya Dar aliwahi kumkashifu dada mmoja mtendaji wa manispaa kuwa ni kichaa. Ni kiongozi pekee anayeweza kufanya na kusema lolote baya lakini asiguswe.

Sent using Jamii Forums mobile app
wala usijali mkuu... kwa yote aliyowafanyia na anayoendelea kuwafanyia watu, nakwambia huyu dogo baada ya awamu ya "baba yake" kwisha atakuwa anakimbikimbia hovyo kama digidigi.
na hapo ndipo kutakuwa na kilio cha kusaga meno!
 
View attachment 1058576"watu kama wakina Pierre sijui,watu wa hovyo hovyo ndio wanakua maarufu watu wa maana hawajulikani,tunajenga jamii ya watu gani?"

Haya ndio maneno ya Makonda wakati anahutubia kwenye tamasha la tokomeza zero Kisarawe,lililofanyika jana Mlimani City,ambalo pia Pierre alikuwa moja kati ya watu waliohudhuria.

Hivi mtu kama Pierre kuwa maarufu yeye inamuuma nini? anaposema ni mtu wa hovyo katika lipi? kati ya Pierre na hao wasanii wake ambao daily wanshinda makahamani kwa kesi za hovyo hovyo,wanatukanana mitandaoni live, wanavujisha picha za ngono mitandaoni, wanabadili wanawake/mabwana kila uchwao na bado anawahusudu na kuwaona wa maana nani ni wa hovyo sasa?

Muache mzee wa watu aingize kipato chake kihalali, ilimradi havunji sheria za nchi.
Tuna nchi nq viongozi wa ajabu sana. wivu tu baada ya kuona Match ya TzVs UG Piere kamfunika kinyume na matarajio yake. Yaani Poere ambaye hakutoa dau kwa wachezaji ndio awe maarufu kuliko yeye na Baba yake??
 
In my opinion, RC Makonda has committed a very serious insubordination in relation to the Vice President's fair comments on Pierre's contributions towards Taifa Stars' victory. Nani anayalinda haya,yenye udhalilishaji hata kwa wakuu wetu wa nchi?
Kila mtanzania amebaki amepigwa na butwaaa kubwa sana

In God we trust
 
Jokate anajuta sana kumualika daah!kamharibia sana yaani!huyu baba naona kafanya kusudi ili watu wasijadili contents ya jokate wamjadili yeye,kashindwa kuondoa Zero DSM kafeli kila kitu for sure


Huyu baba Hamna kitu kabisaa...Jana nimezidi kumdharau !!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu mie mwenyewe hapa nilitegemea kusikia hiyo mikakati ya ONDOA Zero Kisarawe but mwsho wa siku naona mambo yalienda mrama,its my hope kweli Jokate atakwa anajuta kwa kilichotokea.

Sent from Nokia 7 Plus
 
Mimi huwa sikaelewi kale kalevi sawa,lakini pia huyu mkuu wenu wa mkoa anawalakini kidogo.Sitaki kuongea mengi lakini nchi hii imekosa bahati yakuwa na viongozi wenye hekma.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23]
IMG-20190331-WA0046.jpeg


Jr[emoji769]
 
Ama kweli 'shibe mwana malevya, njaa mwana malegeza'

Dah unaweza vipi kumdhihaki binadamu mwenzako kiasi hiko bila ya hata kukosa aibu.
 
Tuwe fair bana huyo Pierre kachangia nini katika ushindi wa Taifa Stars?

Comment ya Makamu wa Rais isi elevate ujinga tunaofanya Watanzania. Makamu wa Rais alikuwa katika Excitement yani tukio linalojaza furaha. Katika tukio kama lile mtu anaweza ongea chochote. Lakin isiwe sababu kuwa kumtrend Pierre ni jambo zuri.

Hakuna ambacho taifa na vizazi vyetu vinajifunza kwa huyo Pierre zaidi vijana wengi wanahsi kufanya upumbavu ndio sehemu yakuwa maarufu na ku earn cheap money.

Kesho tutawakuza na Mashoga, na vijana wataiga. Kati hapa mmeona walichokuwa wanafanya akina ambaruty, ili tu apate umaarufu, atrend apate pesa. Ndio wapo mabint kibao wanatamami wafanye hayo watrend, yjnajenga taifa gani?

kwa jicho pana tunachofanya ni upumbavu

Dumelang
Kwahiyo unayuaminisha bila kuacha chembe ya mashaka kuwa una dharau mawazo ya mama Samia?

In God we trust
 
Back
Top Bottom