Alichohoji Profesa Muhongo ni kama bei ya umeme itakuwa nafuu kuanzia siku ya kwanza au baada ya kurudisha gharama za uwekezaji?

Alichohoji Profesa Muhongo ni kama bei ya umeme itakuwa nafuu kuanzia siku ya kwanza au baada ya kurudisha gharama za uwekezaji?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Leo baadhi ya wabunge wamemshukia Profesa Muhongo na kudai ni heri darasa la saba Msukuma na Kibajaji kuliko PhD holder.

Naye Spika Ndugai akasema ni vema maprofesa wakawa wanajipanga vizuri kabla ya kuongea kuepukuka changamoto za akina Kibajaji kwani uprofesa ni muhimu kwenye kufundisha na utafiti lakini siyo siasani hasa Bungeni.

Imenibidi nifuatilie kujua huyu Muhongo anayeshambuliwa ameongea nini?

Kumbe Muhongo hajasema umeme wa maji mbaya bali inachukua muda mrefu sana kurejesha gharama ndio akahoji labda kama bei nafuu itaanza kutumika day one bila kujali pay back period.

Mantiki yake ni kuwa bei inaweza kuwa kubwa hadi mradi utaporudisha gharama zake, ambayo huwa ni miaka mingi mbele

CCM mko peke yenu bungeni hakuna wa kumsingizia.
 
Kwa Hiyo umejaribu kuwaza pia Kwamba kama ungekuwa mradi wa Umeme wa Gesi ungekamilika basi wenyewe Gharama za mradi zingerudi Mapema zaidi Kulinganisha na huu wa Maji???

Ukweli utabaki Ukweli tu kuwa Prof. Katika hili alikosea kidogo, maana LENGO KUU KWA WANANCHI NI KUPATA UMEME KWA BEI NAFUU NA WALA SIYO KWENDA NA WAKATI ETI UMEME WA GESI HUKU WANANCHI WANAUMIA.
Hata hivyo Nchi zilizoendelea bado zinatumia Maji kama chanzo Kikuu Cha Umeme!!!

Naweza kukubaliana Naye Prof. sehemu moja tu Kwamba Vyanzo mbalimbali vya umeme viendelee kutengenezwa ili kama Wakati wa Matengenezo kusiwe na uhaba Au upungufu wowote wa Umeme nchini
 
Kibajaji nae anajilinganisha na Muhongo,
Kweli hii ni hatari sana. Sijawahi ona, ukiangalia hata anachoongea ni porojo tu. Hakina hata research yoyote, hakina data, yaani ni vitu vya kufikirika tu.
Kibajaji hana tofauti na Ndugaye
 
Bado tuna safari ndefu kwani watu kama nyinyi bado mpo wengi wenye mawazo ya kutetea huo mradi wa MNHP
 
Huo ni mradi wa muda mrefu iweje day one Bei ya umeme iwe nafuu?Kama hajasoma masuala ya biashara si anyamaze.huyu muhongo ni bomu elimu yake haina msaada kwa watz
 
Hoja dhaifu mno kutoka kwa Prof! Kwani kuna mradi gani ambao ukikamilika hatutowajibika kulipa gharama?

Nilitegemea maprof kama hawa ndio wangekuwa watetezi wa kuwekeza kwaajili ya vizazi vijavyo! Hawa wazee wameshikwa na ma lobbyists walambe 10% zao na vizazi vyao na si Watanzania kwa ujumla.
 
Bado akajifungie, ndiyo aje tena.
Maana bei haita badirika kwa namna anayodhani yeye, bali itakuwa ikiongezeka kwa a token to cushion inflation.
 
Hoja dhaifu mno kutoka kwa Prof! Kwani kuna mradi gani ambao ukikamilika hatutowajibika kulipa gharama?

Nilitegemea maprof kama hawa ndio wangekuwa watetezi wa kuwekeza kwaajili ya vizazi vijavyo! Hawa wazee wameshikwa na ma lobbyists walambe 10% zao na vizazi vyao na si Watanzania kwa ujumla.
Prof kaongea kama mwanataaluma siyo mwanasiasa.
 
Leo baadhi ya wabunge wamemshukia Prof Muhongo na kudai ni heri darasa la saba Msukuma na Kibajaji kuliko PhD holder.

Naye Spika Ndugai akasema ni vema maprofesa wakawa wanajipanga vizuri kabla ya kuongea kuepukuka changamoto za akina Kibajaji kwani uprofesa ni muhimu kwenye kufundisha na utafiti lakini siyo siasani hasa bungeni.

Imenibidi nifuatilie kujua huyu Muhongo anayeshambuliwa ameongea nini?

Kumbe Muhongo hajasema umeme wa maji mbaya bali inachukua muda mrefu sana kurejesha gharama ndio akahoji labda kama bei nafuu itaanza kutumika day one bila kujali pay back period.

Mantiki yake ni kuwa bei inaweza kuwa kubwa hadi mradi utaporudisha gharama zake, ambayo huwa ni miaka mingi mbele

CCM mko peke yenu bungeni hakuna wa kumsingizia!

kwa hiyo bwawa likianza kutumika, umeme utapanda bei kufidia hiyo investment cost?
Investment inalenga

1.,Umeme wa uhakika

2.Umeme wa kuuza nje

3.Gharama za umeme za sasa ndio basis ya kuweka ukubwa na kujua lini litakuwa limelipa

4.Uhakika wa umeme unapeleka kuwa na same rates kwa miaka mingi sana....

Swali la Prof ni la kijinga kwa umri wake na elimu yake

wewe hapa hauwezi kujibu; kamuulize prof
 
anayepanga bei ni Serikali sitarajii aweke bei kubwa kwani alishafanya analysis ya mradi.
 
Back
Top Bottom